Mimi swali langu ni moja tu kwa wanaotetea, je huyu mwanamke anaejiunga na hiyo michezo na mnasema ni sehemu ya kujiwekea akiba, hii pesa ya kutoka kila siku au kila week anaitoa wapi kama hana biashara ama ajira yoyote ya kumuingizia kipato? Kuna mtu huko juu anasema wanaume hawatimizi mahitaji ndo maana wanawake wanaamua kujiingiza huko ili kutafuta kipato, swali langu ni lile lile tu hela ya kutoa huo mchango sijui mnaita marejesho ataitoa wapi kama hana biashara ama kazi yoyote ya kumuingizia kipato? Nachoamini hawa wanawake wanatumia pesa za matumizi ya familia wanayoachiwa na waume zao wanaziingiza huko kwa kuchomoa kidogo kidogo baadae inaonekana kama mwanaume hahudumii vizuri familia yake. Mbaya zaidi wanaenda kukopa huko bila kumshirikisha Mume wake na anachokifanyia hizo pesa hakieleweki matokeo yake ni kuleta shida kwenye familia tu. Siamini kwenye kwenye mambo za vikoba kabsa kwenye maisha yangu, nikimwona mtu anajihusisha na hizi mambo hua namwona kama mtu aliekosa focus ya maisha kwasababu kama uko serious na biashara ama mradi wowote nenda kakope Bank... utaratibu wa kibenki unakulazimisha uwe smart na mwenye discipline na project unayotaka kuifanya.