Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Ndiyo. Alikuwa kiongozi mzuri na kama binadamu wa kawaida pia alikuwa na mapungufu yake. Uuzaji wa kiholela wa mashirika ya umma, mauaji ya Mwembechai (alishalijutia hili) na tamaa yake ya kujilimbikizia mali mpaka ikabidi watu wapige makelele kwenye baadhi ya mambo (mf. Kujimilikisha mradi wa makaa wa Kiwira) kunaonyesha udhaifu wake. Ila aliiacha nchi ikiwa na neema kuliko alivyoikuta. Apumzike kwa amani kiongozi huyu mzalendo, msomi na mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza [emoji1545][emoji1545]