Historia|Wasifu: Je, Benjamin William Mkapa ni nani hasa?

Elezeeni basi na mazuri ya viongozi walio hai...
Yanaelezwa na kuandikwa Kama history sema akifa ndio wengi tunapata chanzo au chachu ya kuyajua mengi zaidi ukitafuta na ukitaka kuyajua yapo Sana na yanazungumzwa Sana sema tuu hata we mwenyew haujapata sababu ya kutaka kuyajua akifa maybe unaweza unapata chanzo Cha kuyajua Kama unavyoona kwa mkapa
 
We ni lofa mwenzetu wala usiwe hofu,kuzaliwa siku moja na kufa ivo ivo.
 
U
UNGESEMA.AKIWAHAII HAYÀ NINGEFURAHIA SANAAÀ HAPO AONI ULICHOANDIKAA NEXTYM.TUJIFUNZE KUSIFIA MTU AKIWA HAI
 
Magu akiondoka ataliliwa kuliko Mwana Lupaso


Siku akiondoka Mzee Ally Hassan kama atatangulia kabla yetu… tutaeleza mengi sana mazuri juu yake

Huyu Mwinyi ndio aliichomoa Nchi kwny Mfumo wa kijima wa Ujamaa na akalifuta Azimio la Arusha bila ya kuomba kibali Butiama… Uchumi wa Soko Huria aliousimamia Genious Mkapa uliwezekana kwa kuwa kuna Mtu alishaweka Mazingira

Tutawaeleza kuwa Mkapa aliweza kuboresha maisha ya Watumishi wa Umma kwa kuwa kuna mtu alishapitisha 'fagio la chuma'1994 kwa kupunguza Wafanyakaz wengi aliorithi ili wabaki wachache Wanaoweza kuboreshewa Maslahi

Tutaeleza alipotutoa Mzee Mwinyi 1985
Elezeeni basi na mazuri ya viongozi walio hai...
 
Binafsi naona jamaa alikuwa na exposure kubwa sn...Cv yake inajieleza pia nadhani Mwl Nyerere alimuandaa Ben kuwa rais kwa mda mrefu sn baada ya kuona uwezo wake
 
Hapo ndo umeongea ushuzi huyo tuliyenaye kafanya kitu gani kipya?au unampigia kampeni?
 
Nakubali kwamba Mkapa was the brightest president after Mwalimu lakini hizo sifa ulizompa kutokana na uanzishwaji wa hayo yote, mengi hayakutokana na akili yake bali external force!!

TRA-- hii ilianzishwa awamu ya Mwinyi, Mkapa amekuja kula matunda yake tu! Uanzishwaji wake ni external force ya Mabeberu kupitia Structural Adjustment Program!

TAKUKURU-- Hii haikuanzishwa na Mkapa bali na Kikwete! Mkapa alianzisha TAKURU, yaani Taasisi ya Kuzuia Rushwa, JK ndo akaanzisha ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa!

Na kabla ya hapo sio kwamba hatukuwa na taasisi kuhusu hayo mambo, hell no... we'd Kikosi cha Kuzuia Rushwa!

TCRA-- Yes, Mkapa

NSSF- Yes, Mkapa lakini sio kwamba alianzisha kitu kipya kwa sababu kabla ya hapo ilikuwa inaitwa NPF. Mabadiliko ya kiuchumi ambayo na yenyewe yaliasisiwa naMabeberu yalilazimisha kufanya mabadiliko ya mifuko ya hifadhi za jamii!!

TPA-- Yes, Mkapa lakini hakuna kipya saaaaana hapo ambacho kilianzishwa na Mkapa kwa sababu TPA ilikuja kuchukua nafasi ya THA, na kupewa mamlaka ya kusimamia na bandari za maziwani ambazo hapo kabla hazikuwa chini ya THA!

Lakini wakati Mkapa anafanya hayo ambayo positive, kwa mkono wa kushoto akaisaliti TPA baada ya kuuuza container terminal kwa TICTS! Sitasahau siku uncle anarudi home anaonekana yupo down ile mbaya; namuuliza kulikoni, akaishia kusema "Yaani Mkapa!"

Siku ya pili ndipo akanijuza kwamba jana yake TICTS walikuwa wamefanya bonge la sherehe la ku-break even only 10 months after acquiring the container terminal!!! Mbaya zaidi, kabla hawajamaliza mkataba wao wa kwanza, akawaongezea miaka mingine 10 wakati anajiandaa kuondoka madarakani!!

Bodi ya Utalii-- Hii ilianzishwa na Utawala wa Mwinyi ikichukua nafasi ya Tanzania Tourist Corporation.

TAA-- Yes, Mkapa but it wasn't something new kwa sababu ilianzishwa ku-take over majukumu ya Kurugenzi ya Masuala ya Anga!

MKURABITA, TASAF, na MKUKUTA (uliisahau hii)-- Haya ni matunda ya Mabeberu wa IMF, WB, Paris Club na Donors wengine ambao walikubaliana kupunguza madeni kwa zile walizoita Heavily Indebted Poor Countries!

Mabeberu walitoa orodha ya nchi 38 including TZ ambazo zingesamehewa madeni kwa sharti kwamba wakishaonesha nia, basi kiasi cha deni kutoka kwa mabeberu kielekezwe kuhudumia wananchi badala ya kupeleka kwa mabeberu!

Mabeberu waliorodhesha maeneo walikotaka pesa zao zitumike, na ndipo ikaanzishwa Mkakati wa Kukuza na Kuondoa Umaskini (MKUKUTA)

Through MKUKUTA, serikali ya Mkapa na zingine ambazo zingefuatia zilitakiwa kuelekeza pesa za mabeberu kwenye: access to education (ndipo ikazaliwa Shule za Kata), access to health service (ndiyo inayotekelezwa leo na Magu), kupunguza umaskini wa kipato )ndipo ikaja TASAF, na hapo pia ndipo ikaja MKURABITA ambayo ilikuwa influenced na Professor Hernando de Soto!
 
Hii. Ndio point ya msingi

Naomba wote tukazie hapa[emoji3516]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…