Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Lilikuwa sio vazi rasmi bali ni umwanjomwanjo wa kutaka ujulikane kuwa unafanya kazi kwa wazungu. Kwengine lilikuwa uniform. Kwa Nyerere kama ilikuwa ni "official" au "un official" alikuja Dar na kaptura, sijui kuna tatizo lipi mnaloliona kama alikuja Dar na kaptura na hapo ndipo alipovuliwa hiyo kaptura, wazee waliovaa kaptura Dar walizivaa kwa occassion zake na si kila pahala na kila wakati kama ilivyokuwa kwa Nyerere, ndio lilikuwa vazi lake kabla ya kuvuliwa.

Kama ni usomi kuvaa kaptura kwa wakati huo basi tusikatae kama alikuwa hajavaa kaptura na tusikatae kuwa alivuliwa hizo kaptura na wazee wa Dar. Sioni cha kubisha ni nini hapo, whatever reasons may be the answer will remain to be kavuliwa kaptura na wazee wa Dar.
 
Naomba kukuuliza maswali...wewe ni muingereza,mjerumani au mfaransa? Mswahili ni mtu wa aina gani kwa tafsiri yako?
 
Ndivyo nnavyo amini, kuwa alikuja hajui kuvaa suruali na hao wazee wa Dar. ndio waliomfunda. Lakini Mohamed Said kishasema tuyaache haya tuchukuwe hii fursa adhim kujuwa ukweli uko wapi na porojo ziko wapi.

Kwa vile ni imani siwezi kukupinga maana wapo wanaoamini kabisa kuwa mwezi umetengenezwa kwa jibini na kuwa yupo kiumbe ambaye nusu ni mtu na nusu samaki!
 
Niweke sawa na kwa lugha rahisi kabisa isiyoleta utata na kubadilli mada. Mlima kilimanjaro upo Tanzania- Facts.
Kwanini Klimanjaro, kagera na Mbeya watu wanaelimu kuliko sehemu nyingine- yatakauwa matokeo ya research.

Baada ya hapo nifafanulie Pro-Nyerere ni akina nani na je ndio Pro-TANU?

Maiaka 10 iliyopita CCM ilikuwa madhalimu walio kandamiza waislam. Hiyo kauli imeishia wapi? si ndio ilikuwa kauli mbiu ya kuunga mkono falsafa ya 'Haki- Sawa' ya CUF. Lini uswahiba umerudi na ni kwa historia gani tofauti na ile iliyowakandamiza.

Kama source za Mohamed ni credible kama unavyodai, kwanini hakumhoji Fundikira, Rais wa EAMWS na right hand man wa Nyerere?
Kwanini hakumhoji mama Maria Nyerere kuhusu samaki aliopelekewa na marhum mzee Kiyate.
Kwanini hakumhoji marhum Rajab Diwani na Kitundu mapema(anasema alifariki masaa machache kabla ya mahojiano).
Kwanini hamhoji Sakim Ahmed Salim au Butiku wa NF

Kama ni credible, kwanini asikanushe au kukubali ushiriki wa Wanawake wa Pare katika kuanzisha chem chem ya kisiasa.
Kwanini asikanushe au kukubali uwepo wa harakati nje ya Dar es salaam kama Mwanza n.k
Kwanini majina ya akina Kisenge na Mashambo waliokuwa na hadhi katika TANU hayajitokezi
Kama ni credible kwanini asihoji namba za mtihani wizara husika
Kwanini asihoji madiwani wa kariakoo na gerezani waliobadili majina ya wapigania uhuru.
Kwanini asimhoji Silvano aliyeandika kitabu anacho kinukuu mara zote
Kwanini hakumhoji marhum Kawawa kama mwislam na mshiriki wa Nyerere, na mbona ushiriki wa Kawawa kama kiongozi katika vyama vya wafanyakazi hauonekani licha ya kuwa alikuwa Mwislam.

Soma post yangu ya awali, Mohamed anakiri kwa maneno kuwa 'anahadithia' maneno aliyosikia ili aweke sawa historia ya Waislam. Amekiri hivyo, sasa wewe unaposema ya Tanganyika umeitoa wapi zaidi ya Mohamed wenyewe.

Nina uhakika hujasoma vitabu vya Mohamed au makala zake. Nasema hivi kwasababu ametumia neno 'Inasemekana' mara nyingi sana. Credibility ya source zake iko wapi?

Unaweza kuwa na credible source halafu useme inasemekana!!! Inasemekana kutoka kwa nani maana yeye amesikia na hivyo ilipaswa aseme nimeambiwa. Ukishasema 'inasemekana' hiyo ni third party. Credibility ipo wapi.

Narudia, data na info zingine tunazofanyia kazi zimeletwa na 'credible' source kama aliyofanya Mohamed na Mdondoaji. Kwanini tulaumiwe kwa kuuliza au kuhoji.
 

Sasa kama unafahamu kwamba wazee wako wa dsm nao walikuiwa wanavaa kaptura isipokuwa walizivua ili waingie msikitini(hapa bila shaka walivaa kanzu na si suruali). Kwahiyo hoja ya Nyerere kuvaa kaptura inakuwa na uzito gani kama ilikuwa ndo uniform enzi hizo na hata wazee wako walivaa?

Kama mnajenga hoja ya Nyerere kuvaa kaptura ilikuwa ni ushamba au identity ya umanamba basi hata wazee wako wa dsm nao walikuwa manamba!
 

Yani wewe unatapatapa na historia ya wazee wa gerezani dsm, unafinyangafinyanga tu hata hueleweki.

Wazee wako waliokuwa wakivaa kanzu na misuli walipata wapi ujasiri wa kumfundisha Nyerere kuvaa suruali ambayo wao wenyewe hawaivai?
 

Sababu yote uiletayo iwe ndio hivyo, ukweli utabaki kuwa Nyerere kaja na Kaptura na ukweli utabaki wazee wa Dar ndio waliomvuwa kaptura amma kwa kupenda kwake amma kwa kutokupenda kwake, waliomuona akija Dar enzi hizo walimuona kaja na kaptura.

Sioni kuna tatizo lipi ikiwa Rais wa kwanza wa Tanzania ikijulikana kuwa alikuja Dar na kaptura? Tunaongelea Historia hapa na ushahidi wa picha nimeuweka hapo juu, wenzake wooote wakiwa na suruali yeye alikuwa kavaa kaptura. Rejea picha hapo juu. Na wala sijasema kuwa wazee wote wa Dar walikuwa hawavai kaptura, nimesema wako waliokuwa wakizivaa kwa (occassion) munasaba unaohusiana na kuvaa kaptura, amma makazini kwao amma kwa kujionesha kuwa wanafanya kazi kwa wazungu. Nyerere alikuja Dar na kaptura na wazee wa Dar wakamvuwa kaptura. Kuna uwezekano kuwa ilikuwa haina haja tena ya kuji "identify" kama ni mfanya kazi wa wazungu kwa maslahi ya kugombea madaraka, Jee, tatizo ni lipi? Historia ibaki kuwa historia ya ukweli na hili la kaptura lina ushahidi kamili.
 
Mohamed,
Mwalimu aliweka ndani watu wengi tu. Sio hao "Waislamu" wako uliowataja pekee. Kwa nini hauwataji hao wengine wenye majina ya kikristo nadhani ni katika kuimarisha hoja yako. Jana, katika kipindi cha WOSIA WA BABA, katika moja ya hotuba zake nzuri, Mwalimu alieleza jinsi alivyoifahamu TAA na hatimaye kujiunga nayo kupitia kwa mzee mmoja aliyeitwa Mwangosi na Mzee KaselaBantu ambao wewe hauwataji sana wala kuwapa uzito kama akina Sykes.
Punguza UDINI na chuki zako kwa Mwalimu. Historia ya nchi hii haikupi nafasi uibadili na hatimaye ukubali kwamba Mwalimu ndiye alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na hatimaye Tanzania. Labda nikuulize swali moja Mohamed; ulipata kuonana na kuongea na Mwalimu ukamuuliza juu ya haya unayoyasimulia?
 
Yani wewe unatapatapa na historia ya wazee wa gerezani dsm, unafinyangafinyanga tu hata hueleweki.

Wazee wako waliokuwa wakivaa kanzu na misuli walipata wapi ujasiri wa kumfundisha Nyerere kuvaa suruali ambayo wao wenyewe hawaivai?

Tazama picha hapo juu halafu useme ni nini hicho? Usiandikie mate na wino upo, wangapi katika hiyo picha waliovaa kaptura? mimi namuona mmoja tu "The Odd one out" Nyerere.
 
ujinga uliokuwepo hapa ni kutanabaisha dini na harakati za uhuru badala kutanabaisha watu, kama alivyo sema mwana kijiji, ukiongelea pwani wakati huo wengi wao walikuwa waislamu, mbeya wanyakyusa na wasafa, iringa wahehe na wabena, ukienda tabora wnyamwezi(wengine wakatoliki, waislamu, wapagani, morovian) nk
na kama nia ni kuongelea dhuluma, basi ni vizuri mtu aseme tu kwamba watu wa pwani walinyimwa shule, halafu watu wanao dai shule za agakhan zilikuwa za waislamu ni watu wa kuchekesha saana, kwani ile shule ni kwa ajili ya waismailia na si waislamu wa ngozi nyeusi, na hata leo hii ukienda pale utaona hao waisimaili ndio idadi kubwa 80% then wanafuatia wengine iwe mpagani, kafiri na muislamu (sunni au Shia)
ukija uelewa wa hao wazee wangu wa gerezani, labda kutokana na mawasiliano ya redio simu, tv, nk mtu alikuwa hajafika mza, tabora, pare, meru, moshi nk, yeye atakacho kiona kizuri ni kile anacho kiona na bahati mbaya au nzuri wazee wangu wa gerezani walikuwa wanawaona wana gerezani wenzao tu, ni sawa sawa na mtu mweupe/mzungu ambaye hajafika afrika anapokuwa na dhana kwamba weusi tunaishi juu ya mti.
baru baru anazungumzia mwandishi bora ni yule anaye weka reference, lakini hiyo reference inatakiwa isiwe biased, kwa mfano mwandishi kaongea na wazee wakee gerezani, je baada ya hapo kaenda kuhoji wengine? au sample yake ndio hiyo biased? halafu lengo lake ni nini? kurekebisha historia iliyo pindishwa au ambayo haija tambua mchango wa blah blah blah? je historia ya nchii hii haiwatambui sykes au Abdulwahid in particular? je historia haimtambui Bibi Titi?
 
Tazama picha hapo juu halafu useme ni nini hicho? Usiandikie mate na wino upo, wangapi katika hiyo picha waliovaa kaptura? mimi namuona mmoja tu "The Odd one out" Nyerere.
Faiza,
Naamini wewe ni zaidi ya hii hoja ya Nyerere na kaptula.
 
Faiza,
Naamini wewe ni zaidi ya hii hoja ya Nyerere na kaptula.

Mkuu hiyo picha imewekwa purposely, kuna watu hapa wanajaribu kwa kila njia kuonyesha kwamba Nyerere si lolote wala chochote bila wazee wa dsm.

Na mzee mohamed amesema hapa kwamba hoja ya Nyerere na kaptura ilianzishwa na wazee wa dsm baada ya uhuru ikiwa ni dhihaka kwa Nyerere kutokana na hisia kwamba Nyerere ana chuki na uislamu na waislamu.

Ni picha ngapi alipiga Nyerere pamoja na wapigania uhuru wengine lakini mbona haziwekwi hapa?

Anyway tuendelee na mambo mengine hili la kaptura linaeleweka na si hoja ya msingi.
 

Siku hizi kuna usemi unaosema pata pesa tujue tabia yako lakini zamani kulikuwa na usemi usemao fungua kinywa chako tujue upeo wako. Asante kwa kutujulisha wewe ni nani
 
Confidence comes not from always being right but from NOT FEARING TO BE WRONG: Peter T. mcintyre

 
Kwa vile ni imani siwezi kukupinga maana wapo wanaoamini kabisa kuwa mwezi umetengenezwa kwa jibini na kuwa yupo kiumbe ambaye nusu ni mtu na nusu samaki!

Kweli kabisa wala si uongo na picha huwepo za huo mwezi wa jibini kama ilivyo picha ya Nyerere hapo juu na kaptura katika kundi la watu waliovaa sarawili.
 
Asante Mungu JF inaelekea kurudi kwenye hadhi yake mijadala ya aina hii ndiyo ilinifanya nikajiunga na hili jamvi lakini kuanzia mwaka 2010 tulivamiwa na kundi la wahuni wasiopenda mijadala yenye afya bali matusi na kejeli.

Mzee Mohamed Said,Fundi Mchundo,Jasusi,FaidaFoxy,WildCard,Mzee Mwanakijiji,Mwita Maranya,Nguruvi3,Mag3 na wengine wote niliowasahau kwa bahati mbaya tafadhali sana tujiepushe na lugha za kuudhi,kejeli au matusi kwa faida ya mjadala.Niseme kweli nimejifunza mambo mengi kupitia kwenu na nina hakika wako wengi pia kupitia michango yenu wamefaidika sana.
 

Jamani kuna tatizo hapa, ishu sio kuyakataa anayosema Mohamed, ishu ni kuwa yapo mengi kuhusu taifa hili ambayo hatuyajui na yanajulikana na wachache miongoni mwetu. Basi kila mmoja aliandike lake analolifahamu ile wengine nao pia wapate kufahamu na pengine kujua Nyerere aliyakuasanyaje yote hayo pamoja akayazika na kujenga taifa lisilo na historia ndogondogo labda ambazo zisingetuwezesha kuwa wamoja kama tulivyo leo. Kama yapo yasemwe, yaandikwe tuyafahamu na eti si kumwambia mwingine asiseme kwa kuwa wewe hujayasema unayoyafahamu. Ajabu na kweli hata Bibi Titi Mohamed nae ametoa malalamiko ya kusahauliwa waliopigania uhuru kikwelikweli. Malalamiko yake yapo katika kitabu chake kiitwacho WANAWAKE WA TANU, kilichochapishwa na E&D VISION PUBLISHER kikiwa kimedhamioniwa na TGNP. Ukiemda E&D pale Afrika Sana Sinza utakipata au ukienda TGNP utakipata. Kama hata BIBI TITI alilalamika ni wazi kuna tatizo hapa. Kuna Tatizo kama lile alilolizungumza Jaramongi Odinga katika Not Yet Uhuru na kuna Tatizo kama lile alilochagiza Ngugi katika vitabu vyake A grain of Wheat na MATIGARI. Tufungue macho tuone ni jinsi gani tutaweza kuliingiza hili ndani yetu na kusema hili ni tatizo kisha tulitafutie tiba. Hatuwezi kulitibu kama hatujajua hili ni tatizo
 


Ngongo,

Tuko pamoja binafsi Insha Allah nitaeleza yote kama nilivyoyapokea kutoka
kwa wazee wangu na kama nilivyojifunza kwa lugha safi na ya kupendeza.

Naya fanya haya yote kwa heshima ya wazee wangu ambao wengi wametangulia
mbele ya haki.

Nina hakika wagelikuwa hai wangefurahi kuwa mwishowe historia yao ilikuja andikwa.

Mohamed
 

WC,

Sina chuki na Nyerere.

Nishasema hapa jamvini mara kadhaa kuwa ikiwa utachangia bila
kuwa umesoma kitabu changu utaja uliza mambo ambayo kama
ungelisoma kitabu usingeliuliza.

Kama umesoma na umesahau basi kirudie tena na nenda kwenye
faharasha.

Kwenye name index utayakuta majina mengi sana.

Ama kuhusu hilo la Nyerere kuwa rais wa kwanza wa nchi yetu vipi
nitalikataa?

Nalosema mimi ni kuwa ipo historia nyingine ambayo haikuandikwa
na kwa kuwa haifahamiki kuna sifa kapewa Nyerere si zake.

Hazimstahili na kusema hivyo si kuwa nina chuki na yeye.

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…