Hitimisho la Kesi: Licha ya hukumu kutolewa, hakuna official statement niliyokabidhiwa mahakamani

Mkuu moyo wako bado una amini katika familia

Oa mwengine mana utapata tabu
 
Nilikua sijui kumbe shetani ni mwanamke, ulioa shetani kiongozi
 
Hapa wanamjaza sifa ila siku watoto wakianza kuhangaika hawatajitokeza kumsaidia.

Na sio kwamba yeye ni msafi sana, na wala hata huyo anayemtuhumu hana ushahidi wa usaliti.

Muda mwingine wivu tu ndo uliompelekesha.
Mbona Kama unamtetea sana huyo mwanamke jeuri, au ndiyo wewe mwenyewe mke wa jamaa?
 
Ndugu yangu usiwasikilize watu humu, kama mkeo anaonyesha kujutia makosa yake msamehe mlee watoto wenu.
Usifikiri kwamba utakutana na aliyekamilika wanawake wote wana mapungufu.
Ila cha kufanya mwache ajutieee saaanaa, yani afikie hatua ya kukuomba msamaha mpaka apige magoti tena mbele ya wazazi. Yani aombe msamaha mpaka alie machozi. Usimkubalie kirahisi rahisi. Na wewe usimuonyeshe kuwa unamuhitaji onyesha kuwa umesha move on. Mzungushe kwa miezi kadhaa au hata mwaka ndio umrudie tena kwa masharti yako.
Nakuhakikishia atajirekebisha na hatarudia tena upuuzi wake.

Msamehe tu na mtalea watoto wenu kwa amani na wewe atakuheshimu sana. Hayo maamuzi ya kukubali kumuacha yamempa funzo kubwa tu hatarudia tena upuuzi wake.
Narudia tena usiwasikilize watu humu ndani, huyo ni mkeo unamjua na yeye anakujua. Sikiliza moyo wako na samehe saba mara sabini
 
Kama ulivyosema asiwasikilize watu humu
UKIWEMO WEWE NA HUU USHAURI WAKO
 
Utuletee mrejesho na mkirudiana,. Usituonee aibu tutakusapoti tena
Ahahahah...mdogo angu, mimi mrejesho nitaleta tu, sema sababu si kupewa support, sababu ni ku share lakin ku appreciate mchango wa mawazo , imenisaidia sana ni vile tu siwez sema ila humu licha ya utani na kebehi na vijembe, kuna watu unaona kabisa wako seriously concerned na ishu unaleta mezani, na unafanyia kaz ushauri na unaona unakusaidia. Hivyo nami najua mrejesho naouleta ,unawasaidia na wengine pia, lengi si kuungwa mkono bali kupata mawazo mbadala
 
Huu uzi siku usoma kutokana na ubize, ndio nime maliza Sasa hivi itoshe kusema mchungaji hasha uriwi namna ya kuishi na mfugo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…