Hitimisho la Kesi: Licha ya hukumu kutolewa, hakuna official statement niliyokabidhiwa mahakamani

Hitimisho la Kesi: Licha ya hukumu kutolewa, hakuna official statement niliyokabidhiwa mahakamani

Kwa mtazamo mnaweza kuona ni sawa lakini sio sawa.

Kumbuka alikwenda kuwachukua watoto, wale watoto washakuwa na ufahamu na utambuzi. Anataka awatengenezee picha gani watoto?

Katika malezi ya watoto kuna vitu tunatakiwa kutokuviendekeza.
Kwakifupi hakuna kitu mpaka sasa nimefanya ili kumkomesha yeye. Hata kwemda na gari mpya ,lengo halikua kumshtua, na wala hakukua na plan ya mimi na yeye kuonana naye
 
Hii process ya mahakamani inamchakato mrefu. Kama ni wakristo huwa wanaanzia huko kanisani au baraza la kata kwa ajili ya usuluhisho. Kama wangekuwa wanapendana wasingefika mahakamani ambako ni hatua ya mwisho ya kuvunja ndoa. Kama mwanamke kafikia hatua ya kufungua kesi mahakamani, ina maana anamaanisha kuvunja hiyo ndoa, ni vizuri maamuzi yake yahezhimiwe ili asije akaleta tabu baadae.
Exactly. Tumepita huko kote kabisa.

  • kaenda kwa mjumbe
  • tukakalishwa chini na wachungaji
  • akaenda dawati la jinsia
  • tukarudishwa kikao cha familia
  • akaenda baraza la usuluhishi la kata

HUKU KOOTE NILITOKA MSHINDA, HAKURIDHIKA

  • akanitia ndani kwa hila
  • nikatoka, akaenda mahakamani

HATA KAMA TUSEME NI HASIRA, KWA MCHAKATO HUU, LAZIMA ANGEKUA NA MUDA WA KU THINK TWICE
 
Hukumu hio mimi naona mwanamke kacheza mchezo jamaa asiipate ndio hivyo ukiachwa achika ushapewa ulichotaka kubariana na ulichokitaka
Ujue , nilipokua Day care kwa dogo, nikaomba apigiwe simu niongee nae ili nirusiwe kutoka na mtoto, nilipomsalimia tu , swali lake la kwanza likawa "baba xx, ulikuja kufuata ile hukumu?"
 
Kwani we unataka talaka? Maana ni kama mkeo hataki talaka. All in all wanaume epukeni masingo maza si mnaona huyu anambusu mzazi mwenzie.
Sikuitaka talaka from day 1. Nilimpenda mke wangu, na ndio maana hata siku ile usiku nimemchapa makofi, baada ya kukimbia na muda unalwenda, ni mimi ndio nilijipeleka polisi saa 6 za usiki kutoa taarifa kuwa "nimegombana na mke wangu na amekimbia nyumban haomekan ni masaa mawili sasa, nina hofu asije akapata tatizo huko aliko" wakasema acha namba zako za simu, nikaondoka, nilimtafuta sana, mpaka nilipopata simu toka kwa mjumbe.

Nimefanya kila jambo kuzuia kuvunjila kwa ndoa.

Ila nilipoona mwenzagu anakaza mwendo kuvunja, bas nikaona hiz one sided efforts hazitafaa kitu, nikaamua kumkubalia. Hivyo kwasasa NAITAKA TALAKA KWA MOYO MMOJA KABISA.

na kwanza toka aondoke nyumban, ninaona changes kubwa sana. SIJAWAHI KUKOSA KABISAAA PESA. Kuna mirad nilikua nawaza kuifanya ma sikua naweza, ila kwasasa naona kabisaaa Im changing for better.

Acha aende tuuu
 
Mkuu naomba nikushauri kitu hapa
Nakuomba sana tena sana; USIKUBALI KURUDIANA NA HUYO MWANAMKE.
Ni kweli tunavumilia mengi kwenye ndoa lakini kwa mliko fika hutakiwi kurudi nyuma
Kama alikusaliti na bado akaenda mahakamani na kusingizia yote hayo sijui unapata wapi ujasiri wa kupata hata wazo la kumrudia???
Kuhusu watoto asikudanganye mtu, watakua na watakuwa vile mwenyezi Mungu alivyowapangia (fate). Kwani ikitokea ukafa hawatakua?? Nani anaijua kesho???
Kwanza kuna ndoa watu wanalazimisha kuishi pamoja ili walee watoto lakini visa vya hizo ndoa ndo zinawaharibu watoto kabisa bora hata wangeachana.
Kama ukikaza fuvu na kutumia hisia badala ya akili ukarudi niseme tu RIP in advance.
NB: niko kwenye ndoa kwa miaka 8 sasa, tuna watoto watatu na ndoa yangu haina changamoto so far
Nimekuelewa vizuri. Na naomna ni clarify, SIJAPATA WAZO LA KURUDIANA NA MTU.
nimeleta tu mrejesho katika namna ya uwazi sasa sijui kwanini watu wamenielewa vibaya like nataka kumrudia au she has got an upper hamd to lure me back under her life. She has got no influence ovee me at all
 
Sawa sawa mkuu. Ni kweli ule mwenendo wa kesi yule hakim alikua anaandika kwa mkono na kila mtu aliusaini mwishoni, so wakasema utachapwa ndio tupatiwe
Huyo karani anatengeza miaya ya Rushwa Toka February hadi Sasa,pia hili jambo ni gumu,hivyo Huenda wanavuta muda kwamba mnaweza kufuta maamuzi ya mahakama,mkarudiana! Hao watoto wananiuma kama vile wajomba zangu,sio maisha haya!
 
Sijajua hata anataka kufanyia nini hyo Divorce peper, Au kuna sehemu unaweza kuombea kazi?

Hapo ilikua alie omba talaka ndo awe na kihere here cha kudai hyo Divorce peper.

Otherwise, Mleta maada inabidia focus na mambo yake tu na kukumbuka watoto
Plan haikua primarily kufuata divorce paper . Plan main ilikua ni kuhamisha ofis toka Dar maana kwasasa nimeamua kuhamishia operations zangu mkoani. Hivyo nikatumia fursa hii kuunganisha na siku ambayo hukumu itakua tayar
 
Back
Top Bottom