Hivi Dodoma ndio hakuna maji namna hii?

Hivi Dodoma ndio hakuna maji namna hii?

Uwezo mkuu wao ni kula kula kula tu
Wale ila maendeleo mengii walete kwa walipa kodi
Inaumiza sana kila senti unayopata imelimwa kodi lkn bado tena ufike nyumban hakuna maji na bills zinalipwa kwa wakati
 
Huyu Waziri nilikua nampenda sana enzi zilee,,sasa enzi hz hakuna anachokifanya na hakunaa wa kumkemeaa

Kwangu nina familia kubwaa na matank ya maji lkn inafika kpnd ht maji kwa matank yaishaa inatulazimu kuanza kusaka maji

Aisee huyu waziri huyuuu ningekua na namna haki ya Mungu sijui sijui
Pole dada akee
 
upo dodoma au wapi, dodoma hakuna maji wiki sasa. hadi natamani nirudi home.
Dodoma kuna tatizo la maji toka 2020 mwezi wa nane hadi leo hii tunakushangaa wakazi unaongea ongea tu.

Kuna maeneo yanapata maji kila siku kuna maeneo yanapata kila baada siku tatu, visima vya maji viko mayamaya na kuna mradi mkubwa wa maji ulianza kutekelezwa siku nyingi tu

Na katika hayo maeneo yanayopata maji kila baada ya siku tatu kuna laini zinatoa kila siku
 
Kichekesho hayo maji yenyewe yakitoka baada ya hiyo wiki moja, bado unakuta ni maji chumvi!!

Aisee huo mji unahitaji uwekezaji wa kutosha sana mpaka kuwa na hadhi ya kuitwa Jiji!
Kama kitu gani kwa mfano?
 
Nimekaa hapa wiki moja nzima, mabomba hayatoi maji.

Nadhani serikali imeharakisha kuhamishia makao makuu hapa Dodoma kabla suala la maji halijatengemaa.

Awesu ndo yupo Italy anakula bata tu.
Mdau pole kwa changamoto hiyo

Mimi ni Mkurugenzi wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira hapa DUWASA.
Kwanza ningependa kufahamu eneo uliloishi kwa muda huo wote ukakosa maji, pili nielewe kwa kifupi kuhusu hali ya maji jijini Dodoma.

Pamoja na kuhudumia Dodoma Mjini, DUWASA pia inahudumia miji ya Chamwino, Kongwa, Bahi na hivi karibuni tumeongezewa kibaigwa.

Ukiongelea Dodoma mjini, utakumbuka kuwa kati ya mwaka 2017/18 yalifanyika mabadiliko ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo immediately kama taasisi tulitarajia ongezeko kubwa la mahitaji ya maji. Wakati huo tulikuwa tumekamilisha mradi wa maji hapa mjini ambao uliongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji maji kutoka lita 30 milioni hadi kufikia lita 61.5 milioni kwa siku. Mradi huu ulikamilika 2015, na miradi ya maji husanifiwa kwa kipindi cha kati ya miaka 20 mpaka 30.

Kutokana na hali hii ya ongezeko la mahitaji ukilinganisha na uwezo uliopo, hatua kadhaa zimechukuliwa na zinatekelezwa na DUWASA chini ya Wizara ya maji kutatua changamoto hii.

Mahitaji kwa sasa ni lita 133 milioni kwa siku wakati uwezo ni wastani wa lita 68 milioni kwa siku. Hii inatulazimu kutoa maji kwa mgao. Ndiyo maana nimeuliza eneo uliopo ili kujua nini kilitokea.

Tunaendelea na utatuzi wa changamoto hii katika hatua za Muda Mfupi (uchimbaji wa visima pembezoni Mfano Nzuguni), Muda wa kati (Ujenzi wa bwawa pa Farkwa), Muda Mrefu ( Kutoa maji ziwa Victoria)na Mpango wa Dharula (kutoa maji bwawa la mtera)

Yote hii ni kuhakikisha Dodoma inakuwa na huduma toshelevu ya majisafi.
 
Binafsi ningetamani kufahamu huo mradi wa muda mrefu wa kuyatoa maji Ziwa Victoria kuja Dodoma, umefikia wapi! Maana kuna kipindi fulani nilisikia kule Bungeni, huo mradi ungekamilika mwaka 2025.
Na kwangu mimi naona ndiyo mradi wa uhakika ukilinganisha na hiyo miradi ya kuchimba visima.

Mwisho kabisa nakupongeza ndugu Mkurugenzi kwa kutolea ufafanuzi jambo hili. Na pia kwa kukubali maji yenu ya Duwasa mnayatoa kwa mgao kutokana na kuelemewa na idadi ya wateja. Na kweli maeneo mengi ya pembezoni mwa mji, na yenye idadi kubwa ya watu; hali siyo nzuri kivile.

Natamani kuona Wakurugenzi wa taasisi nyingine pia wakijitokeza humu jukwaani kutolea ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
 
Msalato ilikua Haina shida ya Maji Huku mwisho imeanza juzi nimechukiaaaaa....yaani yanatoka Kwa timing na hayana nguvu.
Sehemu isiyo na shida ya Maji ni pale mjini center eneo la makole na bungeni,kutokea bible mpk idara ya Maji Huku hakuna shida ya Maji Kwa kua pale Kuna Bomba kubwaa ,Kisasa SIKU hizi Kuna shida ya Maji kwenye nyumba 300 balaaa...panakera afu vyoo vya kukaa,ukienda nkuhungu Sasa Maji yanatoka Kwa wiki mara mbili (Huku ndo nilikaaa kabisaa mbona nilihama)

Dodoma Kuna shida ya Maji kama Kuna maeneo zaidi ya hayo niliyotaja yanatoka Kila SIKU maji hongera zao..ila panaboa Sanaa ,SIKU za mvua Sasa ndo maji yanatoka almost every day km wachawi vile[emoji57][emoji57][emoji2955][emoji2955][emoji2955]
 
Binafsi ningetamani kufahamu huo mradi wa muda mrefu wa kuyatoa maji Ziwa Victoria kuja Dodoma, umefikia wapi! Maana kuna kipindi fulani nilisikia kule Bungeni, huo mradi ungekamilika mwaka 2025.
Na kwangu mimi naona ndiyo mradi wa uhakika ukilinganisha na hiyo miradi ya kuchimba visima.

Mwisho kabisa nakupongeza ndugu Mkurugenzi kwa kutolea ufafanuzi jambo hili. Na pia kwa kukubali maji yenu ya Duwasa mnayatoa kwa mgao kutokana na kuelemewa na idadi ya wateja. Na kweli maeneo mengi ya pembezoni mwa mji, na yenye idadi kubwa ya watu; hali siyo nzuri kivile.

Natamani kuona Wakurugenzi wa taasisi nyingine pia wakijitokeza humu jukwaani kutolea ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Mwanza tu watu wanalalamika maji ya mgao mkali..ni kivipi tuyapeleke kwanza Dodoma kabla ya kucover kanda ya ziwa yote??

Hivi tumelogwa??
 
Bahati mbaya mtoa mada anaongelea tatizo la maji Dodoma! Na siyo Mwanza. Na mimi nimeongelea Dodoma kwa sababu nimeshuhudia.
 
Makao makuu yanajengwa tangu 1973, lakini suala la maji halikupewa kipaumbele. Ikulu inazinduliwa, lakini tatizo la maji halijatatuliwa. Hii ndio Tanzania ya minazi mirefu.
 
Nimekaa hapa wiki moja nzima, mabomba hayatoi maji.

Nadhani serikali imeharakisha kuhamishia makao makuu hapa Dodoma kabla suala la maji halijatengemaa.

Awesu ndo yupo Italy anakula bata tu.

====

UFAFANUZI KUTOKA DUWASA

====
Kwa kifupi huu ni mji wa ngamia
 
Mdau pole kwa changamoto hiyo

Mimi ni Mkurugenzi wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira hapa DUWASA.
Kwanza ningependa kufahamu eneo uliloishi kwa muda huo wote ukakosa maji, pili nielewe kwa kifupi kuhusu hali ya maji jijini Dodoma.

Pamoja na kuhudumia Dodoma Mjini, DUWASA pia inahudumia miji ya Chamwino, Kongwa, Bahi na hivi karibuni tumeongezewa kibaigwa.

Ukiongelea Dodoma mjini, utakumbuka kuwa kati ya mwaka 2017/18 yalifanyika mabadiliko ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo immediately kama taasisi tulitarajia ongezeko kubwa la mahitaji ya maji. Wakati huo tulikuwa tumekamilisha mradi wa maji hapa mjini ambao uliongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji maji kutoka lita 30 milioni hadi kufikia lita 61.5 milioni kwa siku. Mradi huu ulikamilika 2015, na miradi ya maji husanifiwa kwa kipindi cha kati ya miaka 20 mpaka 30.

Kutokana na hali hii ya ongezeko la mahitaji ukilinganisha na uwezo uliopo, hatua kadhaa zimechukuliwa na zinatekelezwa na DUWASA chini ya Wizara ya maji kutatua changamoto hii.

Mahitaji kwa sasa ni lita 133 milioni kwa siku wakati uwezo ni wastani wa lita 68 milioni kwa siku. Hii inatulazimu kutoa maji kwa mgao. Ndiyo maana nimeuliza eneo uliopo ili kujua nini kilitokea.

Tunaendelea na utatuzi wa changamoto hii katika hatua za Muda Mfupi (uchimbaji wa visima pembezoni Mfano Nzuguni), Muda wa kati (Ujenzi wa bwawa pa Farkwa), Muda Mrefu ( Kutoa maji ziwa Victoria)na Mpango wa Dharula (kutoa maji bwawa la mtera)

Yote hii ni kuhakikisha Dodoma inakuwa na huduma toshelevu ya majisafi.
Hongera mkuu
Ni wafanyakazi wachache sana wa Umma wanaweza kutoka live hapa jf na kujibu kama wewe
 
Shukrani kwa clarifications Mr. Emmanuel,

Me naomba tu kufahamu maeneo ya Ilazo huku mnaturudishia maji lini, Nina miezi sasa at least tulikuwa tunapata maji vyema tu, hata yakikata ilikuwa ni siku chache zinazovumilika..!!

Lakini haikuwahi kuwa mbaya hivi kama ya hii week yaani hamna kitu, tupo kama tunaishi jangwani..!!
 
Bahati mbaya mtoa mada anaongelea tatizo la maji Dodoma! Na siyo Mwanza. Na mimi nimeongelea Dodoma kwa sababu nimeshuhudia.
Kuna mdau wa duwasa hapo juu kasema moja ya suluhisho la maji ni mradi wa maji kutoka victoria , ndo maana mdau kaja na hoja itawezekana vipi maji ya victoria yasaidie dodoma ilhali hapo mwanza kwenyewe tu kuna mgao wa maji!
 
Nimekaa hapa wiki moja nzima, mabomba hayatoi maji.

Nadhani serikali imeharakisha kuhamishia makao makuu hapa Dodoma kabla suala la maji halijatengemaa.

Awesu ndo yupo Italy anakula bata tu.

====

UFAFANUZI KUTOKA DUWASA

====
Bil.47 zinaenda kwenye posho.
 
Back
Top Bottom