Hivi hamsomi mazingira? No way tutamuona akiwa live tena!

Probably you forgot to take your medication today.
Kupiga au kupigiwa ain’t shit in TZ, votes za kwenye ballot boxes si kitu kinachmuweka mtu au kumtoa mtu madarakani.
 
unavyosema mtaani unamaanisha nini kwani watu wanaishi kwenye mitandao
Leo nilibahatika kupita mtaa wa Msimbazi kuanzia Fire pale mpaka kutokea Kamata kule, yale makelele ya spika za wamachinga ni majanga sijui watu wanawezaje kuishi ule mtaa...
Baadae nikasema nikale mihogo pale Coco beach maana napenda kwenda pale siku za katikati ya wiki kunakuwa kimya sana, nikala mihogo na Pepsi ya baridiii, halafu nikaenda kumsalimia Mama yangu Magomeni Mikumi....
Baadae nikarudi zangu nyumbani Kisota.....
Kote huko nimepita sijasikia stori za maandamano wala polepole wala lissu....
Sasa sijui hizi pilika za humu mitandaoni ziko kwenye dunia yao tofauti ya kwetu.....
 
Kaka yake amesema bado yuko hai. Jamaa ana chip haishi kiboya. Na amewaambia wakimuua atajua cha kuwafanya
 
watanzania ni watu wa kufuata mkumbo wanasubiri wakulianzisha
 
Pia ukienda ofisini utakuta shughuli zinaendelea, makaburini watu wanazikana kama siku zote...lakini hakika nakwambia kote huko ukikaa ukatulia LAZIMA katika maongozi yao watapitisha na haya yanayoendelea.
 
dos.2020
Achana na huyu britanicca, mm nazungumzia wananchi wanaotaka kuandamana wanaotaka revolution. Huhu hawezi kuwakilisha kundi kubwa la watu hadi tuseme kuwa watu wanataka raisi afe/auwawe

nguvu ya uma barabarani ndio njia pekee ya kutukomboa, Ila kwa kweli bado sioni dalili.
 
Unaongea sana kwa kuwa unalala kwa dadako ,achana na nyuzi za kichochezi sisi tunapenda amani sana wewe hamia Congo

USSR
Sasa mkuu amani yenyewe unayo? Unajua anaefatia kutekwa na kupotezwa ni Nan? VP kama ukiwa ni ww? Mm napenda amani ndomana nataka serikali ichukue hatua kukomesha utekaji na mauaji holela
 
Baada ya Murilo kusema wanafuatilia taarifa za mwamba kutekwa tayari wameasharuka kimanga hawapo nae . Hapa ni kupaza tu sauti na kuomba itokee miujiza kama ilivyotekea alivyotekwa Mo
Ukiangalia ni kama raia tumemsahau ,sioni nguvu kubwa kupiga kelele dhidi yake. Hata Lisu akifanikiwa kutoka getezani afanye asepe tu watanzania sisi hatutamsaidia ni mdomo tu.
 
Umeandika Kwa hasira sana chief Tena sana!!

Lakini ni kusema intelligence ya kizalendo imezidiwa Kwa mbali na intelligence ya wahuni!!?

Pole pole alikua kiimani zaidi kuliko kiuhalisia na niseme TU wahuni walimstahi sana kwa siku kadhaa alizoishi mafichoni hapa nchini!!Tena sana!

Kumbe kwenye hili taifa hakuna tena Kuta za Siri zinazoongoza kizalendo zaidi ya wahuni na intelligence Yao iliyosheheni kimedani!!?

Unajua mi nilijua Kuna deep state halisi Sasa nashangaa juzi inaonekana na hiyo futungo state ilishatekwa na wahuni kitambo na haipo!!?nilihamaki nikakata Tamaa me nilijua deep state halisi IPO na inapambana na wahuni kumbe deep state nalo ni genge la wahuni kama HP alivyosema!!?

NB
Ulichokiandika mwishoni mwa paragraph sidhani kama kinaweza tokea tz coz watz wazalendo mmewaacha solemba Kwa mida mreefu sana wakaumizwa na kufa na Sasa moyo was kiwa wazalendo wamepoteza na sidhani kama maandamano yanaweza zuia uchaguzi labda jwtz wavae kiraia wawe waandamanaji na sio raia!!

Imani imekufa ,hasta baada ya intelligence kushindwa kumlinda HP Tena akiwa balozi mwenye title ya "Head of mission until 2027" kama mtu muhimu kama huyu mmeshindwa kumlinda mtalindaje raia wanaotafuta ugali wa Kila siku barabarani na hawana uhakika wa kuupata!!?

KAZI na utu tunasonga mbele!!!labda kupotea Kwa watu ndio utu wenyewe unasemwa na Chaka changu!!
 
Mkuu vipi yule alichana picha tu, ndio adhabu yake kufa? Adhabu ya mtu kuchana picha ni kufa ipo kwenye sheria ipi ya nchi?

Acha huyo Polepole ametukana wapi? Acha huyo Heche kwenda msibani ni haramu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…