Hivi hawa watu wanalipwa na hizi redio?

Filbert Kyenshambi kutoka Nshamba Muleba Kagera
 
Ujue madalali wanakaa vituoni tu ila maisha yanaenda
Km yule Ali mrangi gigiri si asubuhi si jioni yupo kwenye daladala anaenda mabibo na txt yake haibadilikagi
 
Miaka ya sitini alikuwepo Zakaria Ndemfoo wa Machame Kisiki, enzi hizo redio RSA(Afrika Kusini), DW(Ujerumani), redio India, VOA(Amerika), China na Urusi hizi zote zilikuwa na matangazo ya kiswahili huyu na wenzake walikuwa hawakosi kila siku wamo ukiacha za hapa TBC na VOK(Kenya). Wakati huo ni lazima ununue Post Card na Stempu ndiyo utume salamu, fikiria alituma ngapi na alinunua stempu na kadi ngapi. Hawa wa sasa shs 200 unapata sms 200 au shs 1000/= sms 10,000, ni sawa na bure.
 
Zakaria ndemfoo alifariki alikuwa mmachame
 
Dalisudi fanicha[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
kuna kipindi huwa nasikiliza JPili EFM
dakika 2 za mwisho wa kipindi kuna kupokea simu

mpaka nashangaa huyu jamaa ni kwamba simu yake special au vipi
maana kila siku ni yeye, hadi kero

zamani nilikua naamini hao jamaa wanatumia simu special, kama BlackBerry(kipindi hii simu inavuma)
mkipiga hata 100 kwa pamoja, yeye yake lazima iingie mwanzo
 
Du sijashuhudia hata kimoja hapo kweli ww muhenga
 
Au anapogaga kwa mtangazaji private😊😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…