Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Sawa 🙏
Aya chukua sharubati glass mbili ntakuja kulipia 🙂
 
Computer keyboard- kicharazio
Memory card- kadi sakima
Toothpick- kichokonoo
Covid 19- uviko- 19( kumi na Tisa)
Spy- shushushu

Mie Ni mkenya wakuu,je mwalimu wangu wa kiswahili alipatia ama alichemka?
 
Nini tasfiri ya neno" serious" kwa kiswahili? Watz naomba mnijuze tafadhali
 
Watakua ni wakenya maana wana kiswahili cha kipuuzi sana ukitaka kuamini angalia kiswahili cha kwenye sim
 
Nini tasfiri ya neno" serious" kwa kiswahili? Watz naomba mnijuze tafadhali
Hilo neno halina tafsiri moja, ila itategemea limetumikaje katika sentensi.
Maelezo:
1. Serious = Hasa/Haswa.
Mfano: Serious problem = Tatizo hasa.

2. Serious = Maanisha
Are you serious? = Je, unamaanisha?
 
Hilo neno halina tafsiri moja, ila itategemea limetumikaje katika sentensi.
Maelezo:
1. Serious = Hasa/Haswa.
Mfano: Serious problem = Tatizo hasa.

2. Serious = Maanisha
Are you serious? = Je, unamaanisha?
Nimekuelewa Sana mkuu
 
Uundaji wa maneno hukuza lugha na zipo njia 8 za uundaji wa maneno mampya ikiwe hii uliyoipendekeza ya kutohosha... ingawa ni njia dhahifu haizingatii mabadiliko ya isitalahi, pia hudumaza ubunifu wa uundaji wa misamiati mipya ...kama we muuandishi umedumaa na unaona usumbufu kuunda misamiati kwa njia ya unyumbuaji na fasiri ya maana na uunganishaji wa maneno....
Neno.. mfano wa maneno tuliyo tohoa... redio, data, programu, eroplaini, dukani, ikulu nk... ukitohoa kazi inakuwa ni kusanifisha muundo wa lugha kisha neno hutumika.
 
Kishkwambi neno limekaa, ki udaku ki kiherehere ki kimbele mbele.

Ni zuri kwa kwel limeendana na siye Watz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…