Lugha ina siri nyingi, ni Tanzania tu ambapo magazeti hayatumii KiSwahili sanifu.
Gazeti la Taifa Leo la Kenya linaweza kutumiwa na mgeni anayejifunza lugha ya kiSwahili lakini magazeti pendwa ya Tanzania kiswahili chake ni cha "mtaa fulani mdogo'.
Lugha ya Kiarabu sanifu classical Arabic hufundishwa mashuleni na kutumiwa katika magazeti makubwa, riwaya na pia ndicho kinachotumiwa ktk kufundishia ktk madrasa.
Tatizo sisi waTanzania hatuheshimu lugha ya kiSwahili, huwezi kutofautisha nani ni mwanzuoni yaani msomi wakati watanzania wakioongea.
Lakini watu wa jamii nyingine wanaotumia lugha kama za Kiarabu au Kingereza ukisikia mtu anaongea unaweza kwa haraka kutambua kuwa mtu huyu ni msomi au kakulia katika mazingira ambayo watu wanauelewa mpana wa lugha ya Kiarabu classical au Kiingereza classical.
Media za Tanzania zinatakiwa kuwa mbele kwa kuchapisha magazeti kwa lugha sanifu haijalishi ukubwa au udogo wa gazeti, kituo cha radio au kituo cha televisheni.
Ndiyo maana hapa jamiiforums tunaona tunasahihisha kuhusu matumizi ya herufi mfano H katika maneno kama atakuja au hatakuja maneno haya mawili ya kiSwahili yana maana tofauti, lakini media zetu utakuta watangazaji au waandishi wa katika media kubwa hata kutamka au kuandika kwa usahihi tunashindwa.