Hivi inakuwaje mzazi anakua tegemezi Kwa mtoto ambaye amejitafuta Kwa jasho lake bila kumrithisha hata mbuzi mmoja

Mleta mada pitia hili somo labda utajifunza chochote kuhusu kuwatunza wazazi👇👇​

Baadhi ya washiriki wa familia wa nyakati za Biblia waliwatunzaje wazazi wao?​

Walifanya hivyo kwa njia mbalimbali kwa kutegemea hali.
  • Yosefu aliishi mbali na baba yake Yakobo aliyekuwa amezeeka. Hali ziliporuhusu, Yosefu alifanya mipango ili baba yake awe karibu naye. Kisha Yosefu akampatia baba yake makao, chakula, na ulinzi.—Mwanzo 45:9-11; 47:11, 12.
  • Ruthu alihamia nchi ya mama mkwe wake na kufanya kazi kwa bidii ili amtunze.—Ruthu 1:16; 2:2, 17, 18, 23.
  • Yesu, muda mfupi kabla ya kifo chake, alichagua mtu ambaye angemtunza mama yake, Maria, ambaye alikuwa mjane.—Yohana 19:26, 27.
  • Biblia inatoa ushauri gani unaoweza kuwasaidia wale wanaotunza wazazi waliozeeka?​

    Biblia ina kanuni ambazo zinaweza kuwasaidia wale wanaotunza wazazi waliozeeka kukabiliana na changamoto ambazo wakati mwingine huchosha kimwili na kihisia.
    • Waheshimu wazazi wako.
      Biblia inasema nini: “Mheshimu baba yako na mama yako.”—Kutoka 20:12.
      Kanuni hii inaweza kutumikaje? Onyesha kwamba unawaheshimu wazazi wako kwa kuwapa uhuru kadiri hali zao zinavyoruhusu. Pia, kwa kadiri inavyowezekana waruhusu wafanye uamuzi kuhusu utunzaji wanaohitaji. Wakati huo huo waonyeshe kwamba unawaheshimu kwa kufanya kwa kiasi unachoweza ili kuwasaidia.
    • Elewa hali zao na uwe mwenye kusamehe.
      Biblia inasema nini: “Ufahamu wa mtu hakika hutuliza hasira yake, na ni fahari kwake kuachilia kosa.”—Methali 19:11
      Kanuni hii inaweza kutumikaje? Ikiwa mzazi aliyezeeka atasema jambo lisilo la fadhili au kuonyesha kwamba hathamini utunzaji wako, jiulize, ‘Ningehisije ikiwa hali zangu zingenifanya nishindwe kutimiza mambo fulani au kuniletea mikazo? Unapojaribu kuelewa hali zake na kuwa mwenye kusamehe unaweza kuepuka kufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi. C&P
 
Amekulea inatosha kushukuru hapo
 
Kuja kulalamika humu kuhusu wazazi wenu kuna tatizo sehemu. Kama mnalofanya ni jema msingetapatapa kuandika mabango marefu humu. Ajabu mitoto ya kiume ndio inaongoza kwa kulalamika kuhusu baba zao ni nadra kukuta kwa watoto wa kike.
 
Nilikuwa na akili mbovu sana kama za mtoa mada ila nilikuja kuzifuta siku niliyopata mtoto wangu wa kwanza maxmillian wangu.. Nilijisemea kimoyomoyo na mimi nilikunga hivi kweli..?. Mtoto ukimkuza tu nao ni utajiri tosha
 
Hata leo nimemtumia kiroho safi kabisa ila sijawahi kuelewa why mama awe na wivu au chuki kwa mtoto aliyemzaa mwenyewe tena kwenye ndoa stable kabisa.
Kuna siri nyingi sana kwenye mahusiano ya hao wazazi wawili ukizijua itakuumiza. Na ukitambua tafuta namna ya kuwasaidia.

Wapo wamama wengi wanazuia misaada kwenda kwa watoto wao. Wapo wamama wanasaidiwa ila hawawaambii watoto kuwa kuna mkono wa baba katika maisha yao. Zaidi wanawalisha sumu watoto.

Wapo wanawake enzi za ubinti wakiwa visu waliwavuruga wanaume kiasi kwamba haikueleweka baba halisi ni yupi. Kwenye senario kama hii huwezi kurupuka tu kulea mtoto wakati unajua baba mko nane
 
Hata leo nimemtumia kiroho safi kabisa ila sijawahi kuelewa why mama awe na wivu au chuki kwa mtoto aliyemzaa mwenyewe tena kwenye ndoa stable kabisa.
Mimi roho kama yako sina kabisa mkuu Zitto. Mimi mama yangu alinifanyia dhuluma kubwa sana ya pesa nyingi na uwezo wa kunilipa alikuwa nao kwa maana alikuja kupata 70 millions baada ya kuuza nyumba yake moja.

Mpaka sasa sijawasiliana naye miezi 18 (mwaka mmoja na miezi 6)
 
Bora asingenizaa kwa maana sikumuomba. Bora nimsaidie mtu Baki au rafiki aliyenisaidia kuliko mzazi aliyenitelekeza..
Alafu humu ndani watu wanasema "bila baba au umama usingekuwepo duniani". Kwani kuna mtu yoyote aliwalazimisha wanilete duniani au bila hao wazazi nisingezaliwa kwenye familia tofauti?

Au utasikia alikubeba miezi 9 as if kuna mtoto aliwahi kubebwa mwezi mmoja tu.
 
Kweli inàbidi uwalaumu sana wazazi wako maana bila wao ungezàliwa familia tofauti. Labda saa hii ungekuwa mtoto wa Dangote unaogelea mahela tuu. Ona sasa unahangaika JF kukashfu màma yako eti kwàni kuna mimba iliwahi kubebwa mwezi mmoja.!
Una akili nyingi sàna wewe.
 
This is purely ironic and sarcastic, umemng'ong'a kijanja, but the guy is right..
 
Maumivu ni makali lakini mwisho wa siku anabaki kuwa mama. Thamani ya pesa ambayo hajakulipa haifikii thamani ya muda aliotumia kubeba mimba yako miezi tisa. Haifikii thamani ya muda aliokuwa chumba cha kujifungua akiwa nusu hai nusu mfu. Haifikii thamani ya kukulea na kukunyonyesha mpaka ukakua angeweza kukutupa chooni. Mama hata awe kichaa ni mama yako huwezi mfananisha na mama mwingine.

Tafuta namna ya kumsaidia lakini asikuingize hasara. Kupigwa mizinga na wakina mama ni kawaida sana.
 
Kama wazazi wenu hawana umuhimu hakuna haja ya kuja kupunguzia stress humu. Piga kimya hukohuko acha kumhudumia hakuna haja ya sisi kujua. Ukilileta humu utaambiwa tu unapoenda tofauti.
 
Wewe ni laana na janga kwa Taifa hili. Asie thamini wazee wake wa nyama na damu basi hatakua na heri kwa yeyote au nchi yake.
Omba radhi za wazee wako haraka sana hata kama wameisha tangulia mbele ya haki. Maneno uliotoa ni laana
 
We ushawahi kubeba mimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…