BlueIvy
JF-Expert Member
- Jan 5, 2022
- 1,034
- 2,882
"Hivi INAKUAJE mzazi anakua tegemezi Kwa mtoto ambaye amejitafuta Kwa jasho lake bila kumrithisha hata mbuzi mmoja"
Nadhani hapa ungeweka sawa kichwa cha habari, "inawezekanaje mzazi uliyetelekeza familia ukataka msaada kutoka kwa hao uliyowatelekeza baada ya kukua na yy kuzeeka".Mzazi ni Mungu wa pili katika hii dunia hata ile kukuleta tu duniani yafaa umshukuru, na kushukuru ni pamoja na kumtunza wakati wa yy hana nguvu tena za kufanya hivyo. Usilipe ubaya kwa ubaya, kila jambo hutokea kwa sababu hata ww kutelekezwa kulikuwa na sababu nyuma ya pazia ambayo hukuwekwa bayana.
Nadhani kila mtu na afanye kwa sehemu yake bila kushurutshwa na mtu, si lazma ufanye kwa ukubwa hata kwa kidogo utapata baraka. Na katika yote tambua soote huzeeka na mwisho tunahitaji msaada hata kama ww ni tajiri, kuna vitu pesa haiwezi fanya.