Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Ccm Ina wenyewe mkuu kama una bisha muulize @ lucas mwashambwa
 
Hapo kwenye kununua vitu vya jumla, kabla sijanunua naanzaje kujua mahesabu ntatumia maharage kg 7, mchele 20 n.k

Ukiachana na vyakula bajeti binafsi je? Usafiri, saloon, mavazi nk
Kama una familia kitu cha msingi ni vyakula kabla ya vyote. Utajua vipi angalia ukubwa wa familia yako, kama ni watu kuanzia 5 nunua mchele kilo 20, unga 20, maharage 10, mafuta lita 10 na mengineyo.

Ukishaweza kudhibiti hapo hayo mengine utaweza kuyamudu kiurahisi maana utaanza kuona chenji zinabaki.
 
Okay walau chakula inapangika....

Haya matumizi mengine, cosmetics nguo, saloon etc hii je? Unaipigiaje hesabu?
 
Hiyo 10% una invest au nayo inaishia viti virefu.
 
Budget inategemea na kipato chako.
Tenga Yale matumizi ya ulazima kwa mwezi..
Kisha akiba ya dharula..
Vitu kama mavazi, pochi, lipstick, nk hivii Tenga muda maalum Kila baada ya muda flan km miezi miwili au mitatu...
 

Bro hii ishu yako inaonekana serious sana manake kuna sehemu nilikuona unaomba hadi softcopy ya kitabu cha matumizi ya hela

Ukitaka kuishi within budget hatua ya mwanzo ambayo binafsi naona ni muhimu ni kutofautisha needs na wants
 
Okay walau chakula inapangika....

Haya matumizi mengine, cosmetics nguo, saloon etc hii je? Unaipigiaje hesabu?
Sasa saloon mwenyewe unajua hapo siwezi kukushauri maana sijui unapenda styles gani kama ni kusuka, lace wigs au unanyoa sijui!

Nguo unanunua kila mwezi Eve? Vipodozi ni rahisi ukinunua vyote kwa pamoja lazima utoboe mwezi.
 
Kila kitu kinawezekana ikiwa bajeti itapangwa na wewe mwenyewe na haitakiwi izidi kipato chako cha mwezi au muda wowote.
Msingi wa bajeti ni huu.

Sasa, ukimkuta ni wa kike halafu ni mtumishi wa serikali au zile NGOs na Taasisi za kumwaga mifwedha nje ya mshahara halisi, HAWAWEZI kamwe kuisho kwa bajeti.

Anaishi jinsi anavyopata...zile za bwerere toka kwenye ajira na zile zinazopatikana kwakuwa ni wa kike!

Wanaume, kama kuna asiyejua bajeti, basi ni Chawa, mwanasisiemu aliye kwenye mfumo, biashara zote haramu na utakatishaji wa kila aina.

Njaa na dhiki lazima ikufanye uijue bajeti na kuifuata, kinyume chake...UTU uko rehani.

Mtoa mada akisema hana zile pesa za buu baa...nitamfundisha kutengeneza na kufuata bajeti.
 
VP hutumii mafuta
 
Sasa bro lipstic ya nini tena?
JksπŸ˜‚
 
Kati ya watu wabovu kwa bajeti ni pamoja na mimi, siku nikianza kuishi ndani ya bajeti na utajiri utaanzia hapo...hapa ninahitaji shule ya ubahili.
 
Bro hii ishu yako inaonekana serious sana manake kuna sehemu nilikuona unaomba hadi softcopy ya kitabu cha matumizi ya hela

Ukitaka kuishi within budget hatua ya mwanzo ambayo binafsi naona ni muhimu ni kutofautisha needs na wants
Bro huko ulikoniona sio mimi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hebu anza kunitofautishia hapo
Ili nijue pa kuanzia
 
Pesa za buuu baaa ndo zipi nadhani sina, naombe unifundishe kutengeneza na kuifata bajeti nipo serious sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…