Hivi kuna uhusiano gani kati ya 'gari' na 'mtoto wa kike?'

Hivi kuna uhusiano gani kati ya 'gari' na 'mtoto wa kike?'

Halafu kuna matangazo mengi ya uzinduzi wa magari mapya yanaambatana na mademu wakali, maana yake ni nini?

Possibly wanamaanisha kwamba ukiwa na hilo gari saizi yake ni hao mademu. Wakati magari yanatengenezwa huwa labda wananuia hivyo.
 
Taratibu bibi weeh. Siku hizi ladies hatutumii simu. Tunatumia devices ama gadgets, simu wanatumia watoto wa shle hehehe. Mwaka huu mtajinyoosha wenyewe.
Haha haaa King'asti umenichekesha....ni sawa na mtu mwenye NOKIA ya tochi akasema ana simu.....kanaitwa mawasiliano na si simu
 
Mim nafikiri itategemea yuko kwny stage gan ya maisha ikiwa ndo kagraduate tu chuo n kapata kazi obviously n lazma avute mkoko hizo idea zako za kujenga nyumba ni za kuanzia 30 yrs na kuendeleaa huwez kua 23 eti uhangaikie mjengo, nkt ndinga n 10m or wht evr vuta ndinga nyumba baadae..bhana..plus nyumba huwezi temebea nayo mgongoni..!!
Nyumba yangu ya kwanza niliijenga nikiwa na 25yrs na sikuwa na gari na wala sikuwa nimeoa. Marafiki zangu walionunua magari kipindi hicho wengi walishaaga dunia kwa kesi gonjwa. Gari + Tamaa ya madem = danger.
 
Kati ya gari na nyumba kipi kinafanya ndoa kuwa imara zaidi?

Wenyewe wana kauli yao kuwa NYUMBA UTAPANGA HATA MASAKI lkn eti huwezi kodisha gari kila siku:wanasisitiza UNUNUE LAKO maisha yasonge mbele ahahahaha!

Thx God siku hizi kuna hizi Noah na vitara hata za milion 2 ahahahahahahahaah!Unaenda Chang'ombe wanalipaka rangi saafi na wanaondoa milleage wanaweka ndogo unamdanganya kuwa ni toleo la mwaka jana maisha yanaendelea ahahahaha

Bila ujanja mjini hapa ndoa itakushinda kaka!
 
Hii inawezekana hana mtu akiwa anavuta sigara huku akitembea mwanamkea anaweza kushoboka....

ndo maana vijana wengi wanajifanya kuvuta sigara ili washobokewe na mademu. hadi mademu wanawaiga kuonesha wanashobokea moshi. mia
 
Wanawake kiasili wanavutiwa na watu wenye hadhi ya aina flani mbele ya jamii. Kitu gani kinapima hadhi ya mtu inategemea na wakati na mazingira. Zamani mtu mwenye mashamba mengi na chakula cha kutosha ndio ilikuwa kipimo cha hadhi ya mtu. Ukiwa huna hivi vitu utakosa au utapata wanawake wa ajabu ajabu wasiotakwa na wenye uwezo.

Na mazingira yana matter, kwa waliosoma shule mtakuwa mnakumbuka wanamichezo mahiri mashuleni walivyokuwa wanang'ang'aniwa na mabinti. Kwenye mazingira ya shule, ukiwa good on the field inakupa hadhi flani ambayo wengine hawana.

The same applies to modern life and cars. Kwa kiasi gari limekuwa kipimo cha hadhi ya mtu kwenye maisha yetu. Ukishakuwa na gari, jamii inakupandisha status yako, na wanawake wengi watakupenda tu.

Kwa wanaopenda STK, hao sijui huwa wanafikiria nini!?

Unaweza ukawa sahihi kiasi fulani tu,lakini wanawake ni wa ajabu sana,hata kama ni dereva wa serikali,atashobokewa kuliko hata bosi wake!Hiyo ni hirizi ya mjapani!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Taratibu bibi weeh. Siku hizi ladies hatutumii simu. Tunatumia devices ama gadgets, simu wanatumia watoto wa shle hehehe. Mwaka huu mtajinyoosha wenyewe.

Haaaaa..... King'asti eeee.....sikuwezi mamie

Uwe na Jumamosi tulivu.......
 
Last edited by a moderator:
Wenyewe wana kauli yao kuwa NYUMBA UTAPANGA HATA MASAKI lkn eti huwezi kodisha gari kila siku:wanasisitiza UNUNUE LAKO maisha yasonge mbele ahahahaha!

Thx God siku hizi kuna hizi Noah na vitara hata za milion 2 ahahahahahahahaah!Unaenda Chang'ombe wanalipaka rangi saafi na wanaondoa milleage wanaweka ndogo unamdanganya kuwa ni toleo la mwaka jana maisha yanaendelea ahahahaha

Bila ujanja mjini hapa ndoa itakushinda kaka!

Gari ni matumizi mabaya ya kipato kidogo tulichonacho watanzania tulio wengi. Kama m2 ana kipato kikubwa - hapo sawa ni bora achukue usafiri wakutembelea. Lakini katika uhalisia wa maisha ya wabongo walio wengi kumiliki gari wakati kipato ndo hicho cha kuangaikia sioni kama ni sahihi.

Kwenye red hapo; naomba nikujibu.
Naamka asubuhi, napanda daladala kwenda kazini (sijakodi)
Jioni napanda tena daladala kurudi nyumbani (sijakodi)
Nikifika mitaa ya stand naenda sehemu kupata moja baridi moja moto; usiku kwenye saa 2 nakodi tax inanipeleka nyumbani kwangu; hayo ndo maisha halisi ya kibongo na gharama ni ya kawaida.
 
Hahahahaaaa shostiii...ie nikionaga mwanaume anaendesha NAVARA nalowaga kabisaaa!!

NAVARA.jpg

You can drive too. Just try....
 
Unaweza ukawa sahihi kiasi fulani tu,lakini wanawake ni wa ajabu sana,hata kama ni dereva wa serikali,atashobokewa kuliko hata bosi wake!Hiyo ni hirizi ya mjapani!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Hata dreva wa gari la kubebea wagonjwa mahututi eti naye madem wanamshobokea? Jamani nyie madem mna matatizo gani.

Nitamjengea binti yangu tabia ya kuwachukia wenye kuendesha magari kwamba ni wauaji
 
Gari ni chombo kinachosaidia sana kwenye movement ya aina yeyote ile hakuna anaepinga hili, lakini ndo yamekua chachu ya migongano mingi kwenye suala zima la mapenzi, Kiukweli kumekua hakuna mapenzi ya dhati na hii ndio sababu kubwa unamwacha anaekupenda kwa dhati kufuata gari end of the day unatendwa unaanza safari za ulozi!kaza buti tafuta lako tuache ushamba that's all!
 
Kwani wewe ukiambiwa utembee umabli wa km 20 kwa mguu na kupanda gari utachagua nini..jamani usafiri unasaidia kwenye time management, au ulikuwa hujui kama wanawake wanajali muda..
 
Ax2+bx+c=0, X is also perpendicular to Y but inversily proportional to b, while b is a reciprocal of 1/x, Now find X utaelewa uhusiano wao.
kweli we kilaza...yaani mda wote huo unatafuta x huioni...!!!???:twitch::twitch:...eti wajameni...na nyie wengine x hamjaiona bado...!!??
 
Ngozi ya Dudu ndo ilitumika kwenye Tambiko la kijapan wakati wa Uzinduz, so kushoboka is inevitable, vitoto vya shule ni chips kuku eti wanasema za kununuliwa na mshkaj tam kuliko za Home! Asilimia 95% ya mimba za Udogon chanzo ni Chips Mayai, sio birian wala Pilau!
haya maneno ya mzeee wa benchi haya
 
Wanamme hawashobokei wanawake wanao-drive?
sio kweli, wanaume wanawaogopa wanawake wenye magari, tena kama hujaolewa ukanunua gari lako upo kwenye risk kubwa katika kupata mchumba, kuna jiran yangu hapo nje ni mhasibu kwenye kampuni moja ya simu, amenunua kari lake spacio, yuko desparate mpaka saiv hakuna anayemsemesha mtaani.. wanaume funguken, je unajisikiaje kuanza kupiga sound dem lenye gari wakati wew huna?
 
siku zote wanawake ndo wana control maisha wa wanaume, kwa wale tuliosoma boarding(boys tu) mtakubaliana na mim kwamba siku tukitembelewa na girls tutaziazima pasi hata kwa headmaster utajitosa kuomba pasi mpaka unyooshe upendeze siku hiyo.., full kuazimana unyunyu nk..nk.., the same hata kwenye maisha ya sasa, watu wananunua sana magari saiv coz ndo wanawake wanavotaka.., wengine wanasema ni ULIMBO WA MADEM, kama nyumba ndo ingekuwa ni priority yao, nadhan msongamano dar ungeshapungua na nyumba zingeshafika bagamoyo na mkuranga saiv, hata kibanda mtu angekomaa awe nacho tu kama tunavonunua starlet na vitz saiv.
 
Ax2+bx+c=0, X is also perpendicular to Y but inversily proportional to b, while b is a reciprocal of 1/x, Now find X utaelewa uhusiano wao.

Tized mwenzio nina mswaki wa namba kwa hiyo hapa kwenye mambo ya inverse nini sijui waniua and yet nahitaji kujua huo ufafanuzi wako. msaada pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz!!
 
Back
Top Bottom