Ila katika mambanga makali ya Marehemu, lile la Kagera lilikuwa kubwa sana. Alikosea mno na akavumiliwa, lakini alikuja kufanya mbanga jingine kubwa zaidi miezi michache kabla hajafariki, mbanga ambalo lilitikisa mno nchi hii hadi kufanya wenzake washindwe kumvumilia hadi wakavunja utamaduni uliokuwepo tangu nchi hii kupata uhuru...
Lakini pia, kusema marehemu alikuwa amejaa mabaya tu, nadhani ni kukosa uungwana. Kuna mazuri na makubwa aliifanyia Tanzania, japo kuna wengine bado hawataki kukubali. Nadhani muda ndiyo utasema kweli.
Yote tisa, tumefika hapa tulipo kwasababu kuna mahesabu mazito ambayo marehemu na mitume wake walikosea kuyahesabu vizuri. Walikata mti waliokuwa wameukalia. Namuombea sana Raisi Samia na yeye asiige kutaka kukata mti anaoukalia, hata kama anadhani unamkwamisha kwenye baadhi ya mipango yake ya baadaye...