Hivi kwanini Hayati Magufuli aliamua tu kuwa katili bila sababu zozote?

Sidhani kama mada umeielewa, soma bila kuwa na usukuma gang akilini ndiyo utaelewa mada.
 
Katili amejenga barabara za kutosha, kawajali wanyonge,kapambana kurudisha umeme kiwa stable,kaboresha afya, elimu na kukuza uchumi. Katili ni huyu anayetoza masikini tozo, analambisha watu asali,anaua wagonjwa kwa miundombinu mibovu,anatumia hovyo fedha za masikini kusafiri na walamba asali n.k huyu ni zaidi ya muuaji na katili, alipaswa kuwepo jela
 
Huo sio uelewa, nilitaka kushangaa kwamba watanzania hawa hawa wawe waelewa!!

Halafu la kumkosoa Nyerere nakumbuka Lissu alivyomkosoa Nyerere bungeni watu walimuona kamkosea heshima baba wa Taifa.
 
Wajane mkaungane na mama Janeth ili mfarijiane maana naona uchungu wa mimba zenu ni mkali. Marehemu hakuwaachia kitu poleni sana.
 
Onayosema ni kweli kabisa....

Ukitembelea kagera na vijiji vyake na pia ukatazama takwimu zinazosema kagera ndo maskini zaidi Tanzania utajiona mbuzi[emoji23]...

Maendeleo ya watu binafsi na mtu mmoja mmoja kagera yanazidi kupaaa...tazama nyumba zinazojengwa vijijini kwa kasi...
 
Hiyo miezi michache kabla ya kufa alifanya mbanga gani mkuu?
 
Samia mjanja
1. Samia alitafuta maridhiano ndani ya ccm kwanza ndio maana anaenda sambamba na ccm kwa ujumla wake kwenye mazungumzo na kila kitu

JK ALITAKA KATIBA MPYA BILA support ya Ccm ndio maana alikwama.
 
Namaanisha kuwa uvumilivu wa maovu ya Jiwe ungefika ukingoni haraka sana kuliko uvumilivu wa maovu ya ccm. Rais kuua raia wako unadhani Watanzania wamgevumilia mpaka lini?
Hakuna hicho kitu mkuu, kwanza hata hii ccm huko kuivumilia ni kwa sababu hakuna tunachoweza kufanya chochote kwa kifupi ccm wanatuweza iwe kwa kutumia nguvu au kucheza na ujinga wetu. Watanzania waliyojaa uwanjani huku wakilia kuaga mwili wa Magufuli hadi wakakanyaga na wengine kupoteza maisha ndio hao wangepoteza uvumilivu wa mauwaji ya Magufuli? Hakukuwa na dalili yeyote kuonyesha kuwa watu wanavumilia mauwaji ya Magufuli na uvumilivu huo unaelekea ukingoni.

Tusikuze mambo, hawa watu waliyokuwa wanatoka makwao na kujaa barabarani kuona mwili wa Magufuli ukipita, nadhani huo uvumilivu wao ulikuwa bado una miaka mingi sana mbeleni.
 
Huyo mwamba wako ni motoni tu, hakuna option nyingine. Bila Mungu kuingilia kati sijui nchi hii ingekuwa wapi

Sawa mungu, na wewe huko motoni unaingia lini🙄🙄🙄🙄
Mungu asingeingilia kati kukupa akili za mkopo unazotumia kumpangia Mungu sijui ungekua mtaa gani ukiokota okota kata
 
Samia mjanja
1. Samia alitafuta maridhiano ndani ya ccm kwanza ndio maana anaenda sambamba na ccm kwa ujumla wake kwenye mazungumzo na kila kitu

JK ALITAKA KATIBA MPYA BILA support ya Ccm ndio maana alikwama.
Kwani ccm tatizo lao ni katiba mpya tu au uwepo wa aina fulani ya vipengele kwenye hiyo katiba mpya?
 
Mm naomba nijue hiyo mbanga ya mwisho aliyofanya siku kadhaa kabla ya umauti wake!.
 
Bado mnapambana na maiti mna akili nyie?
 
Itakuwa kukataa kuwa Covid haipo na kukataa barakoa na chanjo
Wazee wakaona huyu kichaa atamaliza nchi nzima, wakakosa uvumilivu, the rest is history
Mmh itakua sio hii maana covid ilkua moto mwaka 2020 mwezi wa 3-6 ivi baada ya hapo hali ikawa shwari shughuli zikawa zinaendelea na ikawa kama hakuna covid. Nae kaondoka mwezi wa 3
 
Mmh itakua sio hii maana covid ilkua moto mwaka 2020 mwezi wa 3-6 ivi baada ya hapo hali ikawa shwari shughuli zikawa zinaendelea na ikawa kama hakuna covid. Nae kaondoka mwezi wa 3
Hilo lilikuwa wimbi la kwanza, wimbi la pili ndio lilikuwa balaa, likaondoka na gavaa Ndullu, Maalim Seif, Kijazi ndani ya mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…