Hivi kwanini uchawi hautumiki kwenye Uwanja wa Vita?

Hivi kwanini uchawi hautumiki kwenye Uwanja wa Vita?

Ndugu zangu mshawahi kujiuliza kwanini uchawi hautumiki kwenye uwanja wa medani (vitani), nadhani kuna vitu vingi tumeshuhudia vya kichawi ambavyo ki uhalisia au ki fikra za kawaida tu vinaweza kuwekwa kwenye vita na vikafanya kazi..

lakini cha ajabu Uchawi hautumiki kabisaaa ani tena nasikia uzunguni huko uchawi wao upo developed😀😀 sasa inashindikanaje wale wanajeshi wa upinzaniwakapigwa kimbora wakaumwa matumbo wiki nzima.

mi naona uchawi ni wa mchongo... kuna sababu nyingine?
Mbona unatumika Sana tu! Ulizia uambiwe!
 
Zamani nilikua siamini kabisa kama kweli uchawi upo, nilikuja kuamini hii mambo baada ya jamaa yangu kuumwa sana halafu kila tukimpeleka hospitali ugonjwa hauonekani, huyu jamaa alimdhulumu bibi flani pesa yake halafu mbaya akawa anamtolea maneno ya ufidhuli kila anapokuja kumdai.
Siku jamaa alipotapika fundo la nywele na hirizi ambayo ndani yake kuna vipande vipande vya viwembe ndio nikaanza kuamini kweli haya mambo yapo.
Ila pamoja na uwepo wake sio mambo ya kuyaendekeza endekeza, maana ukiyaendekeza ni rahisi kudumbukia kwenye ushirikina.
 
Naunga mkono hoja. Kuna mnaija mmoja nimefanya nae kazi kwa miaka kadhaa aesee piga ua hakupi wala hapokei hela mkononi, anakuwekea mezani na wewe unamwekea mezani. Mkikutana njiani anakupeleka popote mnakaa anakuwekea pesa yako kwenye kitu chochote unachukua
Hii hata wahindi ufanya
 
Ndugu zangu mshawahi kujiuliza kwanini uchawi hautumiki kwenye uwanja wa medani (vitani), nadhani kuna vitu vingi tumeshuhudia vya kichawi ambavyo ki uhalisia au ki fikra za kawaida tu vinaweza kuwekwa kwenye vita na vikafanya kazi..

lakini cha ajabu Uchawi hautumiki kabisaaa ani tena nasikia uzunguni huko uchawi wao upo developed😀😀 sasa inashindikanaje wale wanajeshi wa upinzaniwakapigwa kimbora wakaumwa matumbo wiki nzima.

mi naona uchawi ni wa mchongo... kuna sababu nyingine?
Ufikiri wako ni mdogo sana,hakuna kitu chenye thamani na nidhamu kama uchawi kwani unamipaka yake hasa dhidi ya wasio na hatia.

Hivyo basi hata wewe unaetaka kuutumia unatakiwa uutumie ukiwa na uhakika kwamba unayemfanyia ana makosa kweli sivyo madhara yatakurudia wewe!!

Katika uwanja wa vita mara nyingi pande zote mbili hufanya mambo yasiyo mazuri kama wizi,kubaka,n.k vitu ambavyo havitakiwi ktk uchawi.

Sasa hapo ndipo shida huja je masharti mtayaweza tena?
 
Inakuwaje mchawi anatumia Radi kumpiga mtu or mifugo Si watumie radi vitani pia
Wewe ndiye UNAAMINI mchawi ANAWEZA KUTUMIA RADI kumpiga mtu mwingine.

Lkn UHALISIA wa mambo ni HAKUNA MTU ANAWEZA KUMILIKI RADI!

Hata wewe unayeamini hizo STORI za radi hujawahi kushuhudia MTU YEYOTE anamiliki radi, zaidi unasikiasikia kwa watu ambao nao wamesikiasikia tu!
 
Uchawi haupo acha mawazo ya kijinga.

Ni watu wapumbavu tu wanaamini uchawi upo.

Uchawi, ulogi sijui ujinga gani vitu hivyo havipo.
 
Mbona unatumika Sana tu! Ulizia uambiwe!
Kama unajua unatumikaje TUAMBIE na sisi tujue!

Vinginevyo ni yaleyale tu ya RISASI KUGEUKA MAJI, kitu ambacho wala si uchawi bali MATUMIZI YA AKILI kujaza watu ujasiri na morali wa kupigana na ADUI MWENYE SILAHA KALI bila kuwa na hofu ya kudhurika!
 
uchawi ni technique ndogo sana..nasikia chuma ulete ili ifanye kazi ni lazima akupe hela mkono kwa mkono..leo hii ukienda benk kumpa hela Teller unampa mkononi au unaweka pale kwenye kidirisha then anachukua??..kuna mwanangu mmoja ni mtu wa Finance aliniapanga hii ishu
Hakuna kitu kama hicho tusidanganyane kirahisi hivyo

Ingekuwa mambo yako hivyo basi huku mitaani wanaodaiwa kuwa ni wachawi tungeuona huo utajiri wao

Hii kitu ni fix sana na pale inapokuwa ngumu kuonesha uhalisia utawaskia "mchawi ana utajiri mkubwa kwenye mambo ya kiroho kuliko pesa"
 
Risasi sekunde ishakutoa roho, uchawi mpaka wiki au miezi, slow process..
 
Mwamba Uchawi unatumika sana vitani, tatizo kizazi chetu hakijawahi kushuhudia vita ndio maana unapata ujasiri wa kusema hili, vita inapiganwa mpaka na viumbe ambavyo kwa macho laini uwezi kuviona, rejea vita ya Sodoma na Gomola ( ile haikuwa gharika ni vita mzee, tena ilivyo advance ) nenda kachimbue World War II huko mjerumani alikuwa akitumia vyote, uchawi na [emoji89]..uchawi unatumika vitani, hata hapo kagera tu kuna wazee walikuwa wakifanya yao, na wapo mpaka sasa...
 
Mimi nadhani ni vigumu sana uchawi kudhuru mtu ambaye hauna details zake.

Wachawi utakuta wanakuagiza kitu fulani kwa mtu ambaye unataka adhurike,utaskia lete nywele yake au lete nguo n.k

Kisha wanatumia hiko kitu kumdhuru mtu,mimi nadhani bila kuwa na kitu fulani cha mtu huyo inaweza kuwa ngumu.

Sasa vitani mfano vita ya urusi na ukraine,mchawi atapata wapi vitu vya adui ili amdhuru ?

Ndio maana inakuwa rahisi mtu kumroga mtu anayemjua kwa sababu akiambiwa alete kitu fulani kutoka kwa huyo mtu analeta.

Mnaobeza uchawi hamjakaa na watu wanaojua hayo mambo,uchawi upo.

Kuna mama alikaa miezi kadhaa hajazaa kwa sababu alifanyiwa ucahwi na mke mwenzake kwa mganga.

Mganga alimchukua mbuzi akafanya mambo yake kisha yule mbuzi akamfunga(akamshona)sehemu za siri kisha akamfukia mbuzi,yule mama alikaa na mimba zaidi ya mwaka.

Baadae tena ikatokea sontofahamu mganga na yule mama,mganga akaenda kumfukua mbuzi kisha akampasua sehemu za siri na yule mama kule akazaa mtoto akiwa amekomaa kabisa.

Sasa utaona hapo kwamba wanaofanyiana uchawi ni watu wanaofahamiana kwa sababu mtu unayemfahamu ukiambiwa kuleta nywele yake,au kipande cha nguo,au kiatu chake au kucha yake ni rahsi kuliko kuleta vitu hivi kwa mtu usiyemfahamu.

Uchawi upo na mimi nadhani hao wenye uchawi hawajataka kushughulisha akili yao kuvumbua vitu vya ziada ambavyo vitaondoa vikwazo ama mipaka katika uchawi waliourithi.

Kama ambavyo zamani kulikuwa na redio kisha watu hawakuishia hapo wakafikiria na kufanya tafiti wakagundua mpaka tv na simu za picha.

Basi na 2achawi 2a kishwahili nadhani wametosheka tu na uchawi waliorithi kutoka kwa wazee wao,ha2ataki kufanya tafiti na kuona namna gani uchawi unaweza kufanya mambo makub2a zaidi ya hapo.

Kuna miti ukichanganya na ukajipaka basi unaweza ukapita sehemu na mtu asikuone,unaweza kuona namna gani mtu akiamua kufanya tafiti zaidi juu ya hiyo miti inaweza kuleta manufaa katika mambo mengine ?

Pengine hiyo miti ikichanganywa ina particles ambazo macho yetu hayawezi kuona mchanganyiko huo ?

Ni mawazo yangu tu ila kidini uchawi haufai kwa sababu ya huu ujinga wa kuwadhuru watu wengine
 
Kama unajua unatumikaje TUAMBIE na sisi tujue!

Vinginevyo ni yaleyale tu ya RISASI KUGEUKA MAJI, kitu ambacho wala si uchawi bali MATUMIZI YA AKILI kujaza watu ujasiri na morali wa kupigana na ADUI MWENYE SILAHA KALI bila kuwa na hofu ya kudhurika!
Bahati mbaya mimi si mwanajeshi na sijawahi ingia uwanja wa mapambano hata hivyo nimewahi sikia story mbili tatu toka kwa wanajeshi walioshiriki vita mfano vita ya Tanzania na Uganda! Miongoni mwa ushirikina ni pamoja na matumizi ya madawa ya mtu kutoonekana na adui au risasi kutomdhuru endapo utapiga mwili wake na badala yake kudhurika kama utalenga na kupiga kivuli chake! Kwa kifupi ushirikana upo wa kiwango cha juu sana! Watafute wanajeshi watakusimulia! Hakuna mwanajeshi asiye mshirikina! Ni kama kwenye siasa! Ni labda asilimia moja siyo washirikina wengi ni washirikina na wachawi!
 
Hela HAZIWEZI KUPOTEA TU hivi hivi!

Hicho kitu hakipo!

1. Itakuwa HAUTUNZI VIZURI kumbukmbu au rekodi zako za kinachoingia na kutoka.

Waswahili wanasema MALI BILA DAFTARI HUPOTEA BILA HABARI!

2. Una MATUMIZI YA HOVYO na hauweki kumbukumbu za hayo matumizi

3. HAUKO MAKINI/ SI MTU MAKINI!

Siku hizi kuna matapeli/ utapei na wizi wa viwango vya lami kiasi kwamba kama wewe si mtu makini au tayari umejawa kichwani na imani zako za kichawi lazima utaamini chumaulete na utaanza kuchafua watu wasiokuwa na hatia!

Ukienda kwa mpiga ramli, UNAPIGWA TENA!
sidhani mkuu hii sio sababu..mimi nshawahi kufanya kazi na mama..kipindi hiko nipo yanky..kazi enyewe mama lishe..nilikuwa nikipeleka order sitoi mguu bila kupewa hela... na vile mama yangu alikuwa mzoefu kwenye hii biashara..ila kuna siku tunauza sanaaaa namimi naona kabisa tumeuza..tena mimi ndo nae pokea hela kwa wateja napeleka kwa mama...ila jioni mama akiwa anapiga hesabu hela imepukutika yoote hata ya msingi ...anaanza kukopa..mkuu hatakama ni utunzaji hafifu ndo tupoteze hela hadi msingi ufe kwa siku moja?
 
Back
Top Bottom