Hivi kwanini wanaume wana tabia hii?

Hivi kwanini wanaume wana tabia hii?

Ni rahisi sana urafiki kuwa mahusiano ila ni ngumu sana mahusiano kuwa urafiki, mkishaingia ndani ya mapenzi ikitokea mkaachana tayari kuna uadui.
Kabisa na ndio kitu sipend hasa ikiwa mtu nahis uwepo wake ni muhimu tukiwa marafiki tu bas tuishie hapo
Mapenz mwisho Huwa mbaya sana
 
Inategemea umejiwekaje kama umekaa kutongozwa tongozwa utatongozwa if your a woman with dignity hamna atakaye kukutongoza Zaid yakukuheshimu ,how you behave is how people gonna treats you so change your attitude
 
Katika maisha ya kawaida binadam kusaidiana ni kitu cha kawaida. Haijalishi unamfahamu au humfahamu kama mtu anahitaji msaada msaidie tena bila kutegemea kitu chochote in return.

Kuna hii tabia wanaume ukiwasaidia lazima baadae warudi wakutongoze. Sijui huwa wanawaza nini! Umesaidiwa toa shukrani zako kisha nenda haina haja ya kutaka kuleta mazoea mengine.

Nakutana na hili mara nyingi sana nashindwa kuelewa inaonekana msaada ni kitu cha ajabu sana kwa wanaume hawaamini kama mwanamke anaweza kutoa msaada bila kuhitaji chochote kutoka kwao. Maana wao wamezoea hawatoi msaada hasa kwa jinsia tofauti mpaka wahakikishe kuna kitu atapata kutoka kwa mtu anayemsaidia.

Ukisaidiwa shukuru kisha ondoka usitake kuleta mazoea, wengine hatupendi mazoea na shobo zisizokua na maana.
Namimi nisaidie, sitakutongoza.
 
Kabisa na ndio kitu sipend hasa ikiwa mtu nahis uwepo wake ni muhimu tukiwa marafiki tu bas tuishie hapo
Mapenz mwisho Huwa mbaya sana
Kwetu sisi ni ngumu sana kukubaliana na hilo kwa walio wengi.
 
Katika maisha ya kawaida binadam kusaidiana ni kitu cha kawaida. Haijalishi unamfahamu au humfahamu kama mtu anahitaji msaada msaidie tena bila kutegemea kitu chochote in return.

Kuna hii tabia wanaume ukiwasaidia lazima baadae warudi wakutongoze. Sijui huwa wanawaza nini! Umesaidiwa toa shukrani zako kisha nenda haina haja ya kutaka kuleta mazoea mengine.

Nakutana na hili mara nyingi sana nashindwa kuelewa inaonekana msaada ni kitu cha ajabu sana kwa wanaume hawaamini kama mwanamke anaweza kutoa msaada bila kuhitaji chochote kutoka kwao. Maana wao wamezoea hawatoi msaada hasa kwa jinsia tofauti mpaka wahakikishe kuna kitu atapata kutoka kwa mtu anayemsaidia.

Ukisaidiwa shukuru kisha ondoka usitake kuleta mazoea, wengine hatupendi mazoea na shobo zisizokua na maana.
Tatizo wanawake wa Sasa wapo kimalaya Malaya tu
 
Wewe mwanamke ni lazima utongozwe. Kukataa au kukubali ni juu yako.
 
Depresheni tena 😂
Mi kuna mdada nilimsaidia sikuzingatia namba nikaja kukutana nae kama mwezi baadae hivi akaniuliza mbona sikuchukua namba, chukua namba yangu au nipe yako, nikampa. Huwa hachoki kunijulia hali.
Ndio ubinadamu huo.
 
Dada, upo dunia gani unayoishi bila kujua maisha na tamaduni halisi ya jamii?

Nilitaka nikuanzie mbali sana kukuelewesha sababu ya kutongozwa kila unapotoa msaada kwa wanaume, lakini wacha nifupishe stori.

Katika jamii yetu, mwanamke ni mtu wa kupewa na si kutoa, ndivyo ilivyojengeka katika jamii pia hana kauli ama tuseme 'haki' ya kumtongoza mwanamme hata ikitokea kavutiwa naye.

Kwa hiyo wanawake huexpress desire zao za mapenzi kwa ishara.

Na ishara hizo ni pamoja na kujichekesha chekesha kwa kila neno litamkwalo na ampendaye, kujipitisha pitisha inaitwa kujilengesha kwa mwanaume husika, kutoa lasirimali zake kwa mtu ampendaye kama msaada nk nk, zipo ishara nyingi sana zitumikazo kumuatract mwanamme aingie kwene box.

Hata mimi ikitokea mwanamke akanipatia msaada nitaona kama ni extraordinary, lazima ningetoa mrejesho wa namna hiyo, yaani ningelimtongoza tu.

Wewe ni mwanamke unayeishi katika jamii yenye mfumo huo , kwanini ushangae kutongozwa kama njia ya shukrani kwa msaada wako?

Halafu kwanini ulaani kutongozwa badala ya kushukuru, maana yake umebeba sifa za mwanamke wa kiafrika zinazopendwa na wanaume.

Wenzako wengine wasipotongozwa, hujihisi wameibiwa nyota zao na kupelekea kwenda kwa waganga wa kienyeji kuogeshwa madawa ya kuondoa mikosi!
Sawasawa
 
Agenda za kikao chetu zinafanyiwa kazi vzr, mwanamke anaye jipitishapitisha, haachwi hivihivi!
 
Mwaka jana wakat nafuatilia suala langu kwenye taasisi flan pale morogoro, nilisumbuliwa sana, ilinichukua kama miez mitatu hiv had nikaishiwa pesa ya matumiz.

Sasa kuna sista mmoja anastationary huwanatoa sana kaz zangu kwake akaniuliza shida yangu nkamueleza, akanambia kama kuwa hiyo taasis ndo tabia yake kusumbua watu.

Basi yule sista akawa kila napoenda ofisin kwake ananipatia 50,000 ya matumiz. Ila siku moja wakat nimekaa ofisin kwake akasogea karibu yangu zern distance akanibusu kisha akaninong'oneza masikion akiniuliza "unataka sh ngap?" nilishindwa kumjibu coz nilijisikia aibu nikama nauza utu wangu, nikajikaza nikamwambia nipe 50,000 ileile. Alivonipatia hela nikasepa, nikapanda basi nkarud home mana nikaona ninakoelekea siko.
 
Shida ni nyie huwa hamsaidii.
Ingekua na ninyi ni watoa misaada wala hayo yasingekuwepo, ila ninyi mnataka kusaidiwa ila Me akiomba msaada kwenu mnamdharau, na wanawake wengi wana kauli zao kwamba "hawawezi kumpa hela mwanaume kwa namna yoyote"..
 
Back
Top Bottom