Dada, upo dunia gani unayoishi bila kujua maisha na tamaduni halisi ya jamii?
Nilitaka nikuanzie mbali sana kukuelewesha sababu ya kutongozwa kila unapotoa msaada kwa wanaume, lakini wacha nifupishe stori.
Katika jamii yetu, mwanamke ni mtu wa kupewa na si kutoa, ndivyo ilivyojengeka katika jamii pia hana kauli ama tuseme 'haki' ya kumtongoza mwanamme hata ikitokea kavutiwa naye.
Kwa hiyo wanawake huexpress desire zao za mapenzi kwa ishara.
Na ishara hizo ni pamoja na kujichekesha chekesha kwa kila neno litamkwalo na ampendaye, kujipitisha pitisha inaitwa kujilengesha kwa mwanaume husika, kutoa lasirimali zake kwa mtu ampendaye kama msaada nk nk, zipo ishara nyingi sana zitumikazo kumuatract mwanamme aingie kwene box.
Hata mimi ikitokea mwanamke akanipatia msaada nitaona kama ni extraordinary, lazima ningetoa mrejesho wa namna hiyo, yaani ningelimtongoza tu.
Wewe ni mwanamke unayeishi katika jamii yenye mfumo huo , kwanini ushangae kutongozwa kama njia ya shukrani kwa msaada wako?
Halafu kwanini ulaani kutongozwa badala ya kushukuru, maana yake umebeba sifa za mwanamke wa kiafrika zinazopendwa na wanaume.
Wenzako wengine wasipotongozwa, hujihisi wameibiwa nyota zao na kupelekea kwenda kwa waganga wa kienyeji kuogeshwa madawa ya kuondoa mikosi!