Hivi Lazaro aliyefufuliwa na Yesu, alitoa ushuhuda gani kuhusu kuzimu baada ya kufufuka?

Hivi Lazaro aliyefufuliwa na Yesu, alitoa ushuhuda gani kuhusu kuzimu baada ya kufufuka?

Huwezi kufafanuliwa, yani hivi vitabu mfano wake ni sawa na Nyerere mwaka 1960 anazungumzia jinsi alivyokufa na msiba wake mwaka 1999.

Ni ngumu sana kwa mtu anayetumia akili na logic kuviamini vitabu hivi, hasa kile cha Quran ndio magumashi matupu.
Sawa. Hivyo, sio sahihi kwamba waliokufa hawana kumbukumbu ya ya duniani! They have memories kama yule tajiri akiwa kwenye mateso makali kuzimu alivyokumbuka ndugu zake aliowaacha duniani na kumwomba Ibrahim amtume mtu kuwaonya!
 
Simulizi hii ya Yesu inaonyesha hili ni jambo kamili lilitokea haikuwa hadithi ya kutungwa kama ile hadithi ya Msamaria mwema
Kwanini unadhani habari za tajiri ni kisa cha kweli na simulizi la msamaria ni ya kutungwa?
 
Naye anatuchanganya, kwahiyo alikuwa anamsemea tajiri
... alikuwa anatupa picha ya maisha yajayo baada ya kuondoka katika dunia hii.

In fact hoja ya msingi kwenye huu uzi ni maisha baada ya kifo; Yesu alishaeleza kupitia mfano wa Ibrahim, Lazaro, na tajiri.
 
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.

Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?

Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?

Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?

Mwenye majibu tafadhali.
Hivi haijawahi kuandikwa injili ya Lazaro?
 
Mkuu usipende kuamini story za Biblia na Qur'an kwani zile ni hadithi tu za kuchanganya watu akili wa kuwatia hofu
Unaweza kutunga stori zako; ukaandika kitabu ukazisambaza watu wakaziamini kwa mamilioni Mkuu?
 
Nieleweshe hii
... Lazaro aliyefufuliwa na Yesu (by then Yesu akiwa duniani) na Lazaro aliyekuwa na Ibrahim mbinguni na tajiri akiwa kuzimu (by then Musa akiwa duniani). Hao ni Lazaro wawili.
 
... yule tajiri akiwa kule kuzimu akakumbuka ndugu zake aliowaacha duniani!
Akiwa kuzimu sio akiwa amerud dunian. Halafu ukiwa unataka kuijua Biblia usisome mstari mmoja mmoja soma kwa muktadha mzima utaielewa. Maana Yesu mwenyewe anasema cc au nyie mmepata kupewa kuzijua Siri za Mungu wengine watasikia au kusoma hawataelewa ndio maana Biblia imeandikwa kwa mafumbo. Wako wakuielewa na wako watakaopotea.
 
... Lazaro aliyefufuliwa na Yesu (by then Yesu akiwa duniani) na Lazaro aliyekuwa na Ibrahim mbinguni na tajiri akiwa kuzimu (by then Musa akiwa duniani). Hao ni Lazaro wawili.
Kwahy Lazaro aliyekuwa na Ibrahim hakufufuliwa.?
 
Huwezi kufafanuliwa, yani hivi vitabu mfano wake ni sawa na Nyerere mwaka 1960 anazungumzia jinsi alivyokufa na msiba wake mwaka 1999.

Ni ngumu sana kwa mtu anayetumia akili na logic kuviamini vitabu hivi, hasa kile cha Quran ndio magumashi matupu.
Ngoja nimuite huyo muumini wa hicho kitabu FaizaFoxy
 
... ule mfano wa Yesu kuhusu maskini Lazaro kifuani pa Ibrahimu tunaona yule tajiri kule kuzimu akikumbuka ndugu zake aliowaacha duniani. Ufafanuzi tafadhali.
Ushasema mfano alichokuwa anazungumzia sio kifo halisi
 
Kwahy Lazaro aliyekuwa na Ibrahim hakufufuliwa.?
Hao ni Lazaro wawili tofauti Mkuu tena wa nyakati mbili tofauti kabisa. Lazaro wa Ibrahim akiwa peponi, Musa yuko duniani.

Musa yuko duniani ni maelfu ya miaka Yesu hajaja wala Lazaro mfufuliwa na Yesu hajakuwepo bado.
 
Kifo ni usingizi mzito au ni kinyume Cha kutokuwepo,ukifa huwezi hisi chochote so usifikirie hizo habari za moto wa milele cjuw huo n uwongo.
 
Simulizi hii ya Yesu inaonyesha hili ni jambo kamili lilitokea haikuwa hadithi ya kutungwa kama ile hadithi ya Msamaria mwema
Huo ulikuwa mfano anawapa onyo Mafarsiayo waliokuwa wanajihesabia haki. Mafarisayo ni kama matajiri na Lazaro kama watu wa kawaida. Moto na mateso ya mafarisayo ni mahubiri waliyokuwa wanahubiriwa. Mahubiri ambayo yanawachoma lakini, mahubiri waliyoyakayakataa lakini yakakubaliwa na watu wa kawaida kama wavuvi.
 
Nasikia alikuwa mi mtu wa madeni so watu hawakua na time ya kuhoji aliyoyaona huko alikokua.

Raia walimkomalia arudishe pesa zao maana alifikiri amewakomoa alivyokufa.
 
Huo ulikuwa mfano anawapa onyo Mafarsiayo waliokuwa wanajihesabia haki. Mafarisayo ni kama matajiri na Lazaro kama watu wa kawaida. Moto na mateso ya mafarisayo ni mahubiri waliyokuwa wanahubiriwa. Mahubiri ambayo yanawachoma lakini, mahubiri waliyoyakayakataa lakini yakakubaliwa na watu wa kawaida kama wavuvi.
Ni kitu gani kinawafanya majority ya wayahudi wamkatae Yesu mpaka leo
 
Back
Top Bottom