Hivi mchina ana technolojia gani ya kumsinda Mmarekani?

Ni kweli Gini Coeficient ya Marekani ni kubwa kidogo kuliko China , hii imechangizwa na aina ya mfumo wa ki utawala , Marekani ni Capitalist while China ni Communist , lakini kama tukichukulia huo mfumo kama irrelevant utagundua kwamba Sera ya Mchina ni Quantity Exportations while USA ni Quality Exportations ... ukitofautisha hizo sera mbili utagundua kwamba inahitajika mtaji mdogo kutengeneza bidhaa za ubora wa Chini kwa ajili ya kusafirisha na hapa inambidi mfanya biashara kutengeneza kwa wingi kusafirisha nje ili apate faida , Quality exportations yenyewe inahitajika.mtaji mkubwa kutengeneza bidhaa yenye ubora wa hali ya juu, faida ya hii ni kwamba haihitaji kusafirisha sana ili upate faida ndio maana leo hii unamuona mtu kama.Elon anapata faida sana kupitia Tesla licha ya magari yake kutoonekana kabisa katika baadhi ya nchi za Africa.
Sasa ukishatengeneza kitu quality moja kwa moja unalenga wateja wa Middle class to high class na Vice Versa.
Hapa haimaanishi China hawatengenezi vitu quality lakini siku zote sokoni kabla ya Ubora wa kitu watu wanaangalia hisia zinazoambatana na kile kitu Mfano Xiaomi ana simu yenye uwezo mkubwa tena toleo la mwisho lakini ukamletea mtu simu hizo mbili na toleo la I phone 14 Pro max umwambie achague nakuambia hata wewe utaichukua I phone licha ya ubora na Highend ya Xiaomi.
 
Mkuu kitu ambacho hukijui ni kwamba thamani ya mtumiaji wa tiktok wa Marekani ni sawa na watumiaji kama mia hivi wa Bongo(Afrika)[emoji1][emoji1]...Hii taarifa Tiktok hawezi kuweka wazi lakini ukweli ni kwamba watumiaji wengi wa Marekani ndio wanaongoza kwa kufanya Donations kwenda kwa Content creator na kutoa endorsement, kama huamini uliza hao ma'content creator , Wewe unadhani Kampuni inamjali nani kati ya hawa ambae ameifurahia Content na kutoa donation ya Dola 10 au Mbongo ambae ameifurahia Content na kulike na kujichekesha kwenye comment[emoji1]
Tukija kwenye Tenda mkuu hatufanyi bishara kuonekana tuna bidhaa dukani bali tunafanya biashara kuuza .. Mteja wa kitanzania anaedunduliza huwezi muuzia sabufa ya Milioni moja iliotengenezwa Marekani kwa ajili ya Mziki mzuri si kheri achukue hizo Earthquake detonator za kichina kwa laki tu[emoji1]
Pia umbali mkuu Marekani ni mbali kuliko China.
 
Marekani kama anajiamini si aondoe vikwazo?

Achana na wachina mzee, wale jamaa hawafai
 
USA hayupo vema kama anavyodai. Kwasababu kwanza ana madeni makubwa sana ya ndani na uchumi wake unategemea wizi wa resources kutoka mataifa ya uchumi wa chini kama Tanzania, Congo, Iraq, etc.

US ni waongo waongo hivi. Labda kwenye eneo la entertainment atakuwa anaongoza dunia nzima na ulimwengu wa taalumu especially tertiary industry na corporate world US yupo vema sana. Si unaona ma software, maprogram,ubunifu, technology, mbinu za biashara US yupo vema sana hilo eneo.
 
Ishu ni kushindwa sasa vikwazo vya nn? wenzenu wana free market nendeni mkapambane ... leo kila kitu mchina kashapigwa gap mtu wako kabaki kuweka vikwazo ambavyo havifanyi kazi
 
Ki uchumi huwezi fanikiwa bila kuwa mwizi na mjanja hivi , Anaemzidi mwenzake mbinu za wizi na ujanja ndio anafanikiwa , licha ya hayo madeni lakini ndio taifa lenye stable economy dunia nzima achana na namba za mitandaoni angalia maisha ya wananchi wake , Ni rahisi Foreigner kufanikiwa Marekani kuliko China.
 
Ishu ni kushindwa sasa vikwazo vya nn? wenzenu wana free market nendeni mkapambane ... leo kila kitu mchina kashapigwa gap mtu wako kabaki kuweka vikwazo ambavyo havifanyi kazi
Ubabe mkuu
 
China inaizidi Marekani kwa sababu ya gharama nafuu za wafanyakazi na wataalamu(cheap labour) pamoja na urahisi wa upatikanaji malighafi, sio kwa sababu ya ku advance kwenye scientific knowledge kuliko Marekani, ndio maana hata makampuni mengi ya teknolojia ya Marekani yameenda kufungua viwanda huko.
 
Tekno
Hata hiyo teknolojia ya Semicondutor ya Taiwan imetoka Marekani na Ulaya na wataalamu wake wengi wamesoma MIT, Stanford na Havard
 
Umenena vizuri sana..... USA anapika sana data..... Taarifa zake hazina ukweli kivile.
Taarifa zote za dunia unazipata kupitia USA, huko China hata Google, WhatsApp na mitandao mengine haifanyi kazi, imezuiwa na serikali ya Kikomunisti.
 
And that is to name just a few..., China ina History ndefu sana USA ya leo ni taifa la jana tu kulinganisha na China
USA ni taifa la Miaka 246 wakati China ni Taifa la zaidi ya miaka 4000.
 
Lakini na kuuza hivyo kila mahali afrika, mauzo yake afrika hayafiki hata 7% ya mauzo yake ya jumla. Hii inaonyesha tulivyo na low purchasing power. Mfano mwaka 2022, Afrika ilipo kiasi cha 4.6% ya bidhaa ambazo china ili export nje. Yani na yale matakataka yote ya kariakoo bado hatufiki asilimia hata 10
 
China inaizidi Marekani kwa sababu ya gharama nafuu za wafanyakazi na wataalamu(cheap labour) pamoja na urahisi wa upatikanaji malighaf
Malighafi hata India na Marekani zipo na nchi nyingine.

China ni moja ya taifa ambalo linaimport sana materials kutoka nje mfano pamba zinatoka Marekani na Canada zinaenda kutengenezwa nguo China

China ina cha zaidi kinachofanya wawe the largest industrial capacity duniani na manufacturers waende kuwekeza
●R&D centres
●skilled personnel
●supply chain and logistics
critical technologies kama industrial robots, artificial intelligence, machine learning, computerized algorithms
●strategic location
●Strong business ecosystem
●masuala ya infrastructure
●uhakika wa soko n.k

Ulishawahi kutembela China-based auto factories uone wanavyozalisha?

Hiki ni kiwanda cha magari cha Xiaomi. Xiaomi’s factory produces 40 electric cars every hour — or, one car in 76 seconds — without a single human worker
Your browser is not able to display this video.



Now China uses more robots in factories than the rest of the world combined.


Kwa hizo sababu kwa nini makampuni yasivutiwe kwenda kuwekeza China?

Tangu Marekani wameanza sera ya decoupling wameondoa kampuni zao ngapi China na kuzihamishia India, Vietnam au kwao Marekani?

Propaganda zitaishia tu kuwaambia China kuna cheap labour.

Mbona kuna nchi nyingi sana duniani zina cheap labour hawakwenda kuwekeza?

Ndio ujue China inabaki kuwa the best FDI destination kwa sababu nyingi ikiwepo kubwa ni applicatiion of sci-tech knowledge in manufacturing na skilled personnel

In short China ni full package
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…