Hivi mchina ana technolojia gani ya kumsinda Mmarekani?

Hivi mchina ana technolojia gani ya kumsinda Mmarekani?

V
China anamtishia Marekani kwa biashara inayohusu teknolojia ila sio kwa teknolojia. Teknolojia zote muhimu duniani kuanzia karne ya 18 zimekuwa zinagundulia Marekani na Ulaya. Huko Asia kwenye nchi kama China wamekuwa wakifanya ku copy, reverse engineering na maboresho ya hapa na pale kukakamata soko.
Vipo vilivyogunduliwa Asia (CHINA,JAPAN,PERSIAN GULF).
Usipunje historia.
Vitu vingi vilivyogunduliwa USA ni vichwa vya Germany n.k n.k.
Hata hiyo Boeing muasisi ni MJerumani aitwaje Wilhelm Boeing.
 
Umeona ni kwa kiasi gani hao Tiktok wanavyohangaika ili wasifungiwe , Dunia ni kubwa hii watu kibao lakini wanahaha na Marekani.
Mchina yeye kafungia mitandao ya kijamii nchini kwake , ana watu zaidi ya bilioni na ushee lakini ulisikia wapi Mack Zuckerberg akihangaika na Bunge la China kama Shou anavyohaha[emoji1][emoji1].
Jiulizeni maswali mepesi tu kwanini Marekani kila saa
Hakuna sanctions ambazo USA alimuwekea China zikafanikiwa.
Bali hum back fire tu.
Rejelea kuanzai 5G na Huawei na ishu ya ushuru bandarini.
USA aliathirika kwa kiasi kikubwa pale China alipokataza raw materials zake kutokwenda viwanda vya USA.
Tiktok kuifungia uache kazi ufanye kazi,maana USA ataitaji sapoti ya ULAYA na Ulaya sasa hivi wanamiminika China kuunda nae muungano wa kidiplomasia na kibiashara.
Fuatilia kitu kiitwacho BELT AND ROAD INITIATIVE.
Yani kwasasa USA ni joka la kibisa.
 
Bas ndio ujue Kua USA ndio kama mzee wake
Hamna mkuu,huyo USA tech nyingi anazoringa nazo ni za Ulaya hususan Germany.
Na ukifuatilia katika uwanda wa research hapo USA utakuta wahindi,WaJapan,wayahudi n.k n.k.
China ni mtu ambae anapambana na research mkuu.
 
Facebook, WhatsApp, google havipo China. Mchina alianza yeye kupiga ban
Mchina alipiga ban hivyo vitu baada ya kupigwa Ban ya kutumia google katika simu za HUAWEI.
Hivyo China imelipiza.
Ila kiuhalisia tutake tusitake China ni tishio.
Kama sio tishio USA asingekua anamuandama na vikwazo kila leo,sasa hivi amejiandaa kuzuia gari za umeme za China kutokuuzwa USA.
Hapo utasema nani anamuhofia mwenzie?
 
China inaizidi Marekani kwa sababu ya gharama nafuu za wafanyakazi na wataalamu(cheap labour) pamoja na urahisi wa upatikanaji malighafi, sio kwa sababu ya ku advance kwenye scientific knowledge kuliko Marekani, ndio maana hata makampuni mengi ya teknolojia ya Marekani yameenda kufungua viwanda huko.
Hao USA ukienda kutizama tech zao nyingi za Germany,Japan.
Hata sasa nenda kwenye science centre zao kuna mpaka WaHong Kong.
 
Labda Mimi elimu yangu ndogo, Mchina ana technology gani ya kumzidi USA🇺🇸
Nikiangalia wale mabwana kila sector wapo vizuri.
1) Upande wa ndege hawana mpinzani
2) Mambo ya space science ni hatari
3) Magari ni hatari
4) Micro chips usiseme
5) Computing hawana mpinzani
6) Kwa kilimo ni hatari
7) Kwenye madawa wamo
8) Ujenzi ni hatari
9) Technology ya simu wanatisha

Na mengine mengi tu. Sasa Mimi najiuliza Mchina ana kitu gani cha kuwazidi hawa mabwana.
Upande wa Uchumi kuna gap kubwa mno. USA ana 28.7 trillion USD GDP. Mchina ana 18.5 trillion USD GDP. Gap hiyo ni kubwa.

Anguko LA USA sio Leo wala kesho. Labda miaka Mia mbili Ijayo
Teknoloji aliyonayo China inayoweza kumpa challenge USA, ni "Human Resources"
Angalia hapa

Population of China in 2024 The population of China stood at 1.43 billion in January 2024. Data shows that China's population decreased by 356 thousand (-0.02 percent) between early 2023 and the start of 2024. 49.0 percent of China's population is female, while 51.0 percent of the population is male.

Source:
 
Kila mtu duniani ndoto yake ni kufika nchi ya maziwa na asali- USA 🇺🇲🇺🇲🇺🇲. Rais wa China mwenyewe anacheza green card lottery
 
Hamna mkuu,huyo USA tech nyingi anazoringa nazo ni za Ulaya hususan Germany.
Na ukifuatilia katika uwanda wa research hapo USA utakuta wahindi,WaJapan,wayahudi n.k n.k.
China ni mtu ambae anapambana na research mkuu.
Mchina kakuchanganya tu bidhaa tunazoletewa hapa East kateka soko lakin kwaupande wauvumbuzi tumwachie USa
 
Mchina kakuchanganya tu bidhaa tunazoletewa hapa East kateka soko lakin kwaupande wauvumbuzi tumwachie USa
Ukifuatilia uvumbuzi lazima turudi Asia mkuu na Europe.
Hata sasa centre za research USA ni wengi WaJapan,Wakorea,Wachina,Wahindi na wazungu hasa wa Germany.
Kafuatilie mkuu.
 
Teknoloji aliyonayo China inayoweza kumpa challenge USA, ni "Human Resources"
Angalia hapa

Population of China in 2024 The population of China stood at 1.43 billion in January 2024. Data shows that China's population decreased by 356 thousand (-0.02 percent) between early 2023 and the start of 2024. 49.0 percent of China's population is female, while 51.0 percent of the population is male.

Source:
Mbona Nigeria wana population kubwa Afrika lakini bado ni taifa masikini!?
Population isiokuwa literate inasaidia nini kimaendeleo!?
 
Ukifuatilia uvumbuzi lazima turudi Asia mkuu na Europe.
Hata sasa centre za research USA ni wengi WaJapan,Wakorea,Wachina,Wahindi na wazungu hasa wa Germany.
Kafuatilie mkuu.
We google hapo nani ni more powerful kweny tech.

USA anaanza wengine wanapita humihumo
 
Ninaamini mchina amemuacha usa karibia kwenye kila idara ikiwepo budget. Sote tunajua kuwa usa ana kambi za kijeshi karibia kwenye kila nchi rafiki (
Despite recently closing hundreds of bases in Iraq and Afghanistan, the United States still maintains nearly 800 military bases in more than 70 countries and territories abroad—from giant “Little Americas” to small radar facilities. Britain, France and Russia, by contrast, have about 30 foreign bases combined.

By my calculation, maintaining bases and troops overseas cost $85 to $100 billion in fiscal year 2014; the total with bases and troops in warzones is $160 to $200 billion.) https://www.politico.com/magazine/story/2015/06/us-military-bases-around-the-world-119321/
Ukiondoa hilo, USA wanatumia matrilion ya pesa kwenye kufadhili ugaidi sehemu tofauti tofauti duniani. Ila tukienda kwa mchina, karibia asilimia 95 za bajeti yake, zinatumika kuisogeza nchi mbele kiuchumi.
Turudi kwenye uhalisia, tangu huu mwaka uanze, ni nani ametumia bidhaa ya mmarekani?? Kama wapo, basi walitumia sio zaidi ya bidhaa 3, nadra sana. Je bidhaa kutoka China?? Je umeona barabara na treni ngapi zinajengwa Africa na wakandarasi wa USA??? Ila China, wapo nchi zooote za kiafrica kujenga sio reli, sio trains, sio nyumba bali kila kitu complex wao wamo. USA ana budget kubwa sana, ila haimnifaishi. Fuatilia jinsi baadhi ya barabara na mazingira ndani ya USA yalivyochakaa, ila China yapo?? USA mitaa mwingine ni majunk tupu, ila China hamna huo ushenzi. USA amempiga mchina kwenye kutumiwa kwa pesa yake kama means of exchange duniani, ila kwenye kila sekta isipokuwa matumizi ya kijeshi, USA amegalagazwa kama mtoto wa darasa la 7 anayepigana na tyson mwenyewe.
Bado uwezo mdogo. Bidhaa za Marekani ziatumika sana, sema ujui unatumiaje izi ni bidhaaa ambazo unatumia masaa 24.
Google
Android
Ios
ATM
Visa and master card
GPS
Opera, Google chrome
Kwa iyo America ni zaidi ya wewe uijuavyo
 
Hiyo ni innovation.
Copy na paste wewe kama unaweza.
Ugunduzi/uvumbuzi yaani invention kwenye teknolojia nyingi initially sana hutokea US na Ulaya na baadae kwa kuanzia commercialization ya hizo teknolojia hufanyikia huko huko US na Ulaya ndipo baadae mchina/makampuni ya US/Ulaya hutengeneza bidhaa hizo china kwa gharama/ ndogo ili kuweza kupata faida kubwa mfano Apple. Sasa nenda bidhaa zilezile akiwa amezalisha mchina kwa maana ya brand za kichina (anakopy paste sasa hapo) ni kawaida sana kuwa na quality ya chini ya US na ulaya maana masoko anayotarget mchina yanataka bidhaa za gharama ndogo.

Ndiyo maana utakuta teknolojia ya ndege, simu za mikononi, mezani, computer, mabasi na kingine kibao mchina hajagundua chochote ila ni mzalishaji mkubwa sana leo hii wa bidhaa hizo na nyingine mbalimbali. Mfano haya mabasi ya mwendokasi, mabus ya yutong, malori howo, sinotruck ubora huwezi linganisha na brand za US au Europe ila yanafaida kubwa kwa mfanyabiashara na hata mtumiaji hasa nchi za dunia ya 3.

Kwa hiyo kwa maana ya ugunduzi wa teknolojia mbalimbali kwa ujumla wake China bado hajaifikia US na Europe. Ila kwa maana ya mass production tena wa ghara ndogo ni ukweli ulio wazi China kamzidi US na Ulaya.

Kwa hiyo hiyo innovation unayosema wewe basically mchina hucopy alichofanya mwingine na kuangalia material gani aweke ili apunguze gharama za uzalishaji au feature ipi aongeze then aweze uza kwa gharama ya chini kuliko wazalishaji wengine wa bidhaa hizo. Ndo simu kama itel,tecno,infinix utawakuta hapo.

Ila kwa level aliyofikia mchina yupo vizuri sana na ataendelea kufanya vizuri maana kateka soko la dunia.
 
Teknoloji aliyonayo China inayoweza kumpa challenge USA, ni "Human Resources"
Angalia hapa

Population of China in 2024 The population of China stood at 1.43 billion in January 2024. Data shows that China's population decreased by 356 thousand (-0.02 percent) between early 2023 and the start of 2024. 49.0 percent of China's population is female, while 51.0 percent of the population is male.

Source:
Huu ndo ukweli ambao watu hawataki kuukubali. China ana cheap skilled labor force ambayo imemsaidia kuvutia kampuni nyingi kwenda kuzalisha vitu nchini kwake kama ilivyo kwa nchi nyingi za Asia.
Hiki kimsaidia China kuwa na access ya teknolojia kutoka sehemu mbalimbali na kuweza kuitumia.
Shida ya USA na China ipo upande wa biashara kutoka na china kuendelea kushusha thamani ya pesa yake kitu ambacho kinaifanya kuvutia uwekezaji mwingi zaidi na kufanya bidhaa zake ziwe na bei rahisi ukilinganisha na za USA. Ukiangalia kwenye orodha ya nchi ambazo zina teknolojia ya juu China humkuti tano bora.

Michango mingi watu wanaiponda USA kutoka na chuki zao binafsi
 
Back
Top Bottom