Ugunduzi/uvumbuzi yaani invention kwenye teknolojia nyingi initially sana hutokea US na Ulaya na baadae kwa kuanzia commercialization ya hizo teknolojia hufanyikia huko huko US na Ulaya ndipo baadae mchina/makampuni ya US/Ulaya hutengeneza bidhaa hizo china kwa gharama/ ndogo ili kuweza kupata faida kubwa mfano Apple. Sasa nenda bidhaa zilezile akiwa amezalisha mchina kwa maana ya brand za kichina (anakopy paste sasa hapo) ni kawaida sana kuwa na quality ya chini ya US na ulaya maana masoko anayotarget mchina yanataka bidhaa za gharama ndogo.
Ndiyo maana utakuta teknolojia ya ndege, simu za mikononi, mezani, computer, mabasi na kingine kibao mchina hajagundua chochote ila ni mzalishaji mkubwa sana leo hii wa bidhaa hizo na nyingine mbalimbali. Mfano haya mabasi ya mwendokasi, mabus ya yutong, malori howo, sinotruck ubora huwezi linganisha na brand za US au Europe ila yanafaida kubwa kwa mfanyabiashara na hata mtumiaji hasa nchi za dunia ya 3.
Kwa hiyo kwa maana ya ugunduzi wa teknolojia mbalimbali kwa ujumla wake China bado hajaifikia US na Europe. Ila kwa maana ya mass production tena wa ghara ndogo ni ukweli ulio wazi China kamzidi US na Ulaya.
Kwa hiyo hiyo innovation unayosema wewe basically mchina hucopy alichofanya mwingine na kuangalia material gani aweke ili apunguze gharama za uzalishaji au feature ipi aongeze then aweze uza kwa gharama ya chini kuliko wazalishaji wengine wa bidhaa hizo. Ndo simu kama itel,tecno,infinix utawakuta hapo.
Ila kwa level aliyofikia mchina yupo vizuri sana na ataendelea kufanya vizuri maana kateka soko la dunia.