Hivi mchina ana technolojia gani ya kumsinda Mmarekani?

Uwezo wa ku produce ana muachq USA mbali tu .. EG''USA aki produce 100 per hour basi China and produce 500 per hour
 
Kwa hiyo taifa la china ni ile race au registered citizens? Sasa hizo we chat kwa nini zisiwe maaarufu duniani Kama x na nyinginezo?
 
Kwa hiyo taifa la china ni ile race au registered citizens? Sasa hizo we chat kwa nini zisiwe maaarufu duniani Kama x na nyinginezo?
Tiktok ni maarufu kuliko hizo takataka nyingine, wechat inatumika china mtandao wao ahwaatumii vya mzungu , nenda korea wana mitandao yao .
Nimekuambia uliza watu wanaoagiza vitu china mara nyingi wanatumia mtandao gani, ile Alibaba ni mzungu sio?
 
Mchina kazi yake ni ku-copy ama kuiba kwa hao hao wama gharibi.

Lakini pia jiulize swali moja, kwanini sasahivi Marekani na ulaya wanaweweseka dhidi ya mchina.

Huyo mchina ana nini hadi waweweseke ?

Sasa sera za Marekani na umoja wa ulaya ni "kukabiliana dhidi ya kitisho cha china"

Huyo mchina ana nini hadi wao waweseke na kuunda masera kibao na kuuzita kuwa "za kukabiliana na kitisho cha china"

Nafikiri kuna kitu china ana wazidi westerners na ndiyo maana wana jihami
 
Mkuu unadhani mtu wa Low income wa leo ataendelea kuwa wa Low income miaka ijayo , ukimuona mtu kanunua kitu cha bei rahisi sio kwasababu anakipenda ila ni kwamba hela hana , siku akiwa nazo jua huyo sio mteja wako.
Hio Mass production unayozungumzia ni kwa hapa Africa tu , ndio soko ambalo mchina anatengeneza kila uchafu na kuwatelea vingine vina hadi madhara ila ndio hivyo huwezi ona madhara yake kwa muda mfupi..
Bidhaa zote ambazo mchina anapeleka Ulaya , Amerika ya Kusini na Kaskazini ni high quality na huko anasua sua maana watu washamonopolise soko
 
Upo kishabiki sana mkuu impact ya hio Belt Road and initiatives ni ipi haswa , USA inalazimika kuziwekea baadhi ya kampuni za China kutokana na Sera za taifa ,China kampuni inaweza kuwa na nguvu lakini bado mambo yake mengi yanakuwa influenced na Serikali ,unadhani communist party ikiamua kutaka kupata taarifa za mtumiaji flani wa Tiktok wa Kimarekani inashindwa ,ogopa sana kampuni ambazo zipo chini ya sera ya Socialist Market economy.
Dunia inakoelekea haihitaji Socialist Market economy bali inahitaji free market economy na Marekani licha ya kuwa kwenye Mixed Economy ila uhuru wa kisoko upo.
Hebu nenda kafuatilie Hotuba ya Raisi wa Argentina Javier Miller juu ya Free Market economy kwanza.
China haitoweza kumzidi Marekani labda itokee aondokane na mfumo wa kikomunisti na kuingia kwenye Pure Capitalism.
 
China hatoweza kumzidi USA in which aspects!?
Kama ni trade amekwishamzidi mkuu,siongei kishabiki naongea nachokijua buddah.
Tuanzie ushawishi wa kibiashara/kifedha,Benki kuu ya China inaonekana kuwa ni bora na nafuu kulipa kuliko IMF/WB.
Mpaka sasa China imekopesha mataifa 138+ na kusamehe mataifa 38 madeni,na bado mataifa yanamiminika kukopa China na ukanda unaomiminika ni wa South East Asia,Eastern Europe na South America.
Kibiashara China hakuna sehemu bidhaa zake haziukizi,tena hususan Afrika ndio tumejaza bidhaa za Mchina kuliko bara lolote.
-Kidiplomasia China amekua mwenye kusikilizwa sana kipindi hiki,na hata baadhi ya migogoro yeye ndio amekua mtatuzi,mataifa mengi sasa hivi masuala ya kidiplomasia hufanya reference ya China,na wanaipongeza China kwasababu haingilii ITERNAL SOVEREIGNTY ya taifa lolote,sio kama USA anaenda mbali kiasi kufadhili mapinduzi ya serikali za watu.

Ni wapi unasema China hajamzidi USA?
Belt and road initiative ni mpango wa kibiashara na ujengaji wa miundombinu kwa gharama nafuu baina ya China na mshirika wake yeyote atakayehitaji kuingia nae makubaliano.
Eastern Europe imejengwa sana na China kupitia Belt and road pia biashara nyingi Eastern Europe zime prosper kwa initiative ya belt and road.

Namalizia kusema hivi mkuu,China sio taifa jepesi kama udhaniavyo.
Kaa lifuatilie vizuri mkuu.
Chancellor wa Germany kwenda China hakuwenda kiwepesi.
France officials kwenda China hawakuenda kiwepesi,tena inasemekana ni zaidi ya 20+ years hao watu hawakukanyaga China.
We endelea kuwa understimate mkuu.
 
Wanatumia zile zile za, magharibi, lakini wanazalisha bidhaa kwa bei nafuu, mfano kwenye EVs electrical vehicles, Za, china zina bei nafuu kuliko za, America na ulaya
 
Tiktok ni maarufu kuliko hizo takataka nyingine, wechat inatumika china mtandao wao ahwaatumii vya mzungu , nenda korea wana mitandao yao .
Nimekuambia uliza watu wanaoagiza vitu china mara nyingi wanatumia mtandao gani, ile Alibaba ni mzungu sio?
Una mahaba ya ajabu ngoja nikwambie tech nyingi zilizopo leo chanzo ni USA hilo huwezi kataa
Hapa tunaongelea mwanzilishi wengine wanadevelop tu!
Hivi warusi wangejuaje kuna nuclear bombs Kama wasingeona yakipigwa Nagasaki au Hiroshima .hao tiktok waliiga wapi? Ni sawa leo uanzishe biashara yako halafu wengine waige waimodify kwa kusoma udhaifu wa biashara yako. Halafu wapewe credit wao walikuwa wapi kuibuni? Ndo maana tunasema tech nyingi zinaanziaga west then east wanatwist na kuzinogesha
 
Maeneo ambayo Mchina kaachwa mbali :
1.Semiconductor.
2.Software development
3.Biotechnology and Pharmaceutical: Mfano tu maswala ya Corona.
4.Aerospace : Hapa China anakuja kuja nyuma ya Mrusi, baba yake USA yuko mbele .
Hivyo ni vipengele vichache tu upande wa Tech , twende kwenye international trade hapa Dollar ya Kimarekani katika ku'conclude international transfer hana mpinzani , China amefanya counterattack kwa kutengeneza BRICS na mwenzake Mrusi lakini Dola haijadeppreciate value yake , Uliza wafanya biashara wa Bongo walivyokuwa wakihaha kuitafuta Dola Benki ili wakafungashe.
Makampuni makubwa ya International transaction yapo chini ya Wamarekani hapa tunapoongea una Kadi yako ya Mastercard Au Visa Card mfukoni , Hio kadi ipo chini ya Mmarekani.
Upande wa Product manufuctering China anamfukuzia kwa nyuma Mmarekani sikatai lakini ukweli ni kwamba yupo nyuma sana kwenye swala la Ubora wa Bidhaa zake.
Kijeshi hapa haina haja ya Kuongea ukienda Japani unaikuta Kambi ya Jeshi la Marekani , Ukienda Korea unaikuta bado hujazungumzia teknolojia ya Siraha na kuendelea, Bado hujazungumzia NATO na mengineyo.
Ni kweli China imepiga hatua kwenye mambo mengi lakini tusiongee kishabiki kiasi cha kuexaggarate facts
 
Vizuri mkuu,wacha nipite kwenye point zako.
Kipengele cha kwanza na chapili na kubali,japo China naye ameshaanza kupiga hatua kuja juu katika hizo sehemu,na hatua yake ndio inayomuumiza kichwa USA.
Tukija katika masuala ya kitiba kiujumla iwe biotech,pharmaceuticals iwe masuala ya epidemiology China kapiga hatua kuliko USA.
Kama ulifuatilia Corona China ilichukua siku 90 kuidhibiti corona,vifo vilipungua na maambukizi yalikua yenye kudhibitiwa.
Vifo vingi vilitokea mwanzo wa eruption ya Covid 19.Ila baadae China iliweza kudhibiti usambaaji wa Corona.
Tukija kwa USA,Spain na Italy ndio waliokuja kuongoza kwa vifo na iliwachukua muda kudhibiti Corona.
China ndio nchi pekee ulimwenguni wenye uwezo wa kupambana na aina nyingi za saratani tena kwa tiba za kisasa na kienyeji.
Na ulimwenguni China pekee ndiye aliyeendelea katika herbal science.
Upande wa afya China yuko mbele zaidi kaifuatilie mkuu.
Kuhusu aerospace nakubali japo China anapiga hatua kali kuja hilo eneo katika fighter jets kashakamilika ila katika ndege za abiria bado ndio anajitafuta ila soon anakuja walipo wengine.

Kuhusu dollar kuwa medium of exchange hilo halipingwi kuna factors nyingi zinazofanya dollar bado kuwa na nguvu,japo kukosekana kwa dollar kunatuathiri sisi nchi za ulimwengu wa tatu.

Kuhusu manufacturing CHINA HANA MPINZANI,China is the most industrialized nation na inachangia zaidi ya 32% ya manufacturing goods ulimwenguni,kalifuatilie hili mkuu.
Kiubora China huwenda anazidiwa na Germany na Japan ila sio USA.
China ana uwezo wa kuunda bidhaa zenye ubora kama wa USA na amethibitisha hilo katika soko.
Tesla EV zimeonekana kuwa na ufanisi mdogo chini ya Chinese EVs.
 
Kuhusu jeshi kaka wacha nimalizie.
China ni jeshi lenye silaha bora na zenye ufanisi pia,isipokua haiji promote kama USA.
Hivi unajua kama USA na China waliwahi pimana ubavu kupitia proxies na USA akashindwa!?
Rejelea vita ya Korea war 1950s.
Jeshi la China iliisaidia North Korea na 1959 USA ilipoteza askari wengi sana Jangsari kiasi ili retreat mpaka eneo ambalo sasa linaitwa demilitarized region.
Ndio maana Kule South China sea China kapora mipaka ya maji ya Phillipines ila USA hakufanya hatua yeyote.
Silaha za China zimeuzwa na kufanya ufanisi sehemu nyingi sana.
Technology ya silaha anayotumia North Korea 90% ni kutoka China.
Kamfuatilie huyu jamaa anaitwa NAPOLEON BONAPARTE,aliwahi kusema "China is a sleeping lion,if when it wakes the world will shake".
 
Anasuasua au wanamuundia zengwe asuesue!?
 
Approach ya Vita miaka 50 na sasa hivi ni tofauti sana , ,teknolojia imepiga hatua , Vita za Enzi hizo zimekuwa historia katika vitabu na sio kwenye uwanja wa Vita
Sasa hivi China kuwa na teknolonia kubwa kwenye Siraha imekuwa ni kama Uvumi tu kwasababu hatujaziona zikiwa zinafanya kazi, Ni kheri Mmarekani ambaye anajaribisha baadhi ya Siraha zake pale Ukraine kwa kigezo cha kutoa msaada.
Kuilinganisha nchi na nchi kijeshi ni swala Complex sana kwasababu hakuna nchi ambayo itaweka wazi teknolojia zake
 
Sawa mkuu ila mbona China anauza silaha nchi tofauti na zinafanya kazi?
Au nilete mfano mkuu?
 
Mngekuwa mnafuatilia na kujua mambo mengi ya nchi zenu tungekuwa mbali. M'bongo ukitaka aharishe kila kitu na aingie kwenye mjadala mletee mijadala ya aina hii. 1. Kati ya fulani na fulani nani ni tajiri zaidi? Kati ya nchi fulani na fulani ipi imeendelea zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…