Nianze kwa kusema Nimeishi Arusha,Mwanza ,Dar Moshi, na saivi nipo Dodoma una elekea Mwaka sasa nipo uku kwa sababu za kikazi.
HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua ,mchana kuna jua kali sana na vumbi afu jion na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .
MAKAZI
kwa saivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabsa ,Sizani ata kama wana tumia ramani kwenye kujenga maana wana jenga ma nyumba makubwa kama makubwa jinga afu mabaya hajapakwi rangi wala kupigwa lipu yana achwa ivyo ivyo. na madirishani wakiweka mifuko ya cement ,mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu
Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki
USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM .au STK etc uku hakufai usafiri aueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .
MAJI
Kwa mala ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi l. kama huna kazi apakufai .maji ya kunywa ni ununue bila ivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha .
KAZI
Dodoma ofisi nyingi zina amia uku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar,Mwanza na Arusha uku uta pauka dk 2 baada ya kushuka stand
MWISHO
nisipo ona ata mvua hii miezi ilio baki ata kwa mganga taenda nihame ofisi