Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Kumtafakari Mungu kwa njia ya kibiblia ni kusema Mungu ni Alfa na Omega, alikuwepo kabla ya ulimwengu ni muumba wa vyote, mmiliki wa vyote na mwenye huruma na upendo wa Agape.
Ila ukimtafakari nje ya Biblia unaona Mungu sio kiumbe kinachoshikika ila ni nguvu chanya inayoishi all over the universal ni nguvu inayotusukuma kutenda mema tukiipa nafasi ya kuitumia na tutafanya makubwa ambayo its beyond our mindset, positive energy hutuimarisha na kutupatia ustawi wa maendeleo yetu kama binadamu na viumbe kwa ujumla wake nje ya hapo ni nguvu kinzani ambayo ni hasi.

Kiimani ibilisi ni mkuu wa uharibifu wote, ubaya wote ambapo tukienda nje ya imani ibilisi ni negative energy that can be driven by our selves also tofauti ya hii nguvu na ile chanya ni mipaka ya kiutawala, nguvu hasi is within our mindset haina matokeo makubwa kuliko uwezo wetu wa kufikiri kama hivyo ndivyo uwepo wa nguvu hizi unategemeana ili kutoa muafaka wa ipi ni kuu kuliko nyingine.

All the bad did laying on negative energy na matokeo yake hayana ustawi wa maendeleo ya watu zaidi ya kuangamiza… ndio maana tunasema positive energy hufanya kazi vizuri zaidi ikiwa unajifunza maarifa mapya kila wakati (kiimani soma Biblia na nje ya imani soma vitabu vya kiada, machapisho ya tafiti na fasihi andishi kwa ujumla wake), ukikuza uwezo wako wa kifikira ni rahisi kufikia ustawi, ujinga ni negative energy hufifisha ustawi wa maisha, ujinga huzuia wigo wa kifikira (Biblia hutoa onyo “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” kukosa maarifa hufanya akili kuwa tegemezi wengine wafikiri kwa niaba yako… huu ni ujinga maana unaruhusu kuendeshwa, utadhibiwa, utachomwa moto, utakanyagwa, utaporwa mali zako utalishwa chumvi, utakanyagishwa mafuta, utapewa ahadi za wake 40 after life nk.

Kosa la Adamu na Hawa ni matokeo ya ujinga, hawakufuata maelekezo waliyopewa na Mungu usile tunda la mti wa katikati wao wakala na kusingizia etu ni ibilisi kawadanganya... maana yake waliacha ibilisi afikiri kwa niaba yao walipuuza maelekezo... hata wewe kwenye maisha ya kawaida puuza maelekezo uone kitakacho kutokea ... hatua fulani zitachukuliwa (positive energy will rule against negative energy) iwe ni kwa nia ya kukuonya, kukufunza, kukuelimisha au kukuadabisha. If God is negative energy will rule everything in the universal ....thanks​
Umefafanua vizuri sana mkuu, hakika upo positive mno. Binafsi kuna kitu nimejifunza kwenye comment yako hii Barikiwa.
 
Hii ndio maana ya ujio wa Kristo Yesu kuondoa hasira ya Mungu kwa wanadamu ili kuwe na upatanishi. Na baada ya kristo adhabu za moja kwa moja zilikomeshwa.
 
Mungu kwanini asimwangamize shetani ili na sisi tupumzike na haya mateso???
 
Hakuna pepo ya mteremko tufanye Ibada! We ulitaka uzaliwe,Ufe kisha Uende peponi Kirahisi rahisi Tu....Fanya ibada ukimshinda Ibilisi pepo Inakusubiri.
 
Chanzo cha Iblis , Adam na Hawa kutupwa duniani

Mara baada ya iblis kugoma hata kuomba msamaha na kutubu kwa Mola wake, ndipo akapokea laana. Hii ni majibu kwanini Mungu hakumsamehe Iblis. Jibu ni kuwa Iblis hakutaka kusamehewa. Yeye kuambiwa amsujudie Adam aliona kuwa ni udhalili uliopindukia mipaka na mpaka kesho bado anajiona kuwa yeye ni bora kutokana na kuumbwa kwa Moto.

Makazi ya Adam yakawa ni katika bustani ya Eden,na baadae akaumbiwa mke kutokana na ubavu wake wa kushoto, bi Hawa.

Iblis nae alikuwa akiishi huko huko juu na pia alikuwa akipata nafasi ya kuzungukia bustani hiyo ya Eden.

Masharti aliyopewa Adam na mkewe ni kuwa wale kila kotu kizuri ndani ya bustani hiyo ila wasile tunda la mti mmoja tu. Waliishi hivyo ila iblis kutokana na kujua kuwa ni ngumu kumuingia Adam na kumshawishi ,akaamua amuendee mkewe na kujifanya kuwa ni mshauri mzuri kwao, kwa kumuuliza kuwa anajua kwanini wameambiwa kuws wasile tunda la mti ule? Hawa hakufahamu chochote ndipo Iblis akamwambia kuwa mmekatazwa wewe na mumeo msile tunda lile kwasababu mkila tu mtakuwa kama malaika na mtaishi milele hamtakufa.

Kwakuwa eden kulikuwa na starehe na raha tele, hakuna nafsi ya mwanadamu ingependa kusikia kuwa ipo siku itakufa na kuziacha raha na starehe za bustani hiyo, ndipo bibie Hawa akamfata mumewe na kuanza kumshawishi kuwa wale tunda hilo ili wasife. Adam kwa udhaifu wake akamskiliza mkewe na kwa pamoja wakala tunda lile ,ghafla mavazi mazuri waliyopewa na Mungu yaliwatoka na wakajikuta kuwa wapo utupu, hivyo wakawa wanatafuta majani ya miti humo bustanini ili wajihifadhi miili yao.Kwa aibu Adam akawa amejificha huku akijuta kwanini amekula tunda lile waliloshauriwa na Iblis. Iblis kwa upande wake alifurahi mno na kuanza kumuuliza Mungu kuwa yupo wapi kiumbe uliyemfanya bora kuliko mimi ona sasa amekuasi kwa kula tunda ulilomkataza asilile?

Mungu akamuita Adam aliyekuwa amejificha kwenye miti, na kumuuliza kwanini amefanya yale aliyomkataza, ADAM hakuwa na la kujibu bali alidondoka chini na kuomba msamaha na kutubu kwa Mola wake. Kutokana na kujishusha kwao yeye na mkewe, Mungu aliwakubalia toba zao.

Ila sasa kile kipaumbele cha kuishi bustanini kikawa kimeishia pale na wakaambiwa kuwa watateremshwa duniani huko ndipo watakuta kila kitu chao, wataishi huko na muongozo wa Mungu utawafata huko na mwisho watakufa na kurejea kwa Mola wao tena. Na wakaambiwa kuwa hakika Iblis ni adui kwenu na nyinyi mfanyeni kuwa ni adui,msimsikilize kwa lolote atakalowaambia ama kuwashauri.

Wote watatu kuanzia hapo wakashushwa duniani, adam,hawa na iblis.

asante sana kwa elimu hii
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tenda mema usipigwe moto.
alafu siku ya kiama unapigwa moto na uyo ibilisi,wengine hatumjui hata anafananaje.kwa kweli hao kina adam angemalizana nao uko eden sio kutuuzia kesi yao ambao hatukuepo
 
Hii sirediiiiiiiiiii au ngoja kwanza
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Historia fupi ya Iblis na uasi wake.

Iblis ni jini na hakuwa malaika licha ya kuwa alipata kipaumbele cha kuishi pamoja na malaika huko mbinguni. Iblis alinyanyuliwa na malaika akiwa ni kiumbe mchanga sana katika dunia hii mara baada ya malaika kutumwa kuja kuwaangamiza majini waliokuwa wakifanya uasi hapa duniani,ikumbukwe kuwa majini walipata kuishi katika dunia hii miaka mingi kabla ya uumbwaji wa mwanadamu ila walikengeuka na kufanya ufisadi mwingi sana. Iblis aliachwa na wazazi wake hivyo malaika wakaomba idhini kwa Mungu waondoke nae wakamlee huko mbinguni.Walikubaliwa na hatimaye iblis alikua katika mikono ya malaika , na alipata elimu kubwa tu na pia alikuwa ni kiumbe mchamungu sana.Mtume Muhammad (sala na amani ziwe juu yake) alinukuliwa akisema kuwa hapana sehemu yoyote katika ardhi hii yenye ukubwa wa kiganja cha mkono isipokuwa iblis aliinamisha paji lake la uso chini na kumsujudia Mungu.Alikuwa ni kiumbe aliyefanya sana ibada ila ndani yake alikuwa na kibri/majivuno ambayo malaika hawakuweza kuyajua ila Mungu alimjua kwasababu alimuumba kwa moto na sio Nuru kama ilivyokuwa kwa malaika.

Baada ya majini kufanya uasi na kufurushwa huku duniani ,Mungu akaamua kuumba kiumbe mwingine ambae atakuja kuwa mtawala katika ardhi hii, nae si mwingine bali ni ADAM. Uumbwaji wa adam ulitokana na udongo mweusi wa mfinyanzi tena uliovunda. Ndio asili ya mwanadamu.

Adam aliumbwa kwanza kama fremu tu ambalo lilikuwa halijapuliziwa roho, Iblis alikuwa akiliona fremu la kiumbe huyu mpya wa ajabu, kisha alikuwa akilizunguka na kupita ndani ya mwili wake na kisha kutoka kisha akajisemea kuwa hakika huyu ni kiumbe dhaifu sana na pindi atakapopuliziwa roho basi mimi ndio ntakuwa mwalimu wake.

Malaika mwanzo walikuwa na wasiwasi juu ya kiumbe huyu mpya kuwa pindi atakapoumbwa na kukabidhiwa utawala huku duniani basi atakuja kuyafanya yale waliyoyafanya majini (uasi na umwagaji damu) ila Mungu alikuwa against na maono yao na akawaambia kuwa hakika anayajua yale ambayo malaika hawayajui.Adam akakamilika kuumbwa kisha Mungu akampulizia roho na haraka adam akapata uhai. Kitu cha kwanza Mungu alichompa Adam ni ELIMU. Utambuzi wa kujua kila kitu mpk vile ambavyo malaika hawavijui. Kisha akawaita Malaika,iblis na Adam wote wahudhurie kwani kuna mtihani anataka kuwapa.Mungu alivileta vitu vingi kisha akawaambia malaika pamoja na iblis wavitaje vitu hivyo.Malaika na iblis pamoja wakashindwa kwani walikuwa hawana elimu navyo basi akaitwa Adam akaambiwa kuwa watajie majina ya hivyo vitu, Adam akataja kila kitu kwa usahihi kabisa na alifaulu ule mtihani ndipo Mungu akawaamrisha malaika pamoja na iblis kuwa wamsujudie Adam kumpa heshima. Malaika kutokana na kuwa waliumbwa kwa Nuru na wanafanya yale wanayoamrishwa, basi wote wakasujudu isipokuwa iblis yeye aligoma kusujudu.

Iblis alisimama pamoja na Adam wakati malaika wote wameinamisha mapaji yao ya uso chini, ndipo Mungu akamuuliza Iblis ni nini kilichokufanya uikatae amri yangu?

Iblis akajibu kuwa hakika yeye ni bora kuliko Adam kwani ameumbwa kwa Moto na adam ameumbwa kwa udongo hivyo asingeweza kumsujudia Adam.

Aliiasi amri ya Mola wake mbele ya kundi lote la malaika na licha ya kuasi kwake bado alikataa kurejea kwa mola wake kuomba toba na msamaha. Alishaamua kama mbwai na iwe mbwai. Hapo ndipo MUNGU alipoamua kumlaani Iblis na akafukuzwa kutoka katika kundi la malaika. Iblis aliipokea laana ile ila alikuwa na ombi moja tu kwa Mungu. Mungu akamruhusu aombe anachokitaka ndio akaomba kuwa apewe uhai mrefu mpk mwisho wa dunia hii yaani awe miongoni mwa viumbe vitakavyokufa mwisho.

Mungu alimkubalia , na baada ya ombi lake kupitishwa kwa hasira akasema kwa kuwa Adam ndio amesababisha Mungu kumlaani basi atahakikisha kuwa anavikalia mbele,nyuma,kushoto na kulia vizazi vya adam ili visiielekee njia ya Mungu, ili mwisho wa siku apate watu wengi wa kuingia nao motoni.

Mungu akamjibu palepale kuwa kwa hakika Iblis hana uwezo wa kupoyosha waja wake isipokuwa kwa yule atakaeamua kumfuata.Na kwa hakika ataijaza jahannam kwa iblis na wale wote watakaomfuata.

Yote haya yanatokea huko mbinguni hakuna kiumbe chochote kilichowahi kumuona Mungu ana kwa ana. Sio Adam,sio malaika wala sio huyo Iblis .Walikuwa wakipokea tu sauti ila hakuna aliyemuona Mungu toka ulimwengu unaumbwa mpk pale utakapoisha.

Mungu atakuja kujidhihirisha kwa waja wake watakaoingia peponi tu ndio watapata kumuona. Na hakuna zawadi kubwa mwanadamu atawahi kuipata kama nafasi ya kumuona Mola wake. Mungu atujaalie tuwe miongoni mwao ameen.
Ulishamuona ibilisi wewe?
 
hii ni kwa mujibu wa kitabu gani? kwenye quran imeandikwa ibilisi aliambiwa amsujudie adam (abaa wastakbar) akakataa na akafanya kiburi ndipo Mungu akakasirika akamtupa duniani
Ibilisi alitupwa duniani kabla ya kuumbwa Kwa Adam
 
Unapata wapi ujasiri wa kumlaumu Mungu hivi kweli sisi binadamu ndo wakumlaumu Mungu kweli Aiseeee tumefika mbali


Note Mshukuru Mungu kwa kila Jambo
 
hii ni kwa mujibu wa kitabu gani? kwenye quran imeandikwa ibilisi aliambiwa amsujudie adam (abaa wastakbar) akakataa na akafanya kiburi ndipo Mungu akakasirika akamtupa duniani
Manake Adam na shetani walikuwapo mbingu kabla ya uasi?!
 
Back
Top Bottom