Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Tunajua mapenzi yanaendesha Dunia. Tumesikia na kujionea mapenzi yalivyo na nguvu, lakini sina uhakika kama yanaweza kuhamisha milima kama wasemavyo.
Umri uliyonao na mambo uliyokwisha pitia, hivi bado wewe ni wakuendeshwa na mapenzi kweli au umerogwa? Ndugu yangu kubali kukua na ujifunze kutokana na makosa ili usiendeshwe na mapenzi. Kama mwenzi wako anasumbua na bado unampenda, jitahidi umuelewe kisha jiulize unakosea wapi kisha tafuta suluhu.
Na kama ukianzisha mahusiano mengine rekebisha ulipokosea mwanzo, kama yalikutesa usikubali tena mapenzi yazidi akili yako. Inasikitisha unakuta mtu mzima mwenye zaidi ya miaka 27 ameshapitia mengi kwenye mahusiano, alishawahi kutedwa na kusalitiwa.
Lakini akipata mpenzi mpya anakuwa kama mpenzi wa kwanza na wengine wanachora mpaka tatoo, atapiganae picha, kujirekodi video na kuposti kila mahali na caption ndefu "Akiniacha huyu mje kunizika", wakati huo ni mpenzi siyo mke wala mume! Hivi ukiachwa utawaambia nini watu?
Unakuta baba mwenye familia na majukumu kibao bado anaendeshwa na mapenzi ya mchepuko mpaka mkewe anagundua, unajiongezea stress Bure. Sawa dada uliteseka sana kwenye mahusiano yako ya nyuma, alikuliza mpaka ukasema hutopenda tena. Tunajua umempata wakuponya maumivu yako lakini usijisahau huyo siyo malaika.
Sasa ukiendeshwa hivyo na mapenzi na yule mtoto wa dada yako wa kidato cha tatu afanyeje? Mapenzi huleta furaha hasa ukipenda unapopendwa, unaweza kuhisi dunia nzima mzuri peke yako. Lakini hayo hayo mapenzi maumivu yake ni sumu yanaweza kuua.
Mapenzi ni kama chakula kizuri, kula kwa kiasi, ukizidisha utavimbiwa halafu matokeo yake kitakukinai.
Usiache kupenda, lakini penda kiasi kwa faida yako.