Hivi ni haki kwa mke kumficha mumewe password ya simu yake?

Hivi ni haki kwa mke kumficha mumewe password ya simu yake?

Mwanamke kuilinda na kuwa mkali kwenye simu yake hata kwenye mambo mepesi kabisa ni dalili za wazi kuwa kwenye huo msafara wako wa mamba na kenge pia wamo.......

Tafakari chukua hatua......

Usimchunguze lakini usipuuzie viashiria......

Lisemwalo lipo kama halipo laja......

(Talking from experience)......
 
Huwezi kuwa mkuu wa nchi na hapo ikulu kukawa na baadhi ya vyumba hutakiwi kuviona au kuvikagua. Anapokuzuia kuwa na access na simu yake anakuficha nini na kwa faida ya nani.

Km huna ruhusa au una limitations ya baadhi ya vitu vya mke wako ujue hujamuoa. Yaani unatakiwa ujue kila kitu kwenye simu yake maana ya Mungu ni mengi.
 
Nna miaka sita sijabadilisha password hata nikibadilisha simu naweka ileile anayoijua
Mimi pia najua ya kwake
Huyu ni mimi kabisa , mimi mpka namba za mpesa, airtel money na tigopesa tunatumia moja. Yaani nyeupe nyeupe tu.
 
Wakuu kama inavyojulikana kwa kawaida simu ya mke ndiyo simu rasmi kwa kila mwanafamilia (akiwemo baba) kuitumia kwa uhuru kabisa maana vyote (vikiwemo hiyo simu na huyo mke mwenyewe) hivyo ni mali ya baba.

Sasa kama mke/mama hataki kutoa password ya simu imekaaje hiyo?

Kuna ustawi wa familia kweli hapo?

eti wakuu😳?

Mi nimekwazika kwa kweli

Labella
Mahondaw
financial services
Joanah
Ni wapi iliposemwa kuwa simu ya mke ndiyo simu rasmi kwa kila mwanafamilia kuitumia kwa uhuru kabisa? Kwa nini jambo unalotaka wewe liwe hivyo unataka kulifanya kuwa ndivyo lilivyo kwa kila mtu? Kuna kitu kinaitwa privacy katika maisha ya ndoa, kuna vitu huchukui au kutizama bila idhini ya mwenza wako ikiwemo simu hata kama umemnunulia wewe.
 
Kama line imesajiriwa kwa jina lake Yes ana haki ya faragha 100% ni simu yake na password ni mali yake
Hata kama haikusajiliwa kwa jina lake as long as umempa kwa matumizi yake basi ni haki yake na anachokihifadhi katika simu ni faragha yake na ana uamuzi wa mwisho nani atizame na nani asitizame simu yake. Na hata ukiamua kumpokonya simu basi ni haki yake kufuta kila kilicho chake katika simu kabla ya kukurudishia simu yako.
 
Hata kama kanunua mume
Simu yangu ni ya kwangu,hakuna pimbi yoyote anaweza kunieleza azawaizi

Braza Kede simu yangu haiwezi kuwa mali ya kila mwanafamilia mkuu
Kiufupi hakuna mtu kwenye hii dunia anayejua password ya simu yangu
Bado hujaolewa.
 
Moja ya vitu ambavyo haviwezi kunipotezea muda ni kuhangaika na simu ya mke wangu.
Yeye ana simu yake na mimi nina simu yangu.
Nashukuru vile vile kuwa hata yeye hapotezi muda kuhangaika na simu yangu.
 
Back
Top Bottom