Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Basi kama ni hivyo tulitendeeni haki hili jina mkuu,kimaneno na matendo yetu yawe ya kistaarabu sio Mtu anakuita Mkuu na mwisho anamalizia Mkuu wewe ni --------,Mkuu wewe ni PUNGA,Mkuu wewe ni Mburula.
Sasa heshima ya Ukuu iko waph?

Kuitana jf mkuu nikujenga urafiki hatakama mtu kakutusi lakini kwakuwa ameanza na neno mkuu aliyetukanwa hawez kuwa na hasira sana. Ushaur wangu watu waelimishane badala ya matusi maana tunatofautiana uelewa na fikra kwa ujumla.
 
Mbona Kapuya, Nkamia, kibajaji, Mwigulu wanaitwa waheshimiwa?!

Mkuu, hao wakuu uliowataja hawastahili kuitwa waheshimiwa. Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 huyo Kibajaji na Mwigulu walikuwa wanafurumusha matusi makubwa makubwa lakini Mkuu wa nchi hajawakemea kwa huo utovu mkuu wa nidhamu.

Waziri mkuu nae alitoa kauli ya "wapigwe tu", nadhani kwa kauli kama hiyo hakustahili hata kuwa Mkuu wa Mkoa.

Makame, hilo neno hutumiwa kama ishara ya kuheshimiana humu JF kwa hiyo wacha members waendelee kutumia hilo neno mkuu wangu Makame.
 
Horse Shoe Arch,vizuri umefafanua kwa kina juu ya ukuu wa Jf.
Kwakua hata uchangiaji,busara,hekima na ukongwe wa kujiunga na Jf unaonaje kukawa clasfications za huu ukuu wetu.
Inakuaje mtu amejiunga jf miaka 7 nyuma aitwe mkuu na huyu alojiunga jana au leo nao waitwe wakuu?

Kuna wakati nilikuwa sijapata vizuri tafsiri ya mtu mzima na mtu mkubwa,kipindi hicho nikiona mtu mkubwa kimmri nilijua huenda ndiye mtu mzima na akikoleza tena na nywele nyeupe nilkaamini busara zii nae kumbe sikuwa najua vizuri.

Nimekuja kufahamu kuwa binadamu wote waliozaliwa bila mapungufu kibaiolojia ni watu wazima na kwamba suala la ukubwa na udogo ni la kimaumbile tu na kwamba time factor ndiye mpatanishi mkuu kwenye mlinganyo. Kwa maana hiyo nikajiaminisha kuwa busara na hekima mtu aanaweza kuwa nazo angali mtoto na swala la umri likafuata baadaye.

Profesa James Mdee ni baba mzazi wa Halima Mdee ( Mb), Leo Halima ni Mheshimiwa ila babaye mwanazuoni mbobezi siyo mheshimiwa unless otherwise aitwe tu just in case. Kina Mwigulu na watu wa aina yake leo ni waheshimiwa ilihali wanazuoni waliowafundisha kwenye sehemu anuai kielimu hawaja title hizo.

Kwa sababu hiyo basi tukubaliane kwamba hii Mheshimiwa/Mkuu ni tittle tu inayotumika kwa mfumo wa rejesta kwenye maeneo maalum ambayo yakitumika yanasound vyema. Na kwa kuwa tendo la bata kutokuwa na staha nzuri ya kwenda haja haibadilishi kua aina nyingine ya ndege basi hata wenye hulka sizizo na staha na tabia zisizo za kiungwana waendelee kuitwa tu wakuu ila wao ndio wajipime kutokana na tabia zao!
 
Basi kama ni hivyo tulitendeeni haki hili jina mkuu,kimaneno na matendo yetu yawe ya kistaarabu sio Mtu anakuita Mkuu na mwisho anamalizia Mkuu wewe ni --------,Mkuu wewe ni PUNGA,Mkuu wewe ni Mburula.
Sasa heshima ya Ukuu iko waph?
Mkuu isihofu huo wasifu wa mtu,hujawahi kutana na mtu anamsifia mwenzake kwa vionjo vya matusi mfano k¤m~.#ke Kaseja noma kapungua ile penati,hapa Kaseja kacheza fresh ila hilo tusi sijui ndio msisitizo..
 
ni kweli mkuu, mkuu ni MUNGU, ila kwakua sisi ni mfano wake basi si vibaya kuitana wakuu

Umenifurahisha sana mkuu upo sahihi asilimia mia kwa kuwa mungu ni mkuu na sisi tumeumbwa kwa mfano wake, wengine wanasema sisi ni watoto wake mtoto wa nyoka ni nyoka .yeye mkuu na sisi ni wakuu wadogowadogo. Kwa sisi wenyewe kwa wenyewe ni wakuu.kwa mantiki hiyo sisi wote ni wakuu
Mkuu stroke mambo?
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama mkuu huyu kapata majibu nahisi atakua kachanganyikiwa kwa staili ya majibu
 
Back
Top Bottom