Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Huo ndio utaratibu tuliojijengea mkuu usiwe na shaka
 
Mkuu Makamee Ni ustaarabu tuu na kuonyesha kuheshimiana tuu maana hatujuani kwa namna yeyote ukiwa umri wala nyadhifa, nafasi zetu kijamii.
 
Last edited by a moderator:
unauliza jibu mkuu kiti maalumu!??

Mkuu Remote sijamuelewa kabisa mkuu huyu Blac kid, yani wadada wakuu ni wa vt maakumu nisaidie kuelewa nimeshapaniki mkuu maana sipendi hivi viti maalumu havina umaalumu wowote .naamimi katika usawa wa mwanamme na mwanamke ktk kila kitu.hv hakuna wanaume vt maalumu dunia nzima. Hv wale 201 bungeni sio vt maalumu? Nauliza tu mkuu
 
Last edited by a moderator:
Una maana gani mkuu?
Yani wadada wote humu jf ni wa vt maalumu?
Dadavua tafadhali mkuu

Hahahaha! Mkuu ladies first namanisha ivi mfano mama ndo anaweza akawa anatimiza mahtaji yote ya familia ila Ukuu akapewa baba! Labda nitengue kauli niseme ''Mkuu msaidizi''
 
Kuna wakati nilikuwa sijapata vizuri tafsiri ya mtu mzima na mtu mkubwa,kipindi hicho nikiona mtu mkubwa kimmri nilijua huenda ndiye mtu mzima na akikoleza tena na nywele nyeupe nilkaamini busara zii nae kumbe sikuwa najua vizuri.

Nimekuja kufahamu kuwa binadamu wote waliozaliwa bila mapungufu kibaiolojia ni watu wazima na kwamba suala la ukubwa na udogo ni la kimaumbile tu na kwamba time factor ndiye mpatanishi mkuu kwenye mlinganyo. Kwa maana hiyo nikajiaminisha kuwa busara na hekima mtu aanaweza kuwa nazo angali mtoto na swala la umri likafuata baadaye.

Profesa James Mdee ni baba mzazi wa Halima Mdee ( Mb), Leo Halima ni Mheshimiwa ila babaye mwanazuoni mbobezi siyo mheshimiwa unless otherwise aitwe tu just in case. Kina Mwigulu na watu wa aina yake leo ni waheshimiwa ilihali wanazuoni waliowafundisha kwenye sehemu anuai kielimu hawaja title hizo.

Kwa sababu hiyo basi tukubaliane kwamba hii Mheshimiwa/Mkuu ni tittle tu inayotumika kwa mfumo wa rejesta kwenye maeneo maalum ambayo yakitumika yanasound vyema. Na kwa kuwa tendo la bata kutokuwa na staha nzuri ya kwenda haja haibadilishi kua aina nyingine ya ndege basi hata wenye hulka sizizo na staha na tabia zisizo za kiungwana waendelee kuitwa tu wakuu ila wao ndio wajipime kutokana na tabia zao!
Kumbe mkuu tuko wengi tulioamini umri ni kigezo cha mtu kuwa na busara. Nami kwa kipindi kirefu niliamini hivyo lkn baadae nilibadili kwani niliwaona watu wazima wakifanya mambo ya ajabu ambayo hata macho hayakustaili kuyaona. Nilienda mbele zaidi ktk uchunguzi wangu binafsi na kuona kuwa kumbe umri si kigezo. Mtu aweza kuwa na umri mdogo lkn akawa na busara nyingi na mwenye kutegemewa ktk jamii inayomzunguka. Hivyo basi umri isiwe kigezo cha mtu kuwa mwenye hekima.
 
Hahahaha! Mkuu ladies first namanisha ivi mfano mama ndo anaweza akawa anatimiza mahtaji yote ya familia ila Ukuu akapewa baba! Labda nitengue kauli niseme ''Mkuu msaidizi''

Mkuu unatafuta ugomvi mkuu sisi si wakuu wasaidizi sisi ni wakuu kama nyinyi yani nimevimba kwa hasira mkuu. Hizi zako ni gender stereotypes mkuu
 
Wakuu nimepitia michango yenu yote kwa kweli mkuu mleta mada amewaelewa na si kwa faida ya mkuu mleta mada tuu bali hata wakuu wengine, mkuu mleta mada somo hili tumenufaika wengi mkuu, asante sana mkuu
 
Umenifurahisha sana mkuu upo sahihi asilimia mia kwa kuwa mungu ni mkuu na sisi tumeumbwa kwa mfano wake, wengine wanasema sisi ni watoto wake mtoto wa nyoka ni nyoka .yeye mkuu na sisi ni wakuu wadogowadogo. Kwa sisi wenyewe kwa wenyewe ni wakuu.kwa mantiki hiyo sisi wote ni wakuu
Mkuu stroke mambo?

salama tu mkuu-viti maalum, habari ya ujenzi wa Tanzania YETU??
 
Mkuu Remote sijamuelewa kabisa mkuu huyu Blac kid, yani wadada wakuu ni wa vt maakumu nisaidie kuelewa nimeshapaniki mkuu maana sipendi hivi viti maalumu havina umaalumu wowote .naamimi katika usawa wa mwanamme na mwanamke ktk kila kitu.hv hakuna wanaume vt maalumu dunia nzima. Hv wale 201 bungeni sio vt maalumu? Nauliza tu mkuu

hahaaa wanawake wengi viti maalum mkuu ila pia wapo wanaume wachache viti maalum mf MBATIA
 
Last edited by a moderator:
Kumbe mkuu tuko wengi tulioamini umri ni kigezo cha mtu kuwa na busara. Nami kwa kipindi kirefu niliamini hivyo lkn baadae nilibadili kwani niliwaona watu wazima wakifanya mambo ya ajabu ambayo hata macho hayakustaili kuyaona. Nilienda mbele zaidi ktk uchunguzi wangu binafsi na kuona kuwa kumbe umri si kigezo. Mtu aweza kuwa na umri mdogo lkn akawa na busara nyingi na mwenye kutegemewa ktk jamii inayomzunguka. Hivyo basi umri isiwe kigezo cha mtu kuwa mwenye hekima.

Ni mfumo wa makuzi tuliokulia ulisababisha tukaamini kwamba watu wakubwa hawafanyi makosa na kwamba wao ndio wenye busara sana na mambo yote awkwardly yanafanywa na rika dogo kiumri....

Kwanini hujawahi kujiuliza ni kwanini mambo mengi yanayochangia kumomonyoka kama siyo kupukutika kabisa kwa maadili kijamii yanachangiwa na rika hili kubwa ambalo zamani tulikaririsha kuwa halikosei? Ukirudi kwenye duru za kimentalist utaona pia katika makundi matatu ya kijamii ambayo hayawezi kusema uwongo mojawapo ni kundi la watoto wadogo (la pili ni la ulevi na tatu ni mtu mwenye hasira kwa kuwa staha imekwishawaondoka) kwa maana wanayonena ndiyo yameujaza moyo wao na ndiyo kweli!

Kama zipo kesi za ubakaji ambazo mbakaji ni mtoto nafikiri ni moja ama mbili kwa uwiano wa milioni nyingi kulinganisha na watu wakubwa. Pia uchunguzi mwingine niliofanya ambao si rasmi ni kwamba hata uwezo wa kujenga tafakuri na kuelewa mambo kwa mtoto mdogo ni mkubwa sana kulinganisha na watu wakubwa na kwenye hili ndipo wenzetu waliopata exposure wanapotuacha kwa kuwa wanagundua mapema creativity ya mtoto hivyo kama ni kumwendeleza anaendelezwa moja kwa moja kwenye area yake anayoonekana anaimudu badala ya kum diversify kwenye mlolongo wa mambo hatakuwa compitent badae!
 
Horse Shoe Arch,vizuri umefafanua kwa kina juu ya ukuu wa Jf.
Kwakua hata uchangiaji,busara,hekima na ukongwe wa kujiunga na Jf unaonaje kukawa clasfications za huu ukuu wetu.
Inakuaje mtu amejiunga jf miaka 7 nyuma aitwe mkuu na huyu alojiunga jana au leo nao waitwe wakuu?

Wewe unataka utengeneze matabaka???
 
Nashangazwa na matumizi ya neno MKUU humu Jf. Yaani kila mtu anamwita mwenzake mkuu hivi huu ni ukuu unatokana na kitu gani.

Mkuu, usipate homa. Ni neno la kawaida sana sawa na kusema "Hello" au "Ndugu" wakati ule wa Nyerere ambapo binadamu wote walikuwa ni ndugu au "Mheshimiwa" wakati huu wa pesa mbele. Nadhani umenielewa mkuu/mheshimiwa
 
Mkuu Makamee kuna ubaya gani? Ni heshima tu ukizingatia hapa kuna magreat thinkers ambao wengine kwao ni wakuu wa familia au katika maofisi. We acha tu tumejificha kwenye keyboard zetu lakini ungeruhusu satellite ichungulie kila mmoja utakuta unajibizana na baba au mama yako kama member humu!!!! Wanasiasa wamejaa humu na ID fake na za ukweli!!!Hi hi hi hi!!!! Wewe niite tu mkuu Zogwale.
 
Wewe unataka utengeneze matabaka???

Si kutengeneza matabaka kwani wakuu wote wana hadhi sawa?
Ktk forums zilizomo Jf kuna magwiji wa kila forum hatufanani uelewa na michango tuyotoa ktk uchangiaji wa threads kwa mfano,
Jf docto-Mzizi Mkavu
Jf photo- Utafiti,Moneystuna
Jf Siasa-Mzee Mwanakijiji

Kwahiyo ukuu wetu hauwezi ukawa sawa
 
Back
Top Bottom