Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Mkuu hapa katika hii jamii tunaeshimiana, hakuna dhaifu wala bwana mdogo, kama umejitambua ukajiunga hapa heshima yako mkuu.
 
Nashangazwa na matumizi ya neno MKUU humu Jf. Yaani kila mtu anamwita mwenzake mkuu hivi huu ni ukuu unatokana na kitu gani.

Mkuu
Kila mtu ni mkuu wa fikra zake mwenyewe.
Hivyo humu jf kila mtu ni mkuu. Umenipata mkuu.
 
Ni ishara ya kuitana kistaarabu kwani hatujuani kwa umri vyeo nyazfa n.k
 
Mimi naona kwa kawaida ktk mjumuiko wa watu mkuu (overall) hakosekani.Sasa humu naona watu wote ni wakuu ndo nashangaa ukuu wetu ni nini.

Ni matumizi tu ya maneno mkuu, kwani maana ya neno au kitu itatumika kwa kadri ya makubaliano ya watumiaji
 
Mkuu naona wachangiaji wengi wameendelea kukuita mkuu
 
Basi kama ni hivyo tulitendeeni haki hili jina mkuu,kimaneno na matendo yetu yawe ya kistaarabu sio Mtu anakuita Mkuu na mwisho anamalizia Mkuu wewe ni --------,Mkuu wewe ni PUNGA,Mkuu wewe ni Mburula.
Sasa heshima ya Ukuu iko waph?
 
Ni namna tu kuashiria heshima fulani. Utajisikiaje mtu akianza kukuita MKUU na mwingine akakuita WEWE? Chunguza hizi kauli mbili utaona kwanini MKUU inatumika sana.
 
Back
Top Bottom