Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

sina tatizo na hilo neno, kwanza mnaheshmiana na kutoweka matabaka


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mimi naona kwa kawaida ktk mjumuiko wa watu mkuu (overall) hakosekani.Sasa humu naona watu wote ni wakuu ndo nashangaa ukuu wetu ni nini.
 
Kwa kuwa Jamiiforums imesajiliwa kihalali na kwamba inatambulika kisheria, na kwa kuwa sheria zilizoisajili hii forum ni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa kuwa sheria husika ni ufafanuzi tu wa ibara zilizomo kwenye katiba ya J.M.T na kwa kuwa moja ya ibara hizo inatambua kwamba binadamu wote ni sawa kisheria na tunastahili kupata haki sawa sasa basi ni haki ya msingi kabisa kwa wana board kuitwa wakuu bila kuathiri vipengele vingine vya sheria.

Na kwa kutambua haki kuna hata wengine wanaitwa marais kutokana na kada wanazoziongoza kama Rais wa wasafi na rais wa Watanashati. Ni hayo tu mkuu, kama hukuridhika na tafsiri yangu unaruhusiwa kuweka pingamizi kisheria ambalo litataja wazi aina ya watu wanaostahili kuitwa 'Mkuu' na liseme bila kuacha shaka ni hatua gani anapaswa kuchukuliwa kinidhamu 'Mkuu' aliyefanya mambo yasioendana na hadhi ya ukuu wake. Natoa hoja!
 
Mimi naona kwa kawaida ktk mjumuiko wa watu mkuu (overall) hakosekani.Sasa humu naona watu wote ni wakuu ndo nashangaa ukuu wetu ni nini.

mbona kitu cha kawaida sana mkuu! Ni kuonyesha heshima hata kama mtu humjui.
 
mkuu makamee mbona hii ni kawaida hata nyumbani zenji wao hutumia YAKHEE badala ya mkuu..
 
Horse Shoe Arch,vizuri umefafanua kwa kina juu ya ukuu wa Jf.
Kwakua hata uchangiaji,busara,hekima na ukongwe wa kujiunga na Jf unaonaje kukawa clasfications za huu ukuu wetu.
Inakuaje mtu amejiunga jf miaka 7 nyuma aitwe mkuu na huyu alojiunga jana au leo nao waitwe wakuu?
 
Back
Top Bottom