Kwa kuwa Jamiiforums imesajiliwa kihalali na kwamba inatambulika kisheria, na kwa kuwa sheria zilizoisajili hii forum ni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa kuwa sheria husika ni ufafanuzi tu wa ibara zilizomo kwenye katiba ya J.M.T na kwa kuwa moja ya ibara hizo inatambua kwamba binadamu wote ni sawa kisheria na tunastahili kupata haki sawa sasa basi ni haki ya msingi kabisa kwa wana board kuitwa wakuu bila kuathiri vipengele vingine vya sheria.
Na kwa kutambua haki kuna hata wengine wanaitwa marais kutokana na kada wanazoziongoza kama Rais wa wasafi na rais wa Watanashati. Ni hayo tu mkuu, kama hukuridhika na tafsiri yangu unaruhusiwa kuweka pingamizi kisheria ambalo litataja wazi aina ya watu wanaostahili kuitwa 'Mkuu' na liseme bila kuacha shaka ni hatua gani anapaswa kuchukuliwa kinidhamu 'Mkuu' aliyefanya mambo yasioendana na hadhi ya ukuu wake. Natoa hoja!