Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Kuna mahali nimeingilia maisha ya watu au nimeingilia maisha yako?
Ndugu mdau?
Jisome tena hapa,


''Kuna dada ana miaka 27 ana watoto 6 mpaka sasa

Nikamshauri kuhusu uzazi wa mpango
Alikuepo mtu mwingine pembeni akasema mwache azae kizazi anacho watoto watakuja kumsaidia baadae heh nilipigwa butwaa"

Ukisoma jibu ulilopewa kwa ushauri wako ulioutoa ndio utanielewa.
 
Asante kwa maoni karibu tena
 
Kilimanjaro sio kweli, katika jamii hawazaliani kwa sasa ni Kilimanjaro, shule nzima ya msingi kukuta ina watoto 50 tu ni kawaida
 
Yaan anazaa watoto wa kumtumikia hivi huu nao si ni utumwa?
 
Hii slogan ya zaeni muongezeke mkaijaze dunia....na ya kwamba zaa watoto watakusaidia baadae...KWA NDUGU ZANGU WAZARAMO HII HAIPO!

Unakuta Mu-MAMA WA MIAKA 45-50 NA LIBABA LA MIAKA HIYO HIYO BADO YAKO NYUMBANI KWAO! YANATEGEMEA BABA NA MAMA WACHUKUE KODI YA VYUMBA YAPIKIWE UGALI WA MAMA NA BABA YAO! YALE YALALE...!

Hakuna yanachowaza zaidi ya kula na kulala! Ama mama na baba yao wafe yagawane vyumba!
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Hoja ni kwamba usichanganye wajibu na deni. Ulimsomesha na kumlea kwa sababu huo ulikuwa wajibu wako ulipoamua kumzaa.

Vipi kama mtoto hana kazi, ana familia yake na anahangaika kujikimu, bado utasema hana shukrani kwa sababu hawezi kukupa kile unachotaka?

Msaada unatakiwa uzingatie uwezo wa mtoto, siyo matarajio ya mzazi.
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Kwani alikuaomba umzae ?
Wewe umetimiza wajibu wako maana wewe ndio ulimleta duniani

Issue ya kukusaidia akizeeka ni hiari isiwe shinikizo
 
Kwa nini utumie neno kurudisha fadhila wakati mzazi alifanya wajibu wake?

Ina maana haki ya mtoto kupata malezi na elimu ni fadhila au ni jukumu la mzazi?

kama mtoto ana kipato kidogo, ana familia yake na majukumu mengine, akishindwa kukusaidia kwa kiwango unachotaka, kwanini useme hana shukrani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…