Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Hii mada imechanganya vitu vingi sana! Imechanganya umasikini wa wazazi, utajiri wa wazazi, wajibu wa watoto kusaidia wazazi, watoto kutelekezwa, kuzaa watoto wengi, kutowajibika kwa mzazi. Kila kitu kimo kwenye hii mada. 😊
Kila mtu anachangia kulingana na experience yake hapa. Mwingine hakupata malezi sahihi kwa wazazi wake. Mwingine wazazi wake walimtelekeza. Hisia zote zipo kwenye hii mada. 😊

Ishu ya kusaidia wazazi ni suala binafsi la mtu husika. Kuna mwingine wazazi wake wamempa life na wamemrithisha mali. Bond yake yeye na wazazi wake ni ya kudumu/lifetime bond.
 
Goja siku ukizeeka akutelekeze ndiyo utajua ni nzuri au ni mbaya
Tunaishi kwenye ulimwengu wa economic uncertainty, mtoto anaweza kutamani kukusaidia lakini akashindwa kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Ukimfundisha mtoto kuwa 'kama hujanisaidia basi umeniacha,' hapo unamfanya ajione ni mtu wa kushindwa kila siku pale anaposhindwa kukupa pesa, hii inaharibu mental health ya mtoto.
 
Kwa hiari sio kwa shinikizo
Na ushukuru utakachopewa
Sio tena unakua hu riziki
Nje ya mada; Sema mada yako umechanganya vitu vingi sana, mara masikini, tajiri. Mtoto anatakiwa amsaidie mzazi bila kujali ni masikini au tajiri. 😊
Kuandika kazi Tosheka hivyo hivyo 😊
 
Kupitia huu uzi najifundisha kuona watu wanatokea kwenye familia za aina gani?
Utamtambua mtu kwa emotion yake tu kwenye uchangiaji wake,wengine wanajibu kwa hasira kama zote dhidi ya wazazi wao!
 
Tembea ujionee.
Ukiwa umejifungia kwemu Mkamba Kizapala wilayani Mkuranga na wazazi wako wenye watoto sita unaweza kudhani watu wa Pwani ndiyo wanaozaa sana miongoni mwa makabila ya Tanzania.
Nimeongelea pwani kwa sababu ndio napajua huko kwingine sema wewe hukatazwi
Vyovyote vile iwe pwani iwe kusini kuzaa kama mtaji sio jambo zuri
 
πŸ“Œ
 
Kabisa Mkuu mzazi anakua na matarajio makubwa yasipotimia anaanza kunungunika
 
Ukiona haieleweki kaa tu kando hakuna tabu wataoelewa watachangia kwa kadri watakavyoelewa
 
Tajiri anatumia muda mwingi kutafuta hela ambapo mke na watoto ni kipaumbele cha pili, huku masikini kila wakati anawaza sex tu suala la pesa ni kipaumbele cha pili. Hivyo basi, mtafuta pesa ataongezewa pesa atapunguziwa watoto huku mtafuta watoto ataongezewa watoto atapunguziwa au kunyimwa kabisa pesa. Na mkumbuke mshika mawili.......
 
Kupitia huu uzi najifundisha kuona watu wanatokea kwenye familia za aina gani?
Utamtambua mtu kwa emotion yake tu kwenye uchangiaji wake,wengine wanajibu kwa hasira kama zote dhidi ya wazazi wao!
Endelea kufanya uchambuzi kuhusu wanaochangia huku umetoka kukataza kufatilia maisha ya watu ila JF πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Ni sawa kabisa kusoma na kuja kuwasaidia wazazi wako. Na si wazazi wako tu bali kumsaidia mtu yeyote anayehitaji msaada kwako. Kuwasaidia wazazi ni sawa na kufanya hisani ya kusaidia watoto yatima na wasiojiweza. Charity start at home.
Charity kwa tafsiri yake ni hiari, suala la kuwasadia wazazi hatukatai ni jambo jema sana likifanywa kwa hiari.

Swali ni kwa nini mtoto aitwe hana shukrani au aanze kulaumiwa asipoweza kutoa msaada? Charity huwa hailazimishwi, huwa inatolewa kwa hiari na kulingana na uwezo wa muhusika.
 
Endelea kufanya uchambuzi kuhusu wanaochangia huku umetoka kukataza kufatilia maisha ya watu ila JF πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
Jaribu kua muelewa,nimesema Najifundisha, kuna njia nyingi za kujifundisha jambo ikiwemo kupitia watu wengine,kuna tofauti kubwa kati ya Kujifundisha na Kushauri au kuingilia privacy ya mtu,

Mimi sijamfuata mtu na kumwambia ''Usifanye hivi bali fanya vile'' ''Una watotot 6 usizae watoto wengi''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…