Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Kwani umeambiwa usisaidie wazazi
Jaribu kusoma mada basi na kuelewa wooii🙌 asante kwa maoni
 
Tutunge Sheria iwe ni lazima kusaidia wazazi kama ilivyo fanya china.

Ukishindwa kumsaidia mzazi wako ni faini halafu uanze kumsaidia, ukishindwa jela Hadi miaka 10 na ukitoka lazima uanze kusaidia.

Maana hata yeye alipanga kuzaa ila hakupanga utokee wewe.

Sioni mantiki ya kula vyuku na kumtelekeza mazima mzazi wako.

Tujifunze na kujiepusha laana ndogo ndogo
 
Hakuna sehemu tumesema mzazi asisaidiwe mzazi kusaidiwa ni hiari ya mtoto maana mtoto hakumuomba mzazi amzae

Issue ni kwamba baadhi ya wazazi wanazaa watoto kama mradi wa baadae

Mzazi anazaa watoto wengi huku anafahamu kabisa hana uwezo wa kuwapatia mahitaji ya msingi ila kwa target kwamba waje wamsaidie badae

Wewe unaona ni sahihi kweli?
 
Kabisa na kuwa na watoto wenye kusaidia wazazi wao uzeeni ni moja ya malengo mahausi kabisa ya kuzaa.
 
Kama ukitaka uhakika wa kusaidia kwa kuwalelea watoto ,nenda ukaasili watoto yatima, hao sure 90% watakusaidia ila wa kuzaa mwenyewe ni mtihani.
 
Msaada ni hiari
Watoto yatima wana asilimia kubwa ya kuja kukusaidia , nina mifano zaidi ya saba , tna mmoja ni shekhe wetu ..Mtoto yatima aliyemlelea ndiye kafuata nyadhifa yake , anamsaidia ila wake wamebaki kuwa wahuni tu .
 


Hiyo ilikuwa zamani.

Siku hizi ukizaa watoto usioweza kuwaandaa jua umezaa watumwq na vibarua wa watu wengine
 
Watoto yatima wana asilimia kubwa ya kuja kukusaidia , nina mifano zaidi ya saba , tna mmoja ni shekhe wetu ..Mtoto yatima aliyemlelea ndiye kafuata nyadhifa yake , anamsaidia ila wake wamebaki kuwa wahuni tu .
Unazaa watoto ili waje kukusaidia baadae au?
 
Hili ni swala na mtazamo, imani na kihistoria.
Zamani wazazi walizaa watoto bila kikomo, ilikua tani ya mzazi kuzaa wlidadi awezayo, sababu ya maingi ilikua watoto walikua wazalishaji. Zamani kwetu usukumani, kaya yenye watoto wengi ilikua na uwezo mzuri wa uzalishaji na uchimi imara. Zamani mtoto wa miaka 6-7 tayari ananza kujifunza namna ya kuwa mzalisha, ataenda kuchunga, atakamua, ataenda shamba, kwa ufupi watoto walikua mali haswa kwa mzazi, watoto walikua wazalishaji wazuri kupitia shughuli za wazazi wao.

Baada ya miaka kusonga, ikaingia elimu, wazazi wakapeleka watoto wao shule. Kuanzia hapo taratibu watoto wakaanza kujitoa kwenye sehemu ya uzalishaji wa familia na kuanza kuwa watumiaji tu wa mali ya familia. Baada ya hicho kizazi kumaliza shule kilipata kazi rasmi (wengi wao).

Sasa hawa wazazi ambao walipelekwa shule miaka hio walipokuja kupata familia, wengi wao maisha yao yalikua mijini, hakuna shamba, hakuna mifugo, ninkazi rasmi na mshahara. Watoto wao hawakuwa wazalishaji tena, na likaingia winbi la kusomesha watoto kwenye shule za kulipia. Ukiunganisha logic ya kwamba watoto wao hawazalishi+gharama ya elimu, wazazi hawa wakawa wanazaa watoto wachache wanaoweza kuwaandaalia masha vizuri.

Sasa dunia ya leo tupo matabaka mawili, wapo waliosoma, wanaoishi mijini ambapo mtoto zaidi ya kumtuma dukani hana kingine cha kuzalisha, hao wanazaa lwa malengo na kuwaandaa watoto wao wapate elimu wakiamini watapata kazi nzuri huko mbele. Kundi la pili ni lile ambalo halikupata fulsa ya kwenda shule, hawa wanaishi maisha ya kawaida ya chini ua mtanzania, hawa bado wanaamini katika watoto. Wengi wao hawajapata maisha mzuri hivyo wanayo imani kuwa katika watoto wengi atatokea mmoja wa kuinua familia.

Mtazamo wangu wote wawili wapo sawa. Kundi la kwanza linatumia elimu na maarifa waliyonayo juu ya maisha ya sasa na kujaribu kuandaa vizazi vyao. Kindi la pili linatumia imani, na historia kuamini kuwa mmoja kati ya watoto atakua mkombozi.

Kila mtu afanye inavyompendeza
 
Sawa asante kwa maoni
Karibu tena mkuu🙏🙏
 
Ukiangalia kwa jicho pevu ata wewe baba yako angewaza hivi usingezaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…