Hivi Rais Samia amewahi kuandika Makala au Paper ya utatuzi wa changamoto za jamii?

Alipaswa kujua watanzania ni wavivu kabla ya kutaifisha mashirika na viwanda binafsi na kuvifanya vya serikali, matokeo yake vikawa, vinajiendesha kwa hasara hadi kujifia

Serikali kutoa vitu bure sio ujanja, serikali sio baba au mama yako, serikali inatakiwa kuweka miundombinu sahihi na sera sahihi kwa ajili ya wananchi kuzalisha na kipato na kujilipia huduma wenyewe, nchi zilizoendelea ndio zilifanya hivyo, ujamaa ni kulea uvivu
Kipindi cha Nyerere ndio kipindi wananchi waliishi maisha magumu kuliko vipindi vyote, kwa mgao wa bidhaa, udikteta, njaa
 
Nakubaliana na ujumbe wako kuanzia hapo kwenye 'vinginevyo' upo sahihi kabisa.

Hapo kwenye sentensi ya kwanza, Mungu naomba anipe uwezo wa kunyamaza, kuna vitu vinauma sana!
 
Nakubaliana na ujumbe wako kuanzia hapo kwenye 'vinginevyo' upo sahihi kabisa.

Hapo kwenye sentensi ya kwanza, Mungu naomba anipe uwezo wa kunyamaza, kuna vitu vinauma sana!
Huo ndio ukweli mchungu
 
😅😅😅Tuache sie na mwanamke Rais wetu

Kazi iendeleee...
 
Kaka huo ubongo Hana. Ni mwepesi kichwani. Watanzania mkataeni kwa nguvu zote 2025 kama atajileta kwa faida ya kesho ya taifa letu.
 
Mimi bado nitaendelea kusimamia hoja zangu. Nakubali ni kweli alifanya makosa ila ni makosa yaliyotokana na mtu kufanya mambo kwa nia njema kabisa. Baada yake, marais wote waliofuatia wamekuwa wanafanya mambo kibinafsi zaidi. BTW kuna nchi gani Afrika, kusini ya jangwa la Sahara ambayo rais wake anaweza kupigiwa mfano kuwa alifanya vizuri kuliko Tanzania? Labda Botswana kwa mbali. Baada ya kubahatika kutoka na ku-experince nchi za Scandinavia nitaendelea kusema kosa kubwa la mwalim ni kuwaamini watanzania. Hizo nchi nimekuta mashirika na kampuni nyingi tu zinaendeshwa na serikali na zinafanya vizuri. Tofauti ni kwamba wananchi wa kule ni wachapakazi wa waaminifu sana.
 

..tafuta vitabu vya Edwin Mtei, na Andy Chande.

..naamini ukichanganya na uzoefu wako utapata full picture ya nini kiliangusha uchumi wetu.
 
Aliandika kwa mkono wake mwenyewe makala ya miaka 30 ya vyama vingi vya Siasa na mtazamo wake juu ya mustakabali wa siasa za vyama vingi nchini Tanzania na lilikuwa andiko lililoshiba haswa.

Natumai siku za usoni ataandika makala nyingine
 
Magu na jakaya waiandika nyingi sana wakifuatiwa na Mwinyi
 
Rais Samia alivyokuwa anaanza urais alikuwa idealist fulani hivi, maridhiano, demokrasia, 4R , Rule of law n.k
Baadae akaja kuona upuuzi wa siasa za Afrika, akaamua kuwa pragmatic kama Magufuli
True, na sisi pia tulimpoozea sasa ni spana za kimtindo!.
P
Siyo kwamba alipoanza tu kulewa madaraka (yaani pale tu madaraka yalipo mnogea/alipoanza tu kutukuzwa kupitiliza, na kuanza kuchukuliwa na wasaidizi wake kama mungu mtu) ndipo mambo sasa yaliponza kubadilika!!
 
Karatasi pekee anayo itumia mara kwa mara ni toilet paper [emoji3474][emoji3474][emoji3474] tu
 
Makala au pepa ndio inatatua Changamoto zako au za jamii?

Pili Kauli yake ,miongozo,maagizo ni makala tosha.

Kwa mfano Wizara ya Elimu ilikuwa na proposal ya mradi wa HEET(Mageuzi ya Elimu ya Juu) na ililenga kuongeza uwezo wa Miundombinu,utafiti,kuongeza wakufunzi nk kwenye existing universities and other higher Learning institutions.(Mkopo kutoka WB).

Samia akasema Kaeni Upya na WB Ili kwamba badala ya kurundikaaendeleo maeneo hayo hayo Kila siku tusambaze Nchi nzima ndipo Sasa WB wakakubari na Sasa Vinajengwa vyuo Vikuu na Matawi ya Vyuo Vikuu kwenye Mikoa yote ambayo haikuwa na vyuo.

Huu ni mfano mmja kati ya mambo mengi ambayo Rais ameweka interventions na yametatua Changamoto.

Umeelewa wewe nyumbu wa Chadema?
 
Paper ya nini wewe mapepa yamejaa kibao mtaani yanafungia chapati? Matatizo ya nchi hii yanafahamika na utatuzi unajulikana hakuna haja ya pepa.
 
Namna tu anavopitia mikataba kabla ya kui sign ni sawa na feitoto alivokuwa anafanya kwenye mikataba na Yanga halafu utegemee mtu wa namna hiyo aandike paper tena ya utatuzi wa changamoto, sidhani
Nanga mkono hoja yako ila raisi ni taasisi achana na mbwembwe za yule mwalimu kukariri notice
 
Magu na jakaya waiandika nyingi sana wakifuatiwa na Mwinyi

..kama Magufuli aliandika itakuwa ni ktk majarida ya wakemia wenzake.

..Magufuli hakuwahi kuandika makala yoyote akiwa kiongozi na mwanasiasa ktk masuala ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

..Hata hotuba alizokuwa akitoa hazikuwa zikiwekwa ktk tovuti ya Ikulu kama alivyofanya Mkapa na Kikwete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…