Hivi shule kama hii ina walimu kabisa watakaoweza kuidai Serikali iwaongezee mshahara bila aibu?

Unaweza kukuta hizo IV ni baada ya ku standardise zaidi ya mara mbili kama yale ya Big Resilts Now
 
Kwa idadi hii ya wanafunzi na mahali shule ilipo sitegemei kuona wakifanya maajabu.

Na wasiwasi huenda jumla ya wanafunzi kidato cha 1 hadi 4 ikawa >3,500

Idadi ya waalimu ikawa <35 na 5 wakawa na nafasi za uongozi bila kuhusika na ufundishaji.

Ifike mahali wizara husika ichapishe idadi ya waalimu na wanafunzi kila shule kila mwaka ili tuweze kudadavua na kujua tatizo lipo kwa wanafunzi pekee au uhaba wa waalimu pia ni chanzo.
 
Wanafunzi wa siku hizi ni wapumbavu. Hawafundishiki sababu wazazi hawawalei ipaswavyo.

Tutegemee bomu la makahaba, vibaka, majambazi maana hata serikali ikiwafaulisha bado watafeli tu
Hii ni hatari kubwa... Wanafunzi 500, hakuna division I.. hapana ..hapa na walimu hamuna..

Kuna shida kubwa kwenye elimu yetu..
 
Kama matokeo ndio hayo, kwa maoni yangu hawastahili kulilia nyongeza ya mshahara. Nyongeza ya mshahara tafsiri yake ni motisha; sasa utampa motisha mtu asiyefanya kazi aliyoajiriwa?
 
Kama matokeo ndio hayo, kwa maoni yangu hawastahili kulilia nyongeza ya mshahara. Nyongeza ya mshahara tafsiri yake ni motisha; sasa utampa motisha mtu asiyefanya kazi aliyoajiriwa?
Wa shule hiyoo..
 
Kwa taarifa yako mwanafunzi anayejielewa, hawezi kumtegemea mwalimu kwa 100% ili afaulu! Isipokuwa 25% tu.


Umeshajiuliza ni kwa nini kuna wanafunzi wawili waliopata ufaulu wa division two!! Wazazi wa hao wanafunzi wana mchango gani kwenye malezi ya watoto wao?
Mzazi unatoka nyumbani saa 11 alfajiri, halafu unarudi saa 5 usiku! Unategemea nani atakulelea mtoto wako mtukutu? Mwalimu ambaye aliongezewa mshahara wa kueleweka enzi Rais ni JK! Hilo haliwezekani. Na walimu nao ni binadamu. Hivyo wana njia nyingi za kufikisha ujumbe kwa wahusika.


Serikali nayo kujaza darasa la wanafunzi 500 kwenye shule moja nayo ni akili, au ni matope? Na hapo unaweza kukuta hiyo shule hata uzio haina!! Bado unategemea maajabu!! Mbona watoto wanaosoma shule za boarding, wengi wanafanya vizuri?
 
Mkuu ukiangalia tu idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani huu, utagundua shule ina mrundikano mkubwa wa wanafunzi. Ikiwa serikali inaruhusu darasa moja liwe na wanafunzi 150 unadhani mwalimu anawezaje kumudu kufundisha na kutoa mazoezi kwa darasa kubwa kama hilo? Lawama zote ni kwa serikali sikivu ya CCM.
 
Mbona wana matokeo mazuri sana, au wewe ulitaka yaweje ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…