Hivi shule kama hii ina walimu kabisa watakaoweza kuidai Serikali iwaongezee mshahara bila aibu?

Mkuu , tatizo sio waalimu tu ni ngono watoto wanafanya Sana ngono Hadi wanapoteza focus then wa kiume wana Bet Sana na bangi nyingi na ushoga.


Hapo in short hamna shule
Hilo nalo neno. Wahusika walitazame kwa jicho la kipekee. Usipoziba ufa -Utajenga ukuta.
 
Mmm! Siafiki hoja yako. Mwalimu anazo mbinu nyingi za kuwafikishia wanafunzi wake ujumbe/maarifa kile anachokusudia wakipate. Siku hizi Library zipo nyingi mpaka kwenye Internet. Vikundi vya kujifunza na kujadiliana (Kwa nia njema) vinawezekana. Yapo madarasa rasmi ya masomo ya ziada. Wanafunzi wakihamasishwa vizuri watayapenda masomo yao, na mwanafunzi akilipenda somo atalielewa zaidi.
Kama wazazi watashikamana na waalimu, matokeo mabovu ya 2022 yatakuwa ndo ya mwisho. Huko mbele matokeo yatafurahisha zaidi. (Nimesema hivyo kutokana na uzoefu wangu kama mjumbe wa Bodi huku kwetu).
NB:Tusisingizie mazingira kwani hata huko walikofanya vizuri mazingira yapo na labda ni magumu zaidi.
Mwalimu au mtu wa kumfundisha mwanafunzi wa Sekondari sio lazima awe yule aliyetoka chuo cha ualimu. Baba nyumbani, mama, kaka,dada aliyepita Sekondari anaweza kutoa msaada 1,2,3...na sio lazima kwa masomo yote. Wanafunzi/Mtoto ahamasishwe kuuliza maswali ya kile alichojifunza shuleni na hakukielewa. Sio ahamasishwe (kwa kupewa ruksa) kuangalia TV au Simu janja au kufuatilia Mpira na mambo kama hayo.
 
Kwa hiyo internet anawafikishia kupitia simu yake au? Kwa watoto hao 500? Ukijumlisha wazazi ambao siku hizi hawana hata muda na watoto wamewaacha dada wa kazi na walimu na wakishindwa kabisa wanawapeleka boarding. And by the way, asilimia kubwa ya watoto wanaosoma shule hizo wazazi wao wa kipato cha chini na wazazi wengi wa hivyo wanapambana na maisha hata huo muda wa kufuatilia watoto hawana. Mzazi yeyote mwenye kujiweza angalau kidogo ni ngumu kumwacha mtoto asome darasa lenye watoto zaidi ya 200.
Walimu hawawezi kutenda miujiza, wanahitaji miundombinu pia. Hayo mengine sijuo ya internet sijui nini wanheyafanya kama hata mishahara wanayolipwa ingekuwa inaeleweka.
 
Mkuu; nimesema mwalimu sio lazima awe yule mtu aliyepitia chuo. e.g. Hiyo simu mtoto (mwanafunzi wa sekondari) anayotumia kuangalia porn si aitumie kusearch somo lolote analolitaka?mbona hayo masomo na mifano (+ video)hutolewa kwenye Internet? Mzazi mwenye dada wa kazi ni mzazi mwenye uwezo.
Watoto tunaozungumzia hapa ni watoto wanaosoma Sekondari (F2 na kuendelea+). Kama mzazi anadiriki kumwekea mtoto wa sekondari dada wakazi, hiyo sasa ni too much.
Sidhani ni kweli kwamba wazazi wa siku hizi kama ulivyosema "wazazi ambao siku hizi hawana hata muda na watoto wamewaacha dada wa kazi na walimu...." kwa sababu mbona mtoto e.g. wa Ke akipata mimba mzazi anakomaa na mhusika? Huo muda huwa anaupata wapi kipindi hicho?
Ukizingatia kwamba kazi ya Ualimu inasemwa tangu zamani ni kazi ya Wito. Mwalimu ni kweli anastahili mshahara wake na mshahara wa mwalimu umebainishwa katika nyaraka na miongozo ya Serikali. Kama mtu alikubali kazi hiyo manake alijua kabisa yatakayofuata na atalipwa lini na kiasi gani. Mbona baada ya ajira anageuka na kuwa tena mbabaishaji? Huyo ni mwalimu wa Mshahara na sio mwalimu kama Wito.
Mwalimu mmoja(1)akijizatiti anaweza kufundisha hata wanafunzi elfu moja(1,000). Mbona zamani kulipokuwa hakuna compyuta, hakuna simu janja iliwezekana? Chuoni baadhi ya wanafunzi hodari hurekodi lecture halafu baadaye anakuja kuisikiliza tena akiwa ametulia. Tuseme tu Ukweli ni kwamba wengi Tunakwepa wajibu wetu kwa visingizio vya hapa na pale na kutoa lawama. Lakini ukitulia utaona kwamba hakuna kisichowezekana.
Mwalimu yupo Dar, Nairobi au mbali lakini mwanafunzi yupo huku umasaini ndani-ndani huku na darasa linaendelea.
 
Swala la kufaulu mwanafunzi linabebwa na wadau wanne kwanza mwalimu anajukumu la kumpa maarifa ,ujuzi na kumlea mwanafunzi anapokua kwenye mazingira ya shule pili mzazi anajukumu la kumlea na kufuatailia mienendo na tabia za mwanafunzi huyu za kila siku awapo nyumbani tatu mwanafunzi mwenyewe anawajibu wa kufocus ,awe na malengo na uchu wa kufanikiwa katika elimu(commitmentl) nne serikali anawajibu wa kuandaa sera nzuri za elimu Kwaio ndugu mtoa maada wanafunzi wakifeli hatuilaumu serikali,walimu au wanafunzi tunapaswa kufanya utafiti ili tugundue kati ya hao wadau hapo juu nani hajatimizia wajibu wake ipasavyo
 
Wanafunzi mia tano darasa Moja walikua wengi sana yaani ni idadi ya shule nyingine kabisa. Kwahiyo hapo waligawanywa katika mikondo 6 au Saba. Kutokana na idadi ya walimu waliopo Kama ni wachache kufelisha ni jambo la kawaida.
Endeleeni kubet na viwango ili tuonekane tunatekeleza ilani .Sijawahi

kuona chujio linaongezwa matundu. Graduate wa Leo Ana ufahamu mdogo kuliko STD seven wa 1980.
 
Hii ni Shule iko jioni Dar Es Salaam. Kwa kweli ni aibu tupu! Ina maana waalimu na hao wanafunzi wenyewe Kuna jambo wanafanya sio bure!! Haiwezekani walioko mkoani awafanyie vyema. Huu ni uchumi.
Mkuu wa mkoa na Elimu fanyeni tathmini hapa.!!
 
Kweli kabisa mkuu. Na akibainika ni nani kazembea, basi awajibike.
 
Inasikitisha sana
 
Hyo shule kuanziq benchi la ufundi that means Walimu na wanafunzi wao wana Bet na kucheza upatu... No seriousness at all
We unawajua kweli[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]hyo shule nuksi bin balaaa hamna kitu hapo
 
Aiseee ..hapa hamna shule..View attachment 2474026
Broo nilikua na darasa la watoto 700 ukitoka class kichwa kimestuck jus imagine nilikua nafundisha maths
Nilichokua nafanya class A ndo watoto wanajua hesabu ndo nakomaa nao hao hao kungine Bora liende tu....mara mkondo mpk G,Yaani km mimba changa inatoka Kwa kusimama
Yaani hizi shule za kata watoto ni wengi mnooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…