Hivi south Africa mbona kunatisha Kuna dogo wa mtaani kapigwa risasi Leo huko aisee ni huzuni

Hivi south Africa mbona kunatisha Kuna dogo wa mtaani kapigwa risasi Leo huko aisee ni huzuni

Wabongo wajuaji na story nyingi ni za kuambiwa
Mimi siku tatu zilizopita nilikua Arusha hapo pana matukio ya kuawa watu mmoja sinoni mwingine matejoo hata JF haijaletwa hii tumeizungumzia ile ya rasta alieuawa Sinoni ila wakisikia SA marehemu atapewa kesi zote za ujambazi kweli wahuni sio watu ndio maana nabaki kuwasoma tu kwa kuwa nipo hapa ntafatilia na marehemu tutamchangia kumsafirisha kuja kuzikwa Tanzania.
 
Kuna dogo wa mtaani hapa alienda south Africa kutafuta maisha mwezi wa 1 mwaka huu Kwa jinsi navyomjua dogo hakusoma na Wala Hana kipaji ila ni msela tu mtaani alikua na miaka 27 kapigwa risasi jioni ya Leo tumepata taarifa sijui tatizo ni Nini huko south Africa maana matukio yamezidi sana aisee mlioko huko au mliowaho kufika inakuaje mauaji yanakua mengi sana
Huko south ukikopa ukasema nakulipa jumamosi alafu ukapitiliza hadi jumapili basi unapigwa gun kwisha habari yk..
 
Hivi hii imeka1je Kwa mliowahi kufika south Africa
Unataka kujua kuhusu mdogo wako wa mtaani, ama unataka kujua Nini hasa....!?

Nenda straight kwenye point, Mimi nitakujibu hapa, nimeishi Gauteng, Western Cape na Free state, hizo ni Provinces.
 
Kuna dogo wa mtaani hapa alienda south Africa kutafuta maisha mwezi wa 1 mwaka huu Kwa jinsi navyomjua dogo hakusoma na Wala Hana kipaji ila ni msela tu mtaani alikua na miaka 27 kapigwa risasi jioni ya Leo tumepata taarifa sijui tatizo ni Nini huko south Africa maana matukio yamezidi sana aisee mlioko huko au mliowaho kufika inakuaje mauaji yanakua mengi sana
Mungu dereva
 
South afrika Kwa utekaji ni sawa tu na Tanzania wanavyotekwa Kila siku wakosoaji wa serikali
 
Madogo wasela huko SA wanaenda kwa mkumbo na sio plan za maisha wanaitana huko wanapokeana kwenye ma gang vikundi vya kihalifu wizi uporaji makundi huko yana upinzani hata watz kwa watz huko wanachomeana na kuuwana.

Wengi tunaamini sauz maisha simple ila sio kweli masela wapo kule zaidi ya miaka 10 ukienda kwake utakuta anaishi geto moja na masela zaidi ya 7 ndani ya room moja

wachache sana ukute wamepaga kivyake anaishi pekeake au na mwanamke wake geto moja unakuta kuna watanzania wazambia humo humo wazimbabwe warundi humo humo utasema hayo ndio maisha mazuri?

Wanaogopa kurudi bongo sababu bado hawajatoboa wanaona aibu wanaona bora wakaze ila ndio ivyo wanaishia kutaabika kaburu hakuna maisha mazuri bila juhudi elimu na fani.

Vijana wa ma gang waporaji wavuta bangi madawa kule life yao ni mbaya mno bora hawa waokota makopo wa tz.

Madawa ya kulevya kula ukichukua mzigo ukijaribu kufanya utapeli kule kuna madon wa makundi kuna madon ambao ni wasauz watz warundi wazambia wazimbabwe na mataifa mengine so usnichi kule ni mwingi ukiishi kule ni kama upo vitani rafiki yako leo anakuibia mzigo anatokomea anakuachia msala ww.

Wanaoishi kule kisela asilimia kubwa wamepinda mwanao unaeishi nae anaweza kukugeuka mda wowote kuibiana wenyewe ni kawaida hii inatokana na mtu unaenda kule kwa matarajio makubwa na huna elimu huna fani unaishia kwenye magenge ya kihalifu.

Visa vingi vya kule ni madawa upinzani wa makundi kwenye biashara hii pia mademu kuchukuliana mademu kule ukiwa smart pia ni mbaya ukipenda dem kule dem wa msela nayo inaweza kukumaliza ukiwa ndani ya cirle ile ile ya aina ya maisha.

Sauz au Kaburu kwa wanavyoita wao ukitaka kuishi kwa amani nenda ishi kwa amani nenda ukiwa na fani elimu pia wapo watu wanaishi vizuri kwa elimu au fani nzuri

Fundi magari fundi umeme n badhi ya fani za kawaida kule ajira utapata vizuri tuu muhimu uwe na makaratasi yako yanasomeka vzr kabisa.

hawapo kwenye magenge wala makundi ukiishi kule sana sana ni salama zaidi ukiwa mbali na aina ya marafiki ambao ndio wako kwenye haya mgenge bora uwe lonely kuliko kuwa na rafiki mtanzania ambae heleweki mishe zake ni hatari.

Johanesburg pertoria cape town na durban ndio miji hatari zaidi.
 
RSA sio sehemu ya kuishi hasa kama ni mtu mweusi ,huko kuna ubaguzi na chuki za kila siku,kula chuma ni kitu cha kawaida huko
 
Huko mbona kawaida
Watu kuuwana

Ova
 
Kuna dogo wa mtaani hapa alienda south Africa kutafuta maisha mwezi wa 1 mwaka huu Kwa jinsi navyomjua dogo hakusoma na Wala Hana kipaji ila ni msela tu mtaani alikua na miaka 27 kapigwa risasi jioni ya Leo tumepata taarifa sijui tatizo ni Nini huko south Africa maana matukio yamezidi sana aisee mlioko huko au mliowaho kufika inakuaje mauaji yanakua mengi sana
Huyo alikuwa mhalifu.
 
Wizi Uuzaji madawa Utapeli na kujifanya wanaishi maisha ya ugangstar
 
Unataka kujua kuhusu mdogo wako wa mtaani, ama unataka kujua Nini hasa....!?

Nenda straight kwenye point, Mimi nitakujibu hapa, nimeishi Gauteng, Western Cape na Free state, hizo ni Provinces.
Umeulizwa unapoishi? Jikite kwenye swali kama lilivyoulizwa.
 
Back
Top Bottom