MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Umeandika vema. Mimi huwa nasema ukitoka nje ya TZ fungamana na wenyeji wa huko na sio kuwa karibu na wabongo wenzako. Mimi nikiwa nje ya bongo huwa sitaki mazoea na mbongo mwenzangu hata kiswahili siongei. Inasaidia kuepuka mambo mengi.Madogo wasela huko SA wanaenda kwa mkumbo na sio plan za maisha wanaitana huko wanapokeana kwenye ma gang vikundi vya kihalifu wizi uporaji makundi huko yana upinzani hata watz kwa watz huko wanachomeana na kuuwana.
Wengi tunaamini sauz maisha simple ila sio kweli masela wapo kule zaidi ya miaka 10 ukienda kwake utakuta anaishi geto moja na masela zaidi ya 7 ndani ya room moja
wachache sana ukute wamepaga kivyake anaishi pekeake au na mwanamke wake geto moja unakuta kuna watanzania wazambia humo humo wazimbabwe warundi humo humo utasema hayo ndio maisha mazuri?
Wanaogopa kurudi bongo sababu bado hawajatoboa wanaona aibu wanaona bora wakaze ila ndio ivyo wanaishia kutaabika kaburu hakuna maisha mazuri bila juhudi elimu na fani.
Vijana wa ma gang waporaji wavuta bangi madawa kule life yao ni mbaya mno bora hawa waokota makopo wa tz.
Madawa ya kulevya kula ukichukua mzigo ukijaribu kufanya utapeli kule kuna madon wa makundi kuna madon ambao ni wasauz watz warundi wazambia wazimbabwe na mataifa mengine so usnichi kule ni mwingi ukiishi kule ni kama upo vitani rafiki yako leo anakuibia mzigo anatokomea anakuachia msala ww.
Wanaoishi kule kisela asilimia kubwa wamepinda mwanao unaeishi nae anaweza kukugeuka mda wowote kuibiana wenyewe ni kawaida hii inatokana na mtu unaenda kule kwa matarajio makubwa na huna elimu huna fani unaishia kwenye magenge ya kihalifu.
Visa vingi vya kule ni madawa upinzani wa makundi kwenye biashara hii pia mademu kuchukuliana mademu kule ukiwa smart pia ni mbaya ukipenda dem kule dem wa msela nayo inaweza kukumaliza ukiwa ndani ya cirle ile ile ya aina ya maisha.
Sauz au Kaburu kwa wanavyoita wao ukitaka kuishi kwa amani nenda ishi kwa amani nenda ukiwa na fani elimu pia wapo watu wanaishi vizuri kwa elimu au fani nzuri
Fundi magari fundi umeme n badhi ya fani za kawaida kule ajira utapata vizuri tuu muhimu uwe na makaratasi yako yanasomeka vzr kabisa.
hawapo kwenye magenge wala makundi ukiishi kule sana sana ni salama zaidi ukiwa mbali na aina ya marafiki ambao ndio wako kwenye haya mgenge bora uwe lonely kuliko kuwa na rafiki mtanzania ambae heleweki mishe zake ni hatari.
Johanesburg pertoria cape town na durban ndio miji hatari zaidi.