Habari wanajukwaa kongwe kabisa,
Poleni na majukumu ya hapa na pale pia tusijisahau kuwa Adui yetu COVID-19 bado yupo, hivyo wazungu wanasema "Healthy is the new wealth" hivyo Afya ni mtaji wa kila mtu.
Naenda straight to the point.
Ni hivi: Mimi na mzee wangu ni mstaafu sasa ni miaka mitatu umepita tangu amalize pension yake na mimi nilibahatika kupata kamkopo chuo. Sasa tangu niingie mwaka wa pili huyu mzee wangu amekuwa hana hata haya anasema nimkopeshe, nimemkopesha karibia 45% ya hako kamkopo ka meal and allowance, lakini tena baada ya kusikia vyuo vinafunguliwa na mikopo itatolewa mapema, sasa anataka nimkopee tena zaidi ya sixty thousands nami na mipango yangu ya kuanzia kujitegemea hasa baada ya kuhamasika na Uzi mmoja unaosema "Ewe kijana, ulianzaje kukaa ghetto?"
Maana kwa Dodoma bado tuko hosteli, hivyo nili-plan nianze kununua items kidogo kidogo tu. Sasa hawa wazee wanatukwamisha. Pia, huwa nimkopesha hazirudi na ni ngumu sana kumdai kwa sababu yeye ndo kanisomesha: Ada, mahitaji, n.k
Sasa ni afadhali hata ningekuwa na kazi lakini sina. Kila nikitaka kumwambia ukweli roho inasita. Hapa niko dilemma ndo maana nikaamua nifunguke hapa walau naweza pata ushauri kuhusu hili suala, maana mipango yangu inarudishwa nyuma kweli.
Nawasilisha.
mkuu kwanza tambua fika kuwa boom kiuhalisia sio mkopo bali ni mkopo kwa jina tu boom kiuhalisia ni kama mshahara tu.
Kama ulikuwa unaamini kuwa boom ni mkopo erase it from you mind.boom ni mshahara wa chuo kwa kazi yako ya kusoma.
Kwa sababu unakopeshwa na serikali bila kutoa pesa yako mfukoni,alafu mwisho wa siku serikali hiyo hiyo inakuja kukupa ajira inakuambia tunakulipa laki saba ila laki mbili tunazikata kwa miezi 12 kwaa ajili ya zile pesa ambazo tulikuwa tunakupa shule.
Kwa hiyo unakopeshwa pesa na mtu alafu baadae mtu huyo huyo anakupa ajira anakuambia kile kipesa nakata humuhumu,hapo manake mwanzo alikukopesha mshahara wake.
Sasa jua kuwa huo ni mshahara,usiseme mkopo bwana,umekopeshwa sehemu ya mshahara wako.
Kwa hiyo ukilegalega na kugawa tu ujue kuwa unaugawa mshahara wako,baadae ukiajiriwa utakuja kupokea pesa ambayo ina makato ya hizo pesa zako ambazo ulikuwa unazigawa tu bila kujua kuwa ulikuwa ni mshahara wako.
Usicheze rafu mkuu,kuwa makini na mshahara wako huo.
Kuhusu mzazi mkuu kwanza kuna formula moja huwa naitumia mimi...
Ndugu yeyote akinikopa pesa bila mimi kumuanza basi simkopeshi yote,akinikopa 50000 namuambia mambo sio mazuri namuambia ntakukopesha 25000,hapo najua akinidhulumu inapunguza maumivu kuliko kunidhulumu 50000 yote.
Sasa mzee wako anapokukopa labda 350,000 mwambie "dah faza hapa nimepungukiwa hiko kiasi ila siwezi kusema uongo kuwa sina kabisa,hapa nina kama 150,000 ambayo niliiweka kama kaakiba cha emergence ila emergency zenyewe ndo kama hizi"
Kumbe wewe 350K unayo,sasa hapo ni ngumu kuisusia,hapo akitaka umpe hiyo hiyo 150,000 si utakuwa umeokoa 200,000.
Sas kutokurudishiwa 150k na kutokurudishiwa 350k ipi ina afadhali ?
Utajibu mwenyewe hapo.
Mkuu hakuna ubaya kuwakatalia wazazi wetu yale ambayo yanatuumiza sisi,bali ubaya ni kutoa makavu live kwa mtu ambaye wewe unakuja duniani yeye ana miaka 25 tayari au zaidi.
Jifunze kusema hapana kwa mzazi lakini hapana ya kuzunguka.
Wengi wetu tunakereka na wazazi wetu mienendo yao na tunaumia kwa sababu tunadhani kuwa kukataa ni lazzima useme live kuwa faza sitaki kukupa pesa no.kukataa unaweza kuzunguka zunguka lakini ikawa umekataa vilevile.
So jaribu kusema hapana kwa kuzunguka zunguka hivi kwa mzee,huyo ni mzee wako kumbuka,mzeee hata kama ni malaya epuka kumuambia maneno makavu.
Kuanzia leo epuka kutoa pesa yote,toa nusu mkuu..
Ukikopwa 50k toa 20k.it's better to lose 20k than losing 50k
Kumbuka kuwa BOOM ni shehemu ya mshahara wako,ukiamini kuwa ni pesa ya mkopo from no where basi utakuja kuelewa hapo mbele ukiajiriwa.
Alafu pia ukishamkopesha nusu au robo ya aliyokuomba,usimdai kwa sababu kumdai kuna hasara kuliko faida,tarehe za ahadi zikifika kausha,usimpigie simu kwa sababu pengine ayltaona kuwa unamkumbusha kishkaji,kausha kausha kausha moaka apige yeye.
Hapo itamfanya akumbuke kuwa unamdai na pengine ikasaidia kwake kutokukukopa tena kwa sababubanajua kuna deni analo kwako.
UFUPISHO.
ukikopwa,toa nusu au robo ya uliyokupwa,itamfanya mkopaji aamini kuwa nia ulikuwa nayo ila tu uwezo haukuruhusu,hivyo atakuelewa.
Mkatalie mzee wako kisiasa hivi kwa kutumia mfano wa njia ya hapo juu.
Boom ni sehemu ya mshahara wako.
Ukimkopesha mzazi pesa usimdai wala usimkumbushe,acha ajikumbushe mwenyewe wewe kausha.