Habari wanajukwaa kongwe kabisa,
Poleni na majukumu ya hapa na pale pia tusijisahau kuwa Adui yetu COVID-19 bado yupo, hivyo wazungu wanasema "Healthy is the new wealth" hivyo Afya ni mtaji wa kila mtu.
Naenda straight to the point.
Ni hivi: Mimi na mzee wangu ni mstaafu sasa ni miaka mitatu umepita tangu amalize pension yake na mimi nilibahatika kupata kamkopo chuo. Sasa tangu niingie mwaka wa pili huyu mzee wangu amekuwa hana hata haya anasema nimkopeshe, nimemkopesha karibia 45% ya hako kamkopo ka meal and allowance, lakini tena baada ya kusikia vyuo vinafunguliwa na mikopo itatolewa mapema, sasa anataka nimkopee tena zaidi ya sixty thousands nami na mipango yangu ya kuanzia kujitegemea hasa baada ya kuhamasika na Uzi mmoja unaosema "Ewe kijana, ulianzaje kukaa ghetto?"
Maana kwa Dodoma bado tuko hosteli, hivyo nili-plan nianze kununua items kidogo kidogo tu. Sasa hawa wazee wanatukwamisha. Pia, huwa nimkopesha hazirudi na ni ngumu sana kumdai kwa sababu yeye ndo kanisomesha: Ada, mahitaji, n.k
Sasa ni afadhali hata ningekuwa na kazi lakini sina. Kila nikitaka kumwambia ukweli roho inasita. Hapa niko dilemma ndo maana nikaamua nifunguke hapa walau naweza pata ushauri kuhusu hili suala, maana mipango yangu inarudishwa nyuma kweli.
Nawasilisha.