Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Vingi.
1. Makandarasi wa ndani walipwe ili kuongeza mzunguko wa pesa kwenye uchumi wetu wa ndani.

2. Miradi mingi ya serikali hasa mikubwa ihusishe wazawa zaidi ili pesa nyingi ibakie nchini ili kustimulates uchumi wetu kwa sababu kwa sasa pesa nyingi zinaenda nje kutengeneza ajira na maisha ya wananchi wa hizo nchi kuliko tanzania isitoshe miradi hiyo itachukua muda kuanza kulipa.

3. Siasa ni usindani, bila ushindani hakuna siasa, tuamue moja tunahitaji siasa za ushindani au za uteuzi, kama ni za uteuzi basi tuachane na vyama vingi, tuvifute.

4.
 
Ningelimwambia; Kuua upinzani na kuacha chama kimoja tu Tz sio afya ya maendeleo. Pili, Kuwa na mtizamo tofauti hakumaanishi kuwa sikupendi. Tatu, Kusiwepo na uchaguzi wowote wa mtu kupita bila kupingwa, yeye ni nani akose mpinzani?? Hata meno yasipoingana mdomoni nyama hailainiki hata uji usipoutafuna haushuki tumboni
 
1. Ntamshukuru kwa kurudisha heshima ya Mtanzania kupitia Passport mpya.

2. Ntamshukuru kwa kuleta Usawa baina yetu Watanzania

3. Ntamshukuru kwa Miundombinu yenye kuleta zaidi ya tija, kwani ina wakomboa Watu wengi hasa katika kusafirisha Mazao na Biashara mbalimbali.

4. Ntamuomba haruhusu Kilimo cha BANGE kwa ajili ya ku Export na uvutaji wenye kibali maalumu serikali iingize mapato na Wavutaji wa maana tupate utulivu.
 
Nitamuomba kazi... naona ana projects kibao zisizoenda vema kwa kukosa usimamizi. # experiencedpm #internationalexperience #revolutionofpmintz
 
Back
Top Bottom