Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

1. Aunganishe kila mkoa kwa SGR hata kule ambako reli ya kati haikupita. Atakuwa ameacha bonge la legacy na kusaidia uchumi wetu kwa miaka mingi ijayo. Hata ikibidi tufunge zaidi mikanda nile mara moja kwa siku, nitaunga mkono kama ni kwasababu nitaweza toka Mwanza kwenda kwetu Namanyere kwa kuteleza na kurudi siku hiyo hiyo. Na tunajua akiamua kitu, anaweza. Aamue SGR kila mkoa.

2. Afikirie na kutafakari kabla ya kuongea. Apime malengo ya anayotaka kuyasema, kama hawezi kuyasema mbele za Mungu, anyamaze.

3. Akitaka kutuonyesha jinsi alivyo na nguvu na mamlaka juu ya kila kitu, aache kutoa vitisho hadharani. Hakuna asiyejua nguvu ya ofisi aliyonayo. Kutoa vitisho kwa watendaji wake hadharani ili kuwatishia kutenda ayatakayo ni Ishara ya Udhaifu, na kukosa imani kuwa aliowateua tayari wanajua anauwezo wakuwatengua, na kwa uwoga wa kutenguliwa, watatekeleza ayatakayo.

4.Asiogope kuongea na wanahabari kama walivyofanya Mkapa na Kikwete kila mwezi kutuelezea na kutufafanulia sera anazotekeleza.

5. Asisahau kunyamaza mbele ya hadhara. Hana jipya analoelezaga. Tumeshayasikia yote na kurudiarudia haisaidii. Sio lazima kila akipewa kipaza sauti, aongee.

6.Afunge na kuomba Mungu amjalie Hekima na Busara japo kidogo tu.
 
Vizuri sana,ushauri mzuri mkuu!!..
8
Maisha ya mwanadamu ni ya kipekee sana, japo sote tunafanana kwa umbo la nje lakini kifikra, imani, itikadi na mitazamo tunatofautiana kwa kiwango kikubwa.

Kuna baadhi ya watu wamepata bahati ya kukutana na Rais wetu katika matukio, hafla na dhifa mbalimbali baadhi yao wakiwa wanasiasa, watumishi wa Mungu, wanamichezo, wanahabari, wafanyabiashara, watumishi nk.

Watu hao wote walikuwa na mambo mengi ya kuongea/kushauriana ambayo mengi tunayajua na mengine hatuyajui pia.

Ikitokea kwako unayesoma andiko hili ukakutana na Mheshimiwa na akawa radhi kukusikiliza, hoja, ombi, au ushauri utamwambia kitu gani ambacho unahisi kitakuwa na manufaa kwako na kwa jamii kwa ujumla?
ntamshauri asiendelee kugombea baada mihula yake miwili kumalixika
 
Nitamwomba anisaidie kunirudishia mali zangu nilizodhulumiwa!
Tz inaonekana bado kuna dhulma na ufisadi katika utoaji wa haki.

Kinamama wengi 'waliomwangukia' Magufuli malalamiko yao ni ya msingi na kweli.

Cha kujiuliza, viongozi wenye dhamana ya kutumikia wananchi pamoja na vyombo vya kutoa haki, wako wapi?

Saazingine wanapoitwa na kudhalilishwa kwenye kadamnasi, wala siwahurumii.
 
Nitamuomba anipe nafasi ya kazi nitumikie wananchi wenzangu. Pamoja na rais na kwa umoja, ukweli, nia na lengo moja tunaweza kuifikisha nchi mahali tunapotamani kuwa.
 
Anipe nafasi majukumu ya kulitumikia taifa hili tuu. Kuna mengi makubwa na mazuri anapanga yafanyike ambayo akinipa kazi ya kutekeleza sitamuangusha. Namwelewa sana my President💪
 
1. Aunganishe kila mkoa kwa SGR hata kule ambako reli ya kati haikupita. Atakuwa ameacha bonge la legacy na kusaidia uchumi wetu kwa miaka mingi ijayo. Hata ikibidi tufunge zaidi mikanda nile mara moja kwa siku, nitaunga mkono kama ni kwasababu nitaweza toka Mwanza kwenda kwetu Namanyere kwa kuteleza na kurudi siku hiyo hiyo. Na tunajua akiamua kitu, anaweza. Aamue SGR kila mkoa.

2. Afikirie na kutafakari kabla ya kuongea. Apime malengo ya anayotaka kuyasema, kama hawezi kuyasema mbele za Mungu, anyamaze.

3. Akitaka kutuonyesha jinsi alivyo na nguvu na mamlaka juu ya kila kitu, aache kutoa vitisho hadharani. Hakuna asiyejua nguvu ya ofisi aliyonayo. Kutoa vitisho kwa watendaji wake hadharani ili kuwatishia kutenda ayatakayo ni Ishara ya Udhaifu, na kukosa imani kuwa aliowateua tayari wanajua anauwezo wakuwatengua, na kwa uwoga wa kutenguliwa, watatekeleza ayatakayo.

4.Asiogope kuongea na wanahabari kama walivyofanya Mkapa na Kikwete kila mwezi kutuelezea na kutufafanulia sera anazotekeleza.

5. Asisahau kunyamaza mbele ya hadhara. Hana jipya analoelezaga. Tumeshayasikia yote na kurudiarudia haisaidii. Sio lazima kila akipewa kipaza sauti, aongee.

6.Afunge na kuomba Mungu amjalie Hekima na Busara japo kidogo tu.
Vizuri Mkuu
 
Kiukweli mm Nitaangalia tumbo langu tuuu,ni mwendo WA sifa tuuuu,kuanzia getini mpaka mlangoni naingia naimba Magufuli kwangaruuuuuu,nikiingia ndani ni mwendo WA mbele Kwa mbele,nachezaaa weee halafu napiga pushapu 10,nakaa kwenye kiti namwambia mzee lete mpunga nikawanyooshe nyumbu mtandaoni,baada ya hapo napiga selfie namwambia msigwa ahahakikishe amechukua picha vizuri na ananitumia mapema,
 
Anipe nafasi majukumu ya kulitumikia taifa hili tuu. Kuna mengi makubwa na mazuri anapanga yafanyike ambayo akinipa kazi ya kutekeleza sitamuangusha. Namwelewa sana my President[emoji123]
Ufanikiwa Madam,una tamani zaidi ungepewa nafasi ya kuwatumikia wananchi katika field ipi?.
 
Nitamuomba anipe nafasi ya kazi nitumikie wananchi wenzangu. Pamoja na rais na kwa umoja, ukweli, nia na lengo moja tunaweza kuifikisha nchi mahali tunapotamani kuwa.
Imetokea ukapata Mkuu utapendelea zaidi akupe nafasi eneo gani?.
 
Afute elimu bure
Vipi kwa wazazi/walezi wasio na uwezo kabisa wa kumudu gharama za kusomesha watoto mkuu, huoni kwamba ushauri wako utaathiri watu badala ya kuwafaidisha majority ambao ni watu wasio na kipato/kipato cha chini?
 
Back
Top Bottom