Hivi unapofumba macho bila kusinzia huwa unaona?

Twin hawa unaosema wana matatizo kwenye ubongo kwamba hawawezi kuona kitu chochote kile
Sio kwamba ni vipofu wa macho ila kwenye ubongo ndiyo kuna shida sio?
Unapofumba macho yako na kuhisi kama bado unaona au unajua kabati lilipo ujue ni ule mfumo wako wa ndani wa usalama unaoendelea kufanya kazi kimya kimya hata unapokuwa umefumba macho.
Kumbe ni mfumo wa usalama mi nilidhani ni kumbukumbu za ubongo
Au sijaelewa vizuri🤔 Aiseee kumbe ujue mtu akikaa sana kwenye mazingira kama hayo ataona vitu vya ajabu na anaweza kupiga kelele ni kama ubongo unakua unachoshwa na picha yenye mfanano mmoja Inamana ubongo ndio umetengeza picha kupitia wazo langu hapo kwenye nyama ya mbuzi niliongeza na juice nayo nimeiona 😅😅
Wow thank you twin
The Thinker 🧠
Cc: Marcostilone
 
Ukija hivi hua nakuona kama kijana mdogo mwenye nidhamu kubwa
Hahahaha we mdogo angu bwana😂
Enhee umesema ukifumba macho unaendelea kuona si ndio?
Kile unacho kiona ni halisi au ni ubongo unakutengenezea picha ?
Actually ni halisi,
Ile inakuwa ni nishati... Nishati inayotembea hasa kwenye zile nyama za kope na jicho lenyewe. Hapo sio ubongo. Si unasemea zile picha za kama rani rangi sio?

Ila Kuna ile kwamba umetoka kuona kitu hasa labda chenye mwanga mkali, pale inakuwa ni zile signal za mwanga zinakuwa bado zina exist so ukifumba zinakuwepo bado ndani ya receptor za jichoo. So utaendela kama kusense kile kitu uicho kwisha kukiona
 
Mkuu mbona kama unaelezea imagination na sio kile kitu mleta mada a namaanisha?

Sijakuelewa ukiposema eti mtu akiambiwa scenario au akiimagine kitu atakiona?

Hapo nakataa haoni kama picha halisi ataona kama picha ya mawazo sio halisi
 
Ahaaa asante kwa maoni kijana mdogo
Karibu tena kwenye mada zangu ukiwa msafi nje ndani
 
Twin hawa unaosema wana matatizo kwenye ubongo kwamba hawawezi kuona kitu chochote kile
Sio kwamba ni vipofu wa macho ila kwenye ubongo ndio kuna shida sio?
Twin hawa watu wenye hili tatizo macho yao huwa yanakuwa mazima kabisa, lenzi ziko safi, retina inafanya kazi, na ukiwapima macho na vifaa vya madaktari wa macho utaona kila kitu kiko sawa kabisa. Lakini bado huwa hawaoni kitu chochote, yani mbele yao huwa kuna giza tu. Unajua hiii inatokeaje? Ni kwamba eneo la nyuma la ubongo wao linaloitwa Primary Visual Cortex (V1) linakuwa limepata majeraha labda kutokana na ajali kubwa ya kichwa aliyowahi kupata, kiharusi , au labda ana uvimbe wa ubongo.

Sasa Kwa kuwa eneo la V1 ndio monita kuu ya uchakataji wa picha, hitilafu ikitokea hapo, mfumo mzima wa picha unafeli na kumfanya mtu kuwa cortically blind hata kama sensor za macho ni nzima kabisa.

Aiseee kumbe ujue mtu akikaa sana kwenye mazingira ataona vitu vya ajabu na anaweza kupiga kelele so kama ubongo unakua unachoshwa na picha yenye mnano mmoja
Ndio Twin mtu akikaa kwenye mazingira yenye giza sana kwa muda mrefu mfano vile vyumba wanavyo ingizwa watu kuteswa, lazima ubongo utachoka kwa kukosa visual data kwa sababu kawaida ya ubongo ni kuchakata taarifa mpya kila baada ya sekunde kadhaa, kwahiyo ukikaa bure tu hivyo lazima utaanza kutengeneza picha za kutisha, maluweluwe na sauti za ajabu ili tu ujishughulishe. Unaweza kuanza kupiga kelele ukidhani anaona mizimu, kumbe ni sensory hallucination tu kwa sababu umeunyima ubongo kazi ya kufanya kwa muda huo.
Inamana ubongo ndio umetengeza picha kupitia wazo langu hapo kwenye nyama ya mbuzi niliongeza na juice nayo nimeiona 😅😅
Hahaha huu ndio uthibitisho kuwa ubongo una the mind's eye.
 
Aiseee asante kwa maoni twin
Umeeliza vizuri na umeeleweka

Karibu tena The Thinker 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…