Kazi imeanza miezi 24 iliyopita na ndio maana imekuwa rahisi sana kwenye oparesheni 255
Juhudi ziongezwe zaidi, kazi hiyo ni ngumu sana kama unavyojionea mwenyewe hata humu JF; kunaibuka akina 'Lucas' wa kila aina kila siku.
Ngoja nitoe angalizo, pamoja na kwamba hili halihusiani na mada husika: CCM wana maumivu sana wakati huu, ni kama nyati aliyejeruhiwa tayari.
Mmekwishaambiwa Katiba hata hiyo mbovu ni vikaratasi tu.
Unapotaka kummaliza nyati aliyechini tayari, huendi bila ya tahadhari kwenda kummmaliza, unaweza kujikuta wewe mwenyewe unamalizwa.
Zile staha za hadaa baada ya kutofanikiwa, zitatupiliwa mbali, dalili zinaonyesha hivyo. Wale mabeberu wapiga kelele tokea mbali watapuuzwa wale, ikijulikana wakati ukifika watahaadiwa tena baada ya kupitisha uchafu wa kuwabakisha madarakani CCM.
Jichungeni sana, hasa huyo Lissu ambaye ni wazi ni mwiba wenye sumu kwa hawa watu.
Msiwape nafasi ya kuwaondolea matumaini tena waTanzania kuondoa balaa hili ambayo ni CCM.