Hivi watu wanaozama ndani ya maji na kukaa zaidi ya dakika 1 bila mashine wanatumia mbinu gani?

Hivi watu wanaozama ndani ya maji na kukaa zaidi ya dakika 1 bila mashine wanatumia mbinu gani?

Mimi huwa najaribu kukaa bila kuhema au kuvuta punzi nione tachukua dakika ngapi huwa najitahidi nafika sekunde 25.
 
Mimi huwa najaribu kukaa bila kuhema au kuvuta punzi nione tachukua dakika ngapi huwa najitahidi nafika sekunde 25.
Ukiwa chini ya maji hutakiwi kuvuta hewa(inhale) bali unatakiwa kutoa hewa(exhale)

Hewa unayoitoa ni ile hewa ambayo unaivuta kwa wingi then unaitunza kwenye mapafu halafu unaanza ku exhale kidogo kidogo ukiwa chini ya maji

Usithubutu kuvuta hewa(inhale)ukiwa chini ya maji you will choke to death
 
Heri ya sikukuu ya Iddi Jamani.

Tusahau kidogo mada ngumungumu na mada za mmu. Leo sikukuu angalau tupunzishe akili na kusahau kidogo shida.

Nimewahi kusikia kuna wajuvi wanaweza kwenda ndani ya maji zaidi ya nusu saa,Mimi sijawahi kushuhudia hiyo kitu Sasa sijui Kama ni kweli au story za vijiweni.

Mimi mwenzenu nikizama kwenye maji sekunde tano tu natoka naomba uji wa moto[emoji16].

Wenye maujuzi wa haya mambo hebu mje mtupe uzoefu ili siku na sisi tujaribu.

Kuna wavuvi nasikia wanazama hata saa nzima ndani ya maji anatega nyavu zake halafu anatoka juu ya maji yuko shwari utafikiri alikuwa ndani ya maji alikuwa anavuta sigara[emoji16].

Sijui kuna vimazingaziombwe kidogo hawa wavuvi wanatumia?'

Karibuni.
Hili suala la saa zima nabisha nimekaa pale weka simu Yako niweke simu yangu tukae pembeni tumshuhudie mtu anaezamia saa Moja sio saaa Moja hata dakika 15 tu nabisha [emoji23]
 
Kuna watu wanatumiaga dawa,kuna jamaa alikuwa anazama wanaweka sufuria la ugali mpaka wanasonga ndo anaibuka

Wale wavuvi unaowasemea ni mazoea tu,wanaweza kukaa chini ya maji kwa dakika 3 na anafukuzana na sato chini ya maji mpaka anamkamata,niliwah kujaribu lakin hata sikufanikiwa kufika chini kwenye hzo nyavu zao
 
Back
Top Bottom