Hizi bei za nyama kupandishwa kiholela nani wa kuwasaidia Wananchi? Sasa hivi kilo TZS 12,000/ Bodi ya nyama kazi yake nini?

Hizi bei za nyama kupandishwa kiholela nani wa kuwasaidia Wananchi? Sasa hivi kilo TZS 12,000/ Bodi ya nyama kazi yake nini?

Kuna mwanangu mmoja alikua anatafuta kazi akapewa dili ya kukamata mbwa wanaozurura mtaani awe anawachinja na kuwachuna ngozi alaf kichwa na miguu aizike mbali isionekane.
Mwana alikataa hiyo kazi ila naamini kuna mtu alipewa akakubali na sahivi kuna sehemu watu wanakula mishkaki ya mbwa
 
Nimepitia majukumu ya Bodi ya Nyama, nimeona ina majukumu manne (4) Kwa mujibu wa Sheria iliyoiunda Bodi yenyewe

Ila nimevutiwa na Jukumu lao namba 4, linasema "Kufanya ushawishi na utetezi wa wadau wa tasnia ya nyama"

Sasa hapo sijajua huo utetezi unafanywa Kwa Mlaji ama Muuzaji🙌

Wanasema mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama, hopefully wenye visu vikali watakuwa Wauzaji ndiyo ambao watakuwa wanatetewa badala ya kutetewa Walaji
 
Siku hizi kuna umoja wa kila sekta, pale Arusha kuna umoja wa wauza nyama, wanakubaliana kupanga bei wanavyotaka na ole wako uuse chini ya hiyo bei. Sasa hivi kila butcher Arusha kilo moja ni TZS 12,000/. Hakuna mamlaka au chombo cha kudhibiti huu upandishaji holela? Mlinzi wa mwananchi ni serikali, kwanini serikali isifanye utafiti ijui uhalisia wa soko, nyama ni kitoweo cha lazima sawa tu na mafuta. Tunaishauri serikali iunde mamlaka ya kudhibiti bei za nyama
Unalalama nyama kuongezwa elfu mbili, ila umeme magu alituachia tuvute kwa 27,000! Ila ukapandishwa mpaka 321,000! Hilo ulichekelea acha ccm itambe kila mtu atakula urefu wa kamba na alipopeleka mboga!
 
Siku hizi kuna umoja wa kila sekta, pale Arusha kuna umoja wa wauza nyama, wanakubaliana kupanga bei wanavyotaka na ole wako uuse chini ya hiyo bei. Sasa hivi kila butcher Arusha kilo moja ni TZS 12,000/. Hakuna mamlaka au chombo cha kudhibiti huu upandishaji holela? Mlinzi wa mwananchi ni serikali, kwanini serikali isifanye utafiti ijui uhalisia wa soko, nyama ni kitoweo cha lazima sawa tu na mafuta. Tunaishauri serikali iunde mamlaka ya kudhibiti bei za nyama
Soko La Utalii Arusha pamoja na Uwapo wa Viwanda Vikubwa vya Bidhaa za Nyama kama Eliya Food, Happy Sausage, Arusha Meat na Meat King Distributors LTD vinachangia Upandaji wa Bei Ya Nyama kiholela.

Kukua kwa Soko la Nyama Ya Tanzania Huko Uarabuni pia ni sababu kubwa ya kupanda bei ya nyama kwa sababu inakuwa adimu.

Waarabu wnanunua Wanyama wakiwa hai kwa wingi hivyo kusababisha upungufu mkubwa kwa soko la ndani.

Tabia ya Wamasai Kujilimbikizia Mifugo pia ni sababu moja wapo lakini pia uwepo wa Madalali katika minada ya mifugo ni sababu by ngine kubwa ya Ongezeko kubwa la Bei ya Nyama.
 
Kwako wewe unadhani bei gani ni sawa au unataka mwenye butcher mfugaji apate faida kiasi gani ?

Haya mambo kama Serikali inaona bei ni kubwa and it can do better basi ianzishe ranch ya taifa; haya mambo ya kupangiana bei sikubaliani nayo kabisa, ndio maana mimi ni muumini wa Social Market Economy... State UMMA unaweza kuwa na vitu vyake ila vyote kwenye Soko Huria, wakiona watu binafsi wanafanya cartel basi watakuwa na kitengo chao chenye kutoa bei rafiki....
hawajuwi kuwa Mama kafunguwq masoko ya Dubai na Saudi Arabia.
 
Kuleni panya, si nyama pia? Mliona Mtwara wanalalamikia bei ya nyama huko?

Wanapeleka panya na ndezi kama hawana akili vizuri.

Mipaka yote iliyojazana mitaani, kama huna pesa ya ng'ombe kula paka.
Ivi
Ndezi ni mnyama gani? Ikipatikana picha itapendeza, Nipo curious kumfahamu. Mimi nili dhania ndezi ni neno la kiswahili liki maanisha mtu mzubaifu/mshamba.
 
Back
Top Bottom